Kundi la Wachokonoz
i linaloundwa na Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wamekamatwa leo na watu waliodai kuwa ni askari polisi katika eneo la Maji ya Chai, wilayani Arumeru, Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao waliovamia nyumba ya Joseph Mrindoko walikuwa wamevalia kiraia na kujitambulisha kama Askari Polisi kabla ya kuwaweka chini ya ulinzi wahusika hao wawili.
Taarifa zinaeleza kuwa vifaa vyote vya kazi vya kundi hilo, vikiwemo kamera, kompyuta na nyaraka mbalimbali, vilichukuliwa na watu hao bila kuwasilishwa hati yoyote ya upekuzi au maelezo rasmi ya sababu ya ukamataji huo.
Hadi sasa, haijafahamika rasmi ni kituo gani cha polisi kilichohusika na tukio hilo, wala sababu ya ukamataji wa wachokonozi hao ambao wamekuwa wakijulikana kwa kazi zao za ufuatiliaji wa masuala ya kijamii na kisiasa.
Credit: Martinmaranjamasese