PreGE2025 Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

PreGE2025 Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kundi la Wachokonozi linaloundwa na Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wamekamatwa leo na watu waliodai kuwa ni askari polisi katika eneo la Maji ya Chai, wilayani Arumeru, Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao waliovamia nyumba ya Joseph Mrindoko walikuwa wamevalia kiraia na kujitambulisha kama Askari Polisi kabla ya kuwaweka chini ya ulinzi wahusika hao wawili.

Taarifa zinaeleza kuwa vifaa vyote vya kazi vya kundi hilo, vikiwemo kamera, kompyuta na nyaraka mbalimbali, vilichukuliwa na watu hao bila kuwasilishwa hati yoyote ya upekuzi au maelezo rasmi ya sababu ya ukamataji huo.

Hadi sasa, haijafahamika rasmi ni kituo gani cha polisi kilichohusika na tukio hilo, wala sababu ya ukamataji wa wachokonozi hao ambao wamekuwa wakijulikana kwa kazi zao za ufuatiliaji wa masuala ya kijamii na kisiasa.

Credit: Martinmaranjamasese
Tatizo na Shida iliyopo sasa ni kwamba Vibaraka watanganyika hususani Polisiccm sasa wanatumika na Mkoloni Kaburu Dikteta toka Zanzibar kuwatesa kuwaonea kuwateka kuwaua kuwabambikia kesi watanganyika wenzao kwa masilahi ya mkoloni mzanzibar, ingawa sasa mateso manyanyaso ni mradi Dili fursa ya watesi ibirisi chawaccm kupiga pesa kwa njia haramu za kishetani
 
We jamaa ndo unasema hujafurahishwa... kuwaamini watanzania inahitaji moyo maana kuna siku nimemsikia Chid Benz nae anadai hajawahi kuvuta bangi..
Kwani Mimi Sina wale naowakubali? Wakiingia kwenye matata nitaanzaje kufurahishwa?

Mimi ni mfuasi wa wachokonozi hata kama sikubaliani na Baadhi ya content zao ila mambo mengi nawaunga mkono.
 
ipo Bajeti Kubwa sana haramu imeandaliwa na wezi wa Taifa Akina Amos makala Bulembo chawaccm na wenzao akina Bashungwa IGP na akina Mbowe G55 na chauma ubwabwa ni pesa nyingi sana na laiti zingetumika kuleta maendeleo ccm ingependwa sana isingekuwa ikitumia gharama kubwa kukodi fuso mabasi yawasombee watu kwenye mikutano yao,
 
Hivi Hawa Wasiojurikana Huwa wapo Kila Mkoa...!?
Ama ni kikosi Kazi kinachosafiri Mkoa mmoja mpaka mwingine.....!?
Huzunguka si uliona Tundu lisu walimfuata Ruvuma wakamsafirisha hadi huko Dsm, ikumbukwe hicho ni kikundi cha ibirisi wa ccm kina Bajeti zake kubwa toka kwa Amos makala
 
Muuaji Mkuu kipindi Cha Meko ndio mtu wao WA maana pale Arusha.Kila siku wanamsifia ngoja yatawakuta.
 
Huzunguka si uliona Tundu lisu walimfuata Ruvuma wakamsafirisha hadi huko Dsm, ikumbukwe hicho ni kikundi cha ibirisi wa ccm kina Bajeti zake kubwa toka kwa Amos makala
Siamini kama Wanazunguka Kila Mkoa, naamini wapo Kila Mkoa.
 
We bwege hizo ni taaluma ya watu, we tii sheria bila shuruti. Ukikataa kukamatwa na jeshi la polisi unajiongezea kosa wataongeza nguvu litakuja karandinga na wale mliokwamisha zoezi lao mnaunganishwa na kesi wote korokoroni. Acha kuwaza upumbavu
We mbwiga
 
Katika Hali ya Kushtua Mchana wa Leo kumesambaa taarifa za kupotea kwa Vijana wawili walio kuwa wanafanya Vipindi vya majadiliano kupitia mitandao ya kijamii kama YouTube, TikTok etc wakijadili mambo tofauti tofauti.
Vipindi vyao vya kuvutia na namna Yao ya kuwasilisha n kujadili masuala mazito ya kisiasa na kiuchumi ndani na nje ya Nchi kwa namna ya Ucheshi ilikuwa ni burudani na kivutio kikubwa.
Kiukweli nimekuwa mfuatilia wao wa hivi Karibuni na nilivutiwa mnoo na Vipindi vyao lakini ghafla wapo kusipo Julikana ,🥲🥲
Wako wapi Wachokonozi..!?
images-1.jpg
 

Attachments

  • images-5.jpg
    images-5.jpg
    29.9 KB · Views: 16
  • images-4.jpg
    images-4.jpg
    22.9 KB · Views: 13
  • images-3.jpg
    images-3.jpg
    22.1 KB · Views: 18
  • images.jpg
    images.jpg
    11.1 KB · Views: 16
Back
Top Bottom