DOKEZO Kunguni wanatutesa Wanafunzi tunaolala kwenye mabweni ya UDOM

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wafanye hivyo wote maana ukifanya pekeyako haisaidii wale kunguni wanatapakaa.Hili tatizo kubwa,hata kile Chuo kikubwa dar nenda hostel za mabibo shida ya kunguni ni kubwa.Inasikitisha sana miaka ya nyuma Vyuoni kulikuwa hakuna mambo haya.
 
Kunguni ni mambo ya kawaida mama samia mwenyewe ana chawa.
 
Unawajua kunguni wewe?
Wanakaa kwenye kuta pia. Wakipuliza chumbani kwao watakuja wengine toka vyumba vingine.
Hapo lazima Wapulize jengo zima kila kona.
Wapulize vitanda na magodoro pia.
Wapulize majengo yote.

Hiyo kazi ifanywe na taasisi inayomiliki au inayo simamia majengo hayo.
 
Hivi mlipokuwa likizo walikuwa wanaishije hao kunguni? Isije kuwa mmetoka nao huko vijijini kwenu. Kwani kunguni anaishi muda gani bila kunywa damu?

Edit: eti jamaa wanaweza ishi hadi siku 400 bila kunyonya damu!!! Natengua kauli.
 
Viongozi wengi wa umma wala rushwa
 
Poleni sana.. huyo mdudu ni matesoo.
 

Kuna shehe ubwawa alisema kunguni ni pigo la allah[emoji28].
 

Kunguni dawa sahihi na ya uhakika ni maji ya moto.
 
Mnaji9na wafaransa wenyewe
 
Sijawahi kuona kunguni/chawa siwajui. Lkn nasikia wanasababishwa na uchafu.
 
Watasingiziwa wafaransa na spaniola huku wahuni wakiwa kitengo cha procurement
 
Wafanye hivyo wote maana ukifanya pekeyako haisaidii wale kunguni wanatapakaa.Hili tatizo kubwa,hata kile Chuo kikubwa dar nenda hostel za mabibo shida ya kunguni ni kubwa.Inasikitisha sana miaka ya nyuma Vyuoni kulikuwa hakuna mambo haya.
Mkuu, hao kunguni ni mtu unatembea nao, hawahami toka room moja kwenda nyingine,

NB. Nimesoma UDOM, nimekaa hapo COED anaposema mtoa mada, nishawahi kutana na adha ya kunguni room kwetu, (room za majirani hawakuwa nazo)

Tukapiga usafi wa maana wa vitanda, mara moja tu na mwaka mzima tukaishi vema bila kuandika uzi jf au X,
Sijui kizaz cha sasa kimetoka ufaransa πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kinataka Kunguni tu serikali iingilie kati πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ sijui exile mtapigaje madogo na kunguni hao πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Unaijua UDOM ilivyo? Hao kunguni jamaa kakuza tu tatizo, hawapo vyumba vyote + kunguni hawatoki chumba kimoja kwenda kingine, walikuwa room kwetu walitutesa ila hawakwenda room yeyote ya jirani,

Kijana aache uvivu, afanye usafi, hata kama wapo kwenye kuta, kuta za UDOM ni rahisi kisafishika,

Btw hata uongozi huwa hawapigi dawa jengo zima, wanapiga tu vyumba vyenye kunguni sugu ambavyo vinaweza kuwa viwili jengo nzima
 
Hivi mlipokuwa likizo walikuwa wanaishije hao kunguni? Isije kuwa mmetoka nao huko vijijini kwenu. Kwani kunguni anaishi muda gani bila kunywa damu?

Edit: eti jamaa wanaweza ishi hadi siku 400 bila kunyonya damu!!! Natengua kauli.
Mhhhh source ya kuwa wanakaa siku 400?
 
Mambo mengine ni kuchoshana tu. Hao kunguni mmewaleta wenyewe kutoka majumbani kwenu, halafu mnakuja kuusumbua uongozi wa chuo kuwatokomeza!!

Yaani watu wanapambania elimu yenu, wanapambania usalama wenu hapo chuo! Bado mbawabebesha tena mzigo wa kupambana dhidi ya kunguni, mliokuja nao kutoka majumbani kwenu!!

Kama vipi jichangisheni ili mpate dawa ya kuwaua. Inauzwa shilingi elfu 6 tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…