Kuning’iniza funguo za gari kiunoni kama tunguli ni ushamba uliopitiliza

Kuning’iniza funguo za gari kiunoni kama tunguli ni ushamba uliopitiliza

Suruali ina mifuko, wekeni funguo mfukoni jamani. Unaponing’iniza kwa sababu ya kuionesha kwamba umekuja na gari nahisi ni ushamba fulani wa kiwango cha SGR.
Watu watajuaje kama na wewe una ndinga...?
 
Huku Mahaha hakuna hata anayejua funguo za gari zinafananaje.

Ningekuwa naning'iniza,kuna mazingira zinasaidia.
 
mtu unakuwa na mafungua mengi funguo za gari, nyumba ,hadi ukitembea tunaskia vyuma vinagongana kumbe mtu anafata gari parking
 
Ni mmojawapo ya utunzaji mzuri wa funguo mfukoni inaweza ikaanguka au ukijisahau ukaweka mfuko wa nyuma ukaikalia.
Mimi nawashangaa sana wale ambao hawana Magari ila ananinginiza funguo ya gari
 
New money shouts.
Kiswahili chake
Maskini akipata matako hukia mwatah.
 
Tafuta hela brother mifuko nikwajili yakuweka hela tu
 
Ipo siku utajiona umeloki gari kumbe funguo ushajibinyeza kitu kiko wazi, hapo ndo utaelewa kwanini watu huzishika

NB: Za rimoti pekee
 
Nimejaribu kuchunguza watu wenye magari ya thamani za kutupwa km Mo Dewji, Manji et al.. huwa funguo wananing'iza upande upi wa suruali nimekosa. 😇😇😇
 
Back
Top Bottom