Kunuka kikwapa: Fahamu chanzo, tiba na namna ya kuepuka tatizo

duh, pole kwa kweli una tatizo. Kama wadu walivyosema
1. Hakikisha kwapa lake ni safi kama la mtoto
2. anaoga angalu mara 2, asubuhi na kabla ya kulala au unapotaka kum-consume
3. Ndimu, vinegar hata udi wa kufukiza
4. Deodrant/body mist
5. Perfume ila sio Simla

akichanganya hizo teknik hapo juu zitasaidia
 

Kuna mbaba huwa anakuja shati limelowa sehemu kubwa kweli upande wa kwapa, akishakaa baada ya muda utaisikilizia harufu yake ndugu. Mie huwa namuonea huruma kweli, manake hiyo nayo ni shida! Ningekuwa na mazoea nae kivile ningemuonesha huu ujuzi, sema ni mtu mzima ambae nimezoea tu kumpa shikamoo!
 
Caution: kamwe sirudie nguo bila kufua. Na asitumie deodorant kama hajatoka kuoga. Kuna watu wana tabia ya kutembea na deodorants kwenye handbags sijui wanatumiaje!

mkwe kama hiyo harufu ya kwapa kama ya kishindindo ajue tiba imeshindikana.
 
mimi kwa uzoefu wangu

watu wenye tatizo la kunuka midomo,kikwapa na miguu

tatizo lao sugu ni kuwa 'hawapati' watu wa kuwaeleza ukweli...
wengi hawajijui...


Kweli kabisa mkuu,

Watu wengi hawana watu wa kuwaambia. Na mie naamini kuambiwa ni tiba ya kwanza kabisa...Unashangaa mtu ana mke halafu saa 2 asubuhi anatoa harufu mdomoni utadhani ana swaumu na ni saa 11 jioni!!
 

Kaka leo umegawa ma ujuzi kweli kweli,

Hivi vitu inabidi watu wavipe kipaumbele sana. Vinginenvyo ndio mtu anakutana na kesheshe ya kukimbiwa na watu kila anapofika. Yaani mtu unakuta watu wamekaa kikundi ila mara tu baada ya kufika wanaondoka mmoja mmoja kama wanao wahi kula pilau kwa siri!
 


Duuu...Hii lugha imenikumbusha mbali sana..Enzi zile za form 2, mtu ukishanyoa pank na kuvaa suruali ya miguu ya kuku (don't touch my shoes), lazima lugha ibadilike aisee!
 


lol......umenikumbusha kuna jamaa college alikuwa
ni mmbea mpaka wanawake wanamuogopa ingawa yeye ni kidume...
sasa ilifikia hatua kama mmekaa sehemu mnapiga story....akija yeye
automatically watu wanaishiwa cha kuongea...lol yaani ghafla kunaingia ukimya lol
 

Unajua The Boss,

Hakuna mtu wa muhimu kama mke/mme linapokuja suala la kuelezana mambo ambayo hakuna mtu mwingine anaweza kukwambia. Ndio maana watu wakioa/olewa wanabadilika sana. Mara nyingi wanaume ndio wanabadilishwa hadi mavazi. Pia wengine hufundishwa hadi kufua chupi na kuosha kikwapa!

Ni muhimu sana mkuu!
 


kabisa aisee
na ndo mafunzo hasa ya ndoa yalivyokuwa zamani...
sasa siku hizi ndo unasikia mtu anasema
'nimemkimbia kwa sababu hii na hii' unajiuliza sasa kama sio wewe mpenzi wake wa kumwambia..
ataambiwa na nani??

ndo maana wanaume akishaoa ndo anakuwa 'more handsome' na wadada wengine
wanajiuliza mbona sikumuona zamani...kumbe kapata 'anaemfaa'....
 
ANTI-PERSPIRANTS SI NZURI KWA AFYA YA BINADAMU NA ZINASABABISHA MADHARA MAKUBWA KAMA BREAST CANCER COZ ZINAZUIA JASHO KUTOKA. PIA ZINA Alluminium AMBAYO SI NZURI KWA AFYA YA BINADAMU
 

Mbona wale wenzetu wa upande wa pili mambo yao mara nyingi huwa mabaya baada ya ndoa?? Au ni utaratibu tu wa kubalance equation???
 
Mimi nadhani mwambie azidishe round za kuoga.Kama alikuwa anaoga mala moja kwa siku basi at least iwe mala tatu kwa siku.Japo hakiwezi kwisha lakini kitapungua

paka kwenye kikwapa ndimu au limao baada ya kuoga

Niliwahi kusikia kuwa maji ya limao ni dawa nzuri


mwambia apake vitunguu kabla ya kulala na akiamka baada ya kuoga.


Tumia Deodorant, au pakaa maji ya limao (hii ni kwa mujibu wa Jf Doctors)

Mwambie achukue pamba awe analowesha kwenye spirit halafu aweke kwenye hayo makwapa yake na abana kwa dakika kazaa. Fanyeni hivyo kila siku kwa muda wa wiki 2.
Dah!! Sijui hapa utachukua ushauri wa nani..:lol:
 
Msisahau pia maji katika mwili ni kitu muhimu sana, lita tatu hadi nne kwa siku, punguza spicy foods, caffeine na alcohol, au chochote kinachodehydrate mwili wako. A dehydrated body smells bad especialy kikwapa kinachoacha vitu vyeupevyeupe kwapani, au vinavyoacha alama ya njano kwenye shati jeupe.

Kunywa maji kadri uwezavyo, kiyoyozi nyumbani kama unaweza kinasaidia, tembea sehemu za vivuli au kaa ndani bila nguo na ujipepee.

Whatever it takes not to dehydrate urself.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…