Kuoa mwanamke masikini

Kuoa mwanamke masikini

Wakuu hii ishu ya kumuowa mwanamke masikini asiekuwa na kila kitu mnaichukuliaje, kuna wanaume wengine kama mimi kigezo cha sura na tako wala sikipi uzito.

Mimi ni mpambanaji na kiuchumi walau niko vizuri inakuwaje nioe mwanamke masikini? yaani siku anakuja kwangu anakuja na kabegi kake ka nguo tu.
Mwanamke maskini mkimbie kama kama na wewe ni maskini.. ila kama weye poa vuta tu jiko
 
Mimi sioni shida ya umasikini wake ila tatizo linakuja kwenye familia yake kujiweka mabegani mwako.

Unamuoa yeye na familia yake nzima, uwasomeshe wadogo zake, watoto wa ndgu zake, uwajengee wazazi wake nk hilo ndo janga ila kama ni yeye tu mbona unammudu vizuri.
Niko na mawazo yako, ila naongezea uelewa hapo.
Maskini kabisa na mwenye uwezo wa kati wana uelewa tofauti kutokana na kwao walitokaje.
Mara ya mwisho naachana na demu maskini alicarry somo akarudia semester nzima ila wazazi wake wakagoma kumlipia na wakagoma kumlipia kila kitu sijui kodi na matumizi.

Niliachana naye alipomaliza masomo yake, haikuniingia akilini niwe na mtu wazazi wake wamemtupa vile. Na bado akili yake ilikuwa ina umaskini ndani yake, na akaanza kupenda hela kuliko mapenzi yenyewe.
Nikajiachia na mtu ninayejua kuhusu hela haihusiki, hata kama natoa ila sio niwe na mtu naogopa hata kumwambia plans zangu asijue nina hela kiasi gani asije zalisha shida za kutosha. Unakuwa na mtu unaogopa hata kumsimulia habari njema ulivyopata deal fulani la hela
 
Ndoa sio kitu Cha kukurupukia , tuliza akili ufanye maamuzi sahihi ila kumbuka kwenye suala Zima la ndoa UPENDO, UAMINIFU na HESHIMA ndo nguzo.

Kama kweli unampenda huyo mwanamke na yeye pia ameonyesha Nia ya dhati ya kuishi nawe Basi usisite kumuoa.Usijali kuhusu Hali Yake ya kiuchumi.
 
Ukijaribu kutumia akili. Utaogopa kumuoa maskini.

Ndoa ni muunganiko wa familia.

Ndoa humuoi mtu mmoja bali ni familia nzima yake wanakuwa ndugu zako.

Maskini wengi ni wavivu na wana amini sana ushirikina na miujiza.. hatari sana kuwa na ndugu wenye tabia hizi.

Pia watoto utakaowazaa watakuwa na wajomba, mama wadogo na wakubwa maskini pia.

Sizani kama ni sahihi kuwatafutia watoto wako ndugu wapya maskini
 
........wengi wetu huwa tunadhani vigezo vibayan ktk kuchagua mwanamke ni shepu na sura tu, lakini pia wengi wetu tunadhani kwamba kuoa mwenye kazi au elimu kubwa ndo ujanja, wengi wetu huwa tunadhani taasisi ya ndoa inaendeshwa kidini ndio maana ndo upendo ndani ya ndoa umekufa kwa sababu ya kuchaguana kwa itikadi za kidni, wengi wetu huwa tunadhani ndoa ni taasisi ya kiuchumi ndo maana upendo haupo tena coz watu wanachagua business partner badala ya love partner, wengi wetu hudhani.......endeleza comment hii kwa kuanza na neno wengi wetu hudhani.........
Wengi wetu huingia kwenye ndoa kwa kigezo kwamba umri umewatupa kwahyo wanaingia kwa mkumbo ilhali hamna mapenzi ya dhati baina yao
 
Wengi wetu huingia kwenye ndoa kwa kigezo kwamba umri umewatupa kwahyo wanaingia kwa mkumbo ilhali hamna mapenzi ya dhati baina yao
.......ni kweli bro, tunapaswa kuelewa hakuna muda sahihi wa kuoa ila kuna mwenzi sahihi wa kuoa, atukuja lini ktk maisha yako hilo ni la Mungu, na ndo huwa wakati sahihi......
 
Back
Top Bottom