Kuoa mwanamke masikini

Kuoa mwanamke masikini

Wakuu hii ishu ya kumuowa mwanamke masikini asiekuwa na kila kitu mnaichukuliaje, kuna wanaume wengine kama mimi kigezo cha sura na tako wala sikipi uzito.

Mimi ni mpambanaji na kiuchumi walau niko vizuri inakuwaje nioe mwanamke masikini? yaani siku anakuja kwangu anakuja na kabegi kake ka nguo tu.
Mkuu kigezo cha utajiri kwa mwanamke sio cha msingi kwa kuwa huyo sio partner wako wa kibiashara bali ni partner wako wa maisha na wewe mwanaume ndiye unayepaswa kuhudumia familia. Kuangalia kigezo cha utajiri/umaskini wa mwanamke ni kukimbia majukumu yako. Acha hizo mkuu.
 
Tulianya kukosea tulipo acha tamaduni na mila zetu,ila tukakosea zaidi baada ya kuingiza maswala ya usawa wa kijinsia na 50/50 ktk mitaala ya shule. Yaani hapo ndipo tukaharibu zaidi kwani siku hizi hata kimitizamo watoto wa kiume wana mitizamo fulani kama ya wanawake.
 
Huyo ndiyo mke mzuri wa kuanza naye maisha! Mfundishe kazi au mpe mtaji uone.
Utakuja kushukuru hapa JF.
 
Yaani mtu kazaliwa na baba masikini Alie mchagua mamake akiwa masikini wakamzaa nakumlea wakiwa masikini Leo anawanyanyapaa masikini,,,,,hivi kuwa masikini ni chaguo la mtu au ni vitu huja automatically?? Hili jukwaa niliambiwaga nikwaajili ya magreetthinker Sasa vijana wenye uharo kichwani mmetoka wapi???? Kuna watu unaweza ukawa unatamani kuwa kama yeye kumbe masikini ya mngu niwakumhurumia
 
Mkuu hapo umeongea point sana. Shida Christian inapotoshwa Sana na wamagharibi Feminists Sana..!
Tatizo mnachanganya mila na dini hivi ni vitu tofauti. Kwa jamii zetu za kiafrica kila mtu ni mtafutaji, hakuna mwanamke wa kiafrika ambaye anakaa tu ndani aletewe. Kama ni shamba ni wote, baba atatangulia na mama anakuja baadae na chakula na kusaidia kidogo shughuli za shamba. Umasikini ni janga la kimataifa ndio maana kuna mkakati na malengo ya kidunia kuutokomeza kabisa.

Hakuna binadamu yoyote anaupenda Umasikini ni bahati mbaya tu watu wamezaliwa kwenye hayo maisha. Na ni wa kuukataa kwa nguvu zote.

Halafu kuoa au kuolewa na maskini sio kigezo cha kupata heshima ndani ya ndoa. Heshima inajengwa kupitia malezi na watu ambao unahusiana nao. Na kila mtu atafute vigezo vyake wakati anataka kuoa iwe pesa etc kama anaona vitampa amani. Pesa ni muhimu sana kwenye haya maisha . Na sisi wanawake tusipeleke mbususu tu kwenye mahusiano au ndoa maana kuna leo na kesho, ni muhimu kujenga ustawi wa familia pamoja. Tuweze hata kununua luku sio umeme au chumvi inaisha unasuburi mume arudi jioni.
 
Hapo umenena vyema kabisa dadaa..![emoji253][emoji257][emoji1651][emoji255][emoji259]yako chukua
 
Wewe huna hela acha kurukaruka kama maharage. Ukioa mwanamke hata kama ana kazi nzuri wala hupaswi kujua anapokea kiasi gani kama kidume unapaswa kusimamia shoo zote za msingi kwenye family. Mshahara wake wacha akavae mawigi ya laki3 huko. So same wise hata kama hana pesa mtafutie duty ya kufanya ili nae asimame au kama hana interest weka ndani alee watoto maana nayo nikazi pia.
 
Hii ni kwa wale tuliotokea familia za kawaida na tuna wanaume middle class tu sio matajiri.....
Aisee mwanamke mwenye watoto unawezaje kuenjoy maisha ya ndoa huku ukijua mumeo asipokuwepo huwezi fikia hata 50% ya maisha anayohudumia?
Pesa yangu iombwe isiombwe ila for as long as najua nna kipato changu binafsi ambacho kinaweza sitiri familia kichwa wa nyumba akipata changamoto (not necessarily death) basi hata majukumu ya kifamilia yanakua smooth.

Ewe mwanaume ambae ndo kwanza unatafuta maisha, ukiwa na mwanamke ambae chumvi mpaka akusubiri, kikoba mpaka abane hela ya matumizi utachelewa sana.

Maisha ya sasa hivi, baba pambania mambo makubwa makubwa kama ujenzi, family investments, bima za afya....
Mambo madogo madogo mama amalize kama unaona a too well off woman will hurt your ego.
 
Mwanaume anatakiwa amfungulie mkewe biashara/ kampuni
 
........wengi wetu huwa tunadhani vigezo vibayan ktk kuchagua mwanamke ni shepu na sura tu, lakini pia wengi wetu tunadhani kwamba kuoa mwenye kazi au elimu kubwa ndo ujanja, wengi wetu huwa tunadhani taasisi ya ndoa inaendeshwa kidini ndio maana ndo upendo ndani ya ndoa umekufa kwa sababu ya kuchaguana kwa itikadi za kidni, wengi wetu huwa tunadhani ndoa ni taasisi ya kiuchumi ndo maana upendo haupo tena coz watu wanachagua business partner badala ya love partner, wengi wetu hudhani.......endeleza comment hii kwa kuanza na neno wengi wetu hudhani.........
Wengi wetu tulikua hatujui kuhusu haya hadi tulivoipitia comment yako
 
Wakuu hii ishu ya kumuowa mwanamke masikini asiekuwa na kila kitu mnaichukuliaje, kuna wanaume wengine kama mimi kigezo cha sura na tako wala sikipi uzito.

Mimi ni mpambanaji na kiuchumi walau niko vizuri inakuwaje nioe mwanamke masikini? yaani siku anakuja kwangu anakuja na kabegi kake ka nguo tu.
wakati unamchumbia hukujua kama hana kitu zaidi ya tako tu na mahips, tena we shukuru anatako na mahips wengine hawana hivo vitu ni hazina, acha kulalamika mtoto wa kiume tafta hela tunza mkeo
 
We mwenyewe tajiri? Una nini? Ukute una kajumba na kagari unajiita tajiri
 
Mimi sioni shida ya umasikini wake ila tatizo linakuja kwenye familia yake kujiweka mabegani mwako.

Unamuoa yeye na familia yake nzima, uwasomeshe wadogo zake, watoto wa ndgu zake, uwajengee wazazi wake nk hilo ndo janga ila kama ni yeye tu mbona unammudu vizuri.
HALAFU BAADA YA KUFANYA YOTE HAYO ANAKUSALITI MCHANA KWEUPE
 
Back
Top Bottom