Kuoa wanawake wawili au kuwa na watoto wa mama tofauti kwa dunia ya leo ni kujitafutia matatizo

Kuoa wanawake wawili au kuwa na watoto wa mama tofauti kwa dunia ya leo ni kujitafutia matatizo

Manzile

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2020
Posts
717
Reaction score
1,933
Wanaume wenzangu, dunia imeshabadilika. Leo ukiwa na watoto wa mama tofauti kwenye familia yako jua unatengeneza kaa la moto baadae na kuwa na wake wawili ndio kabisa kwa asilimia kubwa unakuwa unajitengenezea jehanamu yako mwenyewe. Nimeshuhudia familia nyingi sana zinavurugana mpaka kufikia uhasama wa kufikia kuuana.

Wewe baba ukitaka udharaurike baadae na ukose msaada kwa wanao oa wake wengi halafu ufilisike uzeeni, kwa maisha ya sasa hakuna rangi utaacha kuiona kila mtoto atakuwa busy na mama yake na sio wewe tena na ukiwa na mali watakuheshimu ukiwepo ila ukifa tu amini utakuwa umeacha vita kubwa sana

Kama umeoa, Ikatokea umetalakiana ama mmoja katangulia na kuna watoto, kwa mimi binafsi kwa mazingira yalivyo sasa sioi tena, kama ni wanawake wa kutuliza mzuka wapo wengi tu.

Sitaki kuchimbua ndani zaidi, leo naishia hapa
 
Aisifiaye mvua ujue imemnyea, ni ayo tu ila nimekuelewa sana
Wala usije kudhani ni mimi mkuu, mimi bado kijana kabisa. Hiki ninachokiongea nimekiona kwa watu wanaonizunguka na mtu anakupa sababu za msingi kabisa kwa nini hataki kumsaidia baba yake na badala yake kawekeza kwa mama
 
Nimekupata vizuri sana mkuu na ayo mambo chanzo ni baba wanaume wanapenda sana kutia tia mimba matokeo yake uzeeni sasa watoto kibao maugonvi uanza
 
Wala usije kudhani ni mimi mkuu, mimi bado kijana kabisa. Hiki ninachokiongea nimekiona kwa watu wanaonizunguka na mtu anakupa sababu za msingi kabisa kwa nini hataki kumsaidia baba yake na badala yake kawekeza kwa mama
Pole mkuu hiyo ndiyo dunia vumilia tu
 
Yani wewe unakuja na matusi halafu unaniita mjinga sawa bhana ngoja tuone mjinga ni nani !

Nazidi kukupa pole kwa yaliyokukuta.
Watu mna akili za kijinga😀😀, mimi nimeleta mada..sasa usitake kulazimisha kunivisha uhusika wakati ni mambo yapo kwenye jamii
 
Hata Hao wenye watoto kwa wanawake tofauti kabla walikuwa wanamatamanio kama yako lkn wakajikuta ndo hivyo tena! Navyokuona wewe utazaa na wanawake zaidi ya 5 asaiv huwez kuelewa sababu bado ni mvulana
 
Mwambie wewe mkuu mm kaniita mjinga.
Hata Hao wenye watoto kwa wanawake tofauti kabla walikuwa wanamatamanio kama yako lkn wakajikuta ndo hivyo tena! Navyokuona wewe utazaa na wanawake zaidi ya 5 asaiv huwez kuelewa sababu bado ni mvulana
 
Wala usije kudhani ni mimi mkuu, mimi bado kijana kabisa. Hiki ninachokiongea nimekiona kwa watu wanaonizunguka na mtu anakupa sababu za msingi kabisa kwa nini hataki kumsaidia baba yake na badala yake kawekeza kwa mama
anatoa sababu gani?
 
Hahah mzee kuzaa na watoto kukusaidia uzeeni sio jukumu lao hata hao wa mama mmoja pia wanaweza kukusahau tu,kusaidiwa uzeeni ni bahati tu.

Case uliyoiongelea wewe nimeiona kwa mwanaume ambae hakuhusika kwenye kuwapa mahitaji na kusimama kama baba kwenye maisha ya watoto.
 
Bado mvulana huyo maana humu tumevamiwa na watoto wa primary
Namwambia hivi kama kuna wanawake anawachukulia ni kwa ajili ya kutoa mzuka atakuja kujikuta tayari keshazaa na wanawake watano huyu, maugomvi mbeleni huja kama hukuweka mazingira ya Upendo kwa watoto mapema kabla hawajajitegemea
 
1:-Acha uoga..

2:-Lazima uwe na negative perception kwasababu umejifunza kwa waliofeli na hukutaka kujua kwanini walifeli...hvyo badili mtazamo wako,
...What man think about come about..

3:- Adi apo inaonyesha kabsa hujui nn maana ya ndoa,kaa chini dogo ujifunze kwa waliofudhu haya mambo.

La mwisho nakuachia dogo,wanaume kamili huwa tunatumia akili kuishi na wanawake ndomana wafalme na mababu zetu walikuwa wanaishi nao adi vifo vyao...Sasa wanaume sa hv wengi suruali huwa wanatumia hisia kuoa ndo Mana kucha mnalialia.

Don't let your emotional control your thinking...be careful dogo
 
Shida ni malezi. Kama umeoa mwanamke zaidi ya m'moja basi jitahidi kuwaleta wanao pamoja na kuwafanyisha shughuli pamoja..... Wajenge watoto wakubwa kuwahudumia na kusaidiana na wadogo zao, mfano wakati wakulipa ada, baba mtume mtoto mkubwa akamlipie mdogo wake..... Shopping mtoto mkubwa akawahudumie wadogo zake na kuwasikiliza wanataka nini.

Mkemee pale anapomuonea mdogo au mdogo anapomkosea mkubwa adabu hii itawajenga kuheshimiana. Usiwaruhusu mama zao kuaanza kuwapa mafunzo nje ya upeo wako mfano namna ya kuishi na wenzao au namna ya kupenda na kufanya mahusiano maana hawa wanawake wa siku hizi ni tofauti sana na mama zetu..... Hawa wa sasa ni mitambo....
 
Ni kweli kuna balaa kubwa sana,ila utawezaje kuishi bila ya mwanamke,shida yako ni kuchukulia kuwa mwanamke unamuoa au kuishi naye kwa ajili ya ngono,kuna zaidi ya hapo mkuu,kuna umri utafika utagundua faida za kuishi wawili yaani mume na mke na sio tena kuokoteza wanawake kila kukicha,cha muhimu ni kuomba upate mke mwema vingine vyote vitajipanga sawa...
 
Back
Top Bottom