Kuoa wanawake wawili au kuwa na watoto wa mama tofauti kwa dunia ya leo ni kujitafutia matatizo

Kuoa wanawake wawili au kuwa na watoto wa mama tofauti kwa dunia ya leo ni kujitafutia matatizo

maisha ya zamani sio kama sasa usikariri..naungana na jamaa ukitaka upate tabu sasa oa wake wawili.

Acha uoga mkuu..
Sasa wawili tu unaoga je,hao wanne utawaweza kweli... ahahaaa

Anyway, people do shape their life through their thoughts..
 
Wanaume wenzangu, dunia imeshabadilika. Leo ukiwa na watoto wa mama tofauti kwenye familia yako jua unatengeneza kaa la moto baadae na kuwa na wake wawili ndio kabisa kwa asilimia kubwa unakuwa unajitengenezea jehanamu yako mwenyewe. Nimeshuhudia familia nyingi sana zinavurugana mpaka kufikia uhasama wa kufikia kuuana.

Wewe baba ukitaka udharaurike baadae na ukose msaada kwa wanao oa wake wengi halafu ufilisike uzeeni, kwa maisha ya sasa hakuna rangi utaacha kuiona kila mtoto atakuwa busy na mama yake na sio wewe tena na ukiwa na mali watakuheshimu ukiwepo ila ukifa tu amini utakuwa umeacha vita kubwa sana

Kama umeoa, Ikatokea umetalakiana ama mmoja katangulia na kuna watoto, kwa mimi binafsi kwa mazingira yalivyo sasa sioi tena, kama ni wanawake wa kutuliza mzuka wapo wengi tu.

Sitaki kuchimbua ndani zaidi, leo naishia hapa
Vipi mwanamke kuwa na watoto wa wanaume tofauti?
 
Uwiiiiiiiiiiiiih utamu wa ngoma ingia uicheze, ila umeeleweka ipasavyo mweeeeeh
 
Itakavyokuwa ndiyo hivyo. Waki ku shit si basi chukulia km huna watoto uza vihepe lima shamba.fuga ving'om be siku ukifa basii umekufa.ila maisha tumbua sana sasa hivi jirushe ili uzeeke kwa haki.
 
Mkuu pole sana hukupata chaguo zuri kwa hao wanawake uliowaoa, mi nakula bata tu kwa hawa nilonao na wamekuwa walimu wazuri kwa watoto wangu.
 
Uko sawa mzee tushashuhidia Moto wake hapa. Kwa jinsi unavyotukabili.
Swala la kuogopa ni kwamba hizi jinsi za k . Zina maajibu yake , Always they already to kill for something . Ushauri tusioe wake wengi kwa dunia ya sasa kama mleta thread anavyosema .
Ukoo mzima unaweza Isha.
 
Hilo suala la watoto mama tofauti liko kwenye familia nyingi sana za kiafrika na madhara yake hayaonekani.

Hilo lakuoa wake wengi sina ujuzi nalo sana, lakini mimi kama mwamamume sidhani kama mwanaume ameumbiwa mwanamke mmoja. N.B mimi si muislamu.

Isaya 4:1 Wakati huo wanawake saba watamvamia mwanamume mmoja na kumwambia, “Chakula na mavazi tutajitafutia wenyewe, lakini wewe utuondolee aibu yetu, uturuhusu tuitwe kwa jina lako.”

Nimenukuu kidogo hapo kama wewe ni mkristo tafakari hilo neno.
Teh teh pole sana mkuu hilo neno ukilitafsiri halina maana hiyo iliyoelezewa hapo

Ndiyo shida ya kuwa mnasoma biblia kama vile mnasoma kitabu cha mabala the farmer
 
Wala usije kudhani ni mimi mkuu, mimi bado kijana kabisa. Hiki ninachokiongea nimekiona kwa watu wanaonizunguka na mtu anakupa sababu za msingi kabisa kwa nini hataki kumsaidia baba yake na badala yake kawekeza kwa mama
Mimi ni shuhuda. Yamenikuta. Lakini mwanaume mwenye kende 2 na uume, halafu ana akili za kichwa na siyo akili za chini, pambana na kuhakikisha watoto wote unawalea pamoja. Hii itasaidia kuwa nao karibu na kuwasimamia katika kila hatua kiasi kwamba watatambuana na kuwa rahisi kuwajengea misingi unayoitaka waishi kwayo.

Kosa kubwa ni kuwaacha walelewe na mama zao na baba wa kambo na kutokuwa na uhakika wanafunzwa nini.

Lakini naungana na mtoa mada, huu mchezo ni mbaya sana. Oa na kuzaa watoto wako na mke mmoja tu.
 
Watu mna akili za kijinga😀😀, mimi nimeleta mada..sasa usitake kulazimisha kunivisha uhusika wakati ni mambo yapo kwenye jamii
Ni kuvaa tu uhusika wala haitatokea kuwa kweli.
 
Don't let your emotional control your thinking...be careful dogo and don't run with girls in the streets because your sting stands up.
 
Teh teh pole sana mkuu hilo neno ukilitafsiri halina maana hiyo iliyoelezewa hapo

Ndiyo shida ya kuwa mnasoma biblia kama vile mnasoma kitabu cha mabala the farmer
Nimetolea mfano tu mkuu, lakini uhalisia huenda ikawa hivyo wanawake ni wengi mtaani na waoaji hakuna.

Ukisema kila mwanamume awe na mwanamke mmoja hao wengine nani awaoe na uwiano hauko sawa?

Kuhusu biblia unaamini vipi kwamba tafsiri yako ndio sahihi? Na si yangu?

Kwa vigezo vipi labda? Hebu nifafanulie kidogo hapo kwa hoja na si kejeli wala dharau mkuu
 
Asiyejua maana haambiwi maana mkuu
 
Huo ni uwoga wa kimbuni,watoto wakikukuta uko vizuri kiuchumi watakuangalia mpka siku unakata roho...ukiwa kapuku wanakuja siku ya mazishi yako na kusepa,tafuta pesa ndio mpango mzima
 
Huo ni uwoga wa kimbuni,watoto wakikukuta uko vizuri kiuchumi watakuangalia mpka siku unakata roho...ukiwa kapuku wanakuja siku ya mazishi yako na kusepa,tafuta pesa ndio mpango mzima

Nenda kwa Felix Mrema ukaone kinachoendelea na pesa zake zote alizokua nazo.
 
Back
Top Bottom