MLEVi Mmoja
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 8,512
- 15,128
Usitutishe !!
😅😅😅Taratibu akili zinaanza kuwarudia.
umeona kwa baba akooWanaume wenzangu, dunia imeshabadilika. Leo ukiwa na watoto wa mama tofauti kwenye familia yako jua unatengeneza kaa la moto baadae na kuwa na wake wawili ndio kabisa kwa asilimia kubwa unakuwa unajitengenezea jehanamu yako mwenyewe. Nimeshuhudia familia nyingi sana zinavurugana mpaka kufikia uhasama wa kufikia kuuana.
Wewe baba ukitaka udharaurike baadae na ukose msaada kwa wanao oa wake wengi halafu ufilisike uzeeni, kwa maisha ya sasa hakuna rangi utaacha kuiona kila mtoto atakuwa busy na mama yake na sio wewe tena na ukiwa na mali watakuheshimu ukiwepo ila ukifa tu amini utakuwa umeacha vita kubwa sana
Kama umeoa, Ikatokea umetalakiana ama mmoja katangulia na kuna watoto, kwa mimi binafsi kwa mazingira yalivyo sasa sioi tena, kama ni wanawake wa kutuliza mzuka wapo wengi tu.
Sitaki kuchimbua ndani zaidi, leo naishia hapa
maisha ya zamani sio kama sasa usikariri..naungana na jamaa ukitaka upate tabu sasa oa wake wawili.1:-Acha uoga..
2:-Lazima uwe na negative perception kwasababu umejifunza kwa waliofeli na hukutaka kujua kwanini walifeli...hvyo badili mtazamo wako,
...What man think about come about..
3:- Adi apo inaonyesha kabsa hujui nn maana ya ndoa,kaa chini dogo ujifunze kwa waliofudhu haya mambo.
La mwisho nakuachia dogo,wanaume kamili huwa tunatumia akili kuishi na wanawake ndomana wafalme na mababu zetu walikuwa wanaishi nao adi vifo vyao...Sasa wanaume sa hv wengi suruali huwa wanatumia hisia kuoa ndo Mana kucha mnalialia.
Don't let your emotional control your thinking...be careful dogo
SAFI SANA MKUUUkitaka kula matunda ya watoto wako jaribu kufanya haya na mengine yanayoendana na haya:-
Usiwabague kwa namna yoyote ile.
Usiwadharau kwa hali yoyote ile
Waheshimu muda wote
Washirikishe inapobidi
Usimdharau mama yao wakishuhudia
Usimpige mama yao wakiona
Usiwasimange kwa mali zako
Usimuache mama yao kwa kosa linalovumilika maana hata hao watoto watakuwa wakubwa na iwapo watajua kuwa ulimuacha mama yao kisa hakuweka mboga chumvi....hapo chuki itakuangukia.
Epuka kumwaga chozi la mkeo/wakezo na kizazi chako maana itafika wakati wataacha kulia na kuanza kuwaza kisasi.
Kamwe usiwatariki narudia tena usiwatariki mama zao kizembe maana watoto wote duniani either ni wakiume au wakike! Huwaonea huruma wazazi wa kike zaidi ya wale wa kiume. Maumbile yao yanaruhusu huruma wale watu. Hivyo iwapo atakuwa nawe pamoja wataleta pesa nawe utakula kwa mgongo wa mama yao, aibu itajificha kwako.
Kama umejaaliwa mali basi tenga sehemu ya mali na uigawe kwa watoto kila mwaka kuwapunguzia ugumu wa maisha, wengi huwaacha watoto wateseke hadi watakapokufa ndio waje kurithi, hii Huzaa chuki kwa watoto na kuona haina haja ya wewe kuishi na kuwa na mali na hufikia muda watoto huanza kuwaza kukuua.
La mwisho ila sio kwa muhimu ni kuwa kamwe usiwagawe watoto kwa vipaji au mali zao au mapenzi binafsi kwani hata mtoto anaweza kumchukia mzazi mazima na maisha yakaenda.
Swali:
Umeshawahi kusikia watoto wamemtelekeza mama?
Wamemuua mama?
Wamempiga mama?
Kama ni ndio, je ni kwa % ngapi ukilinganisha na baba?
Tuwathamini na kuwavumilia wanawake zetu maana hawa ndio akina Hawa waliomhadaa Adam wakishiriana na Shetani.... sisi hatujui Shetani aliongea mambo gani na Hawa pale Heden...... huenda alimwambia kuwa usinitenganishe na wanangu... who knows!.