Kuomba mchango wa harusi ni matusi makubwa

Mbaya zaidi wanaomba michango alafu mwisho wa siku wanakaa kwenye ndoa wiki moja alafu wanaachana
 
Maisha ni kutegemeana.
Kama unataka maisha ya ki peke yako peke yako basi hata hao marafiki usiwaalike.
 
That’s my principle, nimemsomea kwa nguvu my wife to be, yuko anafua huwa tunatofatiana kuhusu haya masherehe.

Imeisha hiyo
 
Tusipowachangisha hela... tutapata wape mitaji yakuanzisha biashara zetu na familia zetu mpyaaa [emoji28][emoji28][emoji28]
Wakati hela yote huliwa wanufaika NI ukumbi mapambo mc nk...wengine hubaki na madeni
 
Sitasahau sista angu aliolewa Mika Kama 8 huo nyuma mzee nkamwambia apande gari la kawaida...fedha zenyewe unategemea mchango ukimwaga hapa kawaida tu inakuwaje hapana...mi nkamwambia sitoomba MTU mchango mwenye shughuli aombe mwenyewe mchango kwa kila MTU anayehisi anatakiwa kumchangia...MTU unakuta NI ndugu yako hampigiani simu Wala kupeana habari akipata shughuli anatokea mamake ambaye NI mamako mkubwa au mdogo anaomba mchango wa shughuli ya Fulani...kwa Nini asije mwenyewe direct umwelwze Kama hawezi kuwalisha watu abebe mkewe akamlishe homu so kubughudhi watu..
 
Yupo jirani yangu ni mama mtu mzima 50yrs sasa! Kipindi anaolewa Mr akamwambia tukabariki ndoa yetu tuendelee na mishe zingne


Mama yule akasema Mimi bila sherehe, tarumbeta, makeup sifungi ndoa, jamaa akamwambia ok....


Wameenda wee, bi mkubwa yule akaona hapa jamaa yupo serious kumbe, akaanza ku apologize tukafunge sijui ndo kubariki jamaa akamjibu sina muda kwa sasa nipo busy na kazi zangu


Na mwanzoni jamaa alimwambia kama ni sherehe huko mbele tukijaaliwa uhai tutafanya anniversary tueke na sherehe Ila sasa siko sawa kiuchumi na ndo tunaanza, twende hivyo hivyo


Bas ikafikia binti yao kapata mume inakuaje hapo, ikabidi maza abembeleze Tena wakafunga usiku wa Christmas 😂, bila makeup wala tarumbeta, wala ukumbi


Nimekuja kujua wanawake wengi ndo wako busy na sherehe mwanaume usipokiwa na misimamo utakula hasara mpaka ukae sawa!
 
Mkuu sasa unataka wenzako waliojiajiri wakale wapi?
Wajenzi wa kumbi za sherehe,ma MC,wapiga picha na macatering
Huo unaitwa ni uchumi shirikishi

Acha ujuaji,unahitaji watu
 
Kuomba michango ya harusi ambayo utaishi na mwenza wako ni uhuni kabisa.Ndoa siyo jambo la ghafla kama msiba/emergency. Jiandaeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…