1. Kwanza sio lazima kusoma cpa ukasome kwenye tuition centres. Sio lazima.
2. Kwa kua sio lazima kufanya mitihani ya cpa uwe mwanafunzi wa centre hoyote, unaweza kusoma popote ama ukajisomea mwenyewe.
3. Usipende kutoa majibu ya jumla jumla' generalization syndrome'. Bro wangu alimaliza bcom UDSM akawa anafundisha wenzake nyumbani huku na yeye anafanya na wote walifaulu. Yeye alikua anayajua hivyo alikua anafanya kwa ajili ya certificate tu ama kua certified.
Ndio maana nikakwambia huhitaji cheti cha CPA kufundisha watu wa cpa, kama unajua utafundisha tu na watafaulu. Kujua jambo sio lazima uwe na certificate yake, unajua tu. Certificate ni formality tu.
The Assassin ,una maanisha ukijisomea, ukafaulu na mitihani ukapata certificate yako,unakuwa ticket kwamba ni certified? Basi ingelikuwa hivyo,kusingekuwepo haja ya kusoma hiyo course. Pamoja na zile gharama, leo hii ipo wazi mtu anaweza akapakua,akajisomea na akafanya mtihani.
Swali langu ni moja tu: vyuo vimefikia hatua tu ya kupokea pesa kisa mtu anajisikia kuwa mhasibu mwenye CPA?
Sipingi mawazo yako,ila napinga ukweli wake. Mtu anaweza kufanya mtihani wa medecin akapewa certificate,akaendelea na kazi?
Nadhani uulizie kwanza CPA ni nini na utofauti wake na certificate nyingine za uhasibu ni nini.
Na ikitokea(japo haipo),ukamuona mtu mwenye CPA analandalanda mtaani, ujue hiyo ni deal.
Hawa watu hutumia gharama kubwa sana kuwa certified,hawa watu wana soko kubwa sana,huwezi kusoma CPA bila uhakika wa ajira au uwezo wa kufanya mambo yako mwenyewe.
Kwanza karibia wote wanaosoma,unakuta tayari wapo kwenye ajira, na husomeshwa.
Mi sikubaliani na wewe, course za CPA usizichukulie kama chuo cha udereva au tuition ya preform one.