Kuona Maiti ikizikwa na Manispaa kumenitafakarisha sana maisha yetu hapa duniani

Maiti sio ya kuionea huruma, wa kumuonea huruma ni Pele ambaye anajua kuwa hana maisha marefu zaidi ya mwezi mmoja.

Huyu anayejua kuwa hawezi kuishi zaidi ya mwezi mmoja, hakuna namna yeyote ya kumfanya aepuke kifo, huyu ndio mtu wa kumuonea huruma sio maiti.

Kipindi kile yule dogo shabiki wa Arsenal ambaye alikuwa na kansa ya kichwa nakumbuka ilikiwa msimu kama huu, dogo aliambiwa kuwa hatoboi mwezi mmoja lazima afe.

Imagine mtoto mdogo anajua mauti yake ipo karibu na bado anatabasamu (hiyo ndio ilinipa huzuni mimi)

Leo hii kila mtu anakuwa na furaha kwasababu hajui lini anakufa, sasa fikiria uumwe halafu madaktari wakuambie una wiki mbili tu zakuishi.

Sasa maiti imejifia wanaenda kuzikwa kwa kushare kaburi bado unaona sio sawa unasikitika?

Watu wanahisia kali sana
 
Kuna nyimbo moja hivi ya muda kidogo inaimbwa " Nasema sina ndugu, wa kuweza kunisaidia, nikifa leo ama kesho Maiti ya kwangu ni bure! Nitazikwa kama Mbwa, na Kunisahau palepale...!!"
 
Mimi ndo huyo jamaa niliekuwa naenda kuzika yale majeneza uliyoyanunua tuliyarudisha kwa wauzaji wakaturudishia hela na wale jamaa tukaenda kuwafukia, acha uoga mkuu kuzikwa ni kulekule kufukiwa tu
 
Mkuu watu wazuri hawafi, wanaokufa ni watu wabaya
 
Kinachoumiza zaidi hamna mtu yoyote atajua taarifa zako kama umekufa au vipi? Maisha yako yanabaki kitendawili juu ya ndugu jamaa na marafiki zako.
 
Kakudanganya nani
Wewe unaweza kukaa na unachoamini na mimi nitabaki na ninachokiamini.

Mavumbi yanarudi mavumbini na nafsi inaenda kwenye hukumu aidha uzima wa milele kwa walio ndani ya Kristo Yesu au kuzimu kwa wasiomuamini Yesu Kristo kama mwokozi wao.

Imeandikwa mwanadamu anakufa mara moja na baada ya kifo ni hukumu.
 
Ukute hapo una ndugu maskini huwapi hata mia.

Ndugu wafu hawajui neno lolote ni mizoga tu kama mizoga mingine.

Hiyo hela uliyonunulia majeneza ungeenda kugawa kwa maskini wakubariki.

Hayo majeneza nakuhakikishia hawakuzikwa nayo zaidi sana yalirudi kwa wahusika wakapewa chenji yao.

Ukiona unajali sana habari za maiti kuliko uhai ujue una shida.
 

"Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada"

Kuna mahali una shida wewe
 
Ila mtu mweusi ni katili sana
 
Mwananyamala hospital hata kama hukupenda kuweka wazi jina la hospital husika... Je nimepatia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…