Kuona Maiti ikizikwa na Manispaa kumenitafakarisha sana maisha yetu hapa duniani

Sawa ila basi kuwe na utu kwenye hayo mazishi ya manispaa sio unazikwa kama upo vitani au ni mkimbizi..
 
Hakuna muda Kama huo mzee wafungwa wengi wanazikwa na manispaa
 
iyo hela ya majeneza ni bora ungeongeza matunda kwaajili ya wagonjwa ambao wangali hai. mtu akifa hajui lolote kwahyo hawajatambua wema wako hamna ata mwenye uwezo wa kukuombea baraka, ila ungefanya kwa walio hai ungeombewa baraka coz wametambua wema na huruma yako kwao
 
Hao mara nyingi sio kama hawakuwa na ndugu ila unakuta wana deni kubwa hapo hospital na hupewi maiti mpaka ulipie sasa watu wanaona mtu ameshafariki halafu tutoe million tano au million 10 mtu anaamua liwalo naliwe.
 
Binadamu ni tofauti na viumbe wote duniani ndio maana Mungu kamtofautisha na wanyama anahitaji kuzikwa ki starabu
 
Kwahio unataka na sisi tuwe kama Ukraine? acheni hizo mambo, let's say ikitokea familia yako wamepata ajari utakubali wazikwe watano shimo moja kisa Ukraine wamefanya hivyo?
 
Hii ndiyo silaha ya wanaofaidika wewe ukiwa muumini wa dini husika. Kukutisha na kifo, maisha baada ya kifo.
Kwa kawaida binadamu ni waoga wa kitu tusichokijua au mahali tusipopajua. Ni vile tunaoopa giza sababu linatufanya tusijua kama tupo mahali salama sababu hauoni vizuri adui au vitu hatari vinavyotuzunguka karibu yetu tukiwa gizani.

Hakuna uhakika wowote sala/dua za kuombea marehemu zitamfaidisha kwa lolote yule mfu. Hii iwe kuna MUNGU au hayupo maana dini zinasema hatima yako ukifa itategemea na matendo yako ukiwa hai. Unaweza kuonekana mtu wa dini sana kwa nje kumbe unatenda dhambi nyingi mbaya kwa siri.

Pili hakuna uhakika sana kwamba kuna maisha baada ya kifo au utasikia maumiu yoyote baada ya kukata roho.
Ushahidi uliopo ni wa simulizi tu toka kwenye vitabu na mapokeo ya simulizi za midomo. Hakuna aliyekufa akarudi, ila walipoteza fahamu na kurudi wanasema hawakusikia maumiu wala chochote kwa muda ambao walipoteza fahamu hadi pale walipo onesha dalili za kurejesha fahamu ndipo walipata hisia na kusikia watu kwa mbali wakiongea. Hii inatupa uhakika ukisha kufa hakuna maumivi wala nini.

Hivyo uzikwe kwenye jeneza, kaburi la peke yako au kaburi la wengi au uchomwe moto, uliwe na viumbe wengine hakuna tofauti katika hisia za mfu(marehemu).
Zile huduma zote za mazishi ni za kutufariji tulio hai tu na kulinda mazingira tusipate magonjwa ya kuambukiza toka kwa miiili iliyokufa.
Kaburi ni kwa faida ya waliobaki hai wanapata mahali pa kumbukumbu ya ndugu yao aliyekufa na usafi wa mazingira kusiwe na harufu na magonjwa kwa walio hai.
 
Maiti sio ya kuionea huruma, wa kumuonea huruma ni Pele ambaye anajua kuwa hana maisha marefu zaidi ya mwezi mmoja.
It's been 17 day since I wrote this shit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…