Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
MAJIRA YA LAANA YAMEKOMA, SASA NI MWANZO WA MAJIRA MAPYA YA BARAKA TELE KWA TAIFA LETU.
Leo nachukua fursa hii kumpongeza mama kwa kuupiga mwingi.
Rais wetu Samia Suluhu Hassan baada ya kusoma kuhusu laana zinazotumaliza kutokana na kukimbiza mwenge, akaamua auondoe na kuweka Tanzanite madini adhimu, adimu na ya thamani kubwa duniani.
Wachawi wa taifa hili walitaka tuendelee kuishi kwenye laana, hebu jiulize, iweje daraja la Tanzanite liwekewe mwenge badala ya Tanzanite?
Mama akaamua kuwatosa baharini wachawi wote, daraja limepata hadhi yake na thamani yake halisi.
Kitendo hiki kwenye ulimwengu wa kiroho ni pigo kubwa sana kwa wachawi ambao nia yao ilikuwa taifa liendelee kulala kwa huzuni kwa kuuabudu mwenge.
Isaya 50:11 SRUVDC
Tazama, ninyi nyote mwashao moto, mjifungiao hiyo mienge; endeni ninyi katika muali wa moto wenu, na katikati ya mienge mliyoiwasha. Mtayapata haya kwa mkono wangu; mtalala kwa huzuni.
Isaya 50:11 BHN
Lakini nyinyi mnaowasha moto, na kujifanyia silaha za mienge, tembeeni kwa mwanga wa moto huo, miali ya moto mliowasha nyinyi wenyewe. Mtakachopata kutoka kwa Mwenyezi-Mungu ni hiki: Nyinyi mtalala chini na mateso makaliIsaiah 50:11
[11]Behold, all you [enemies of your own selves] who attempt to kindle your own fires [and work out your own plans of salvation], who surround and gird yourselves with momentary sparks, darts, and firebrands that you set aflame!–walk by the light of your self-made fire and of the sparks that you have kindled [for yourself, if you will]! But this shall you have from My hand: you shall lie down in grief and in torment. [Isa. 66:24.]