KERO Kuongezeka kwa gharama za maisha chuo cha UDSM (Direct cost)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Vijana wangu mimi nawashauri mlipe tu. Gharama za maisha kwa sasa zimepanda sana huku pesa yetu ikiendelea kupoteza thamani. Kwa ufupi kila mahali hali ni mbaya.

Nashukuru enzi zangu Boom lilikuwa ni 2500 kwa siku. Nakumbuka nilibebwa hapo Mabibo Hostel, kutokana na kukosa accommodation tangu nikiwa First Year. Asubuhi nilipandia sana tu dirishani kwenye zile shuttle za chuo zilizokuja pale nje. Kuna wakati nilikanyaga kwa mguu kutoka mabibo hostel mpaka chuo! Kwa hiyo muache kudeka.
 
πŸ˜…πŸ˜…

Hujawahi kusikia visa vya akina Julius Mtatiro na migomo yaobhapo Udsm

Leo hii ndiyo wakuu wa Wilaya sasa πŸ€—
Nimevisoma humu humu JF πŸ˜€

Sasa hivi kina Mtatiro hawawezi kutokea tena kutokana na watu tunaodeal nao

Ila tunapoelekea maji yakizidi Unga hatuna budi kufanya kama madereva juzi hapo
 
Endeleeni na kulalamika zaman wanafunz wa vyuo walikua ni sehem za fikra sa hiv mmekua ma uvccm mpaka hamna mnachoweza kusema na fikra zenu zimefungwa na wala hamna mawazo chanya,
 
Wanafunzi hawajahusishwa kwenye mchakato wowote limekuja tu ghafla

Kuna makosa makubwa mnayafanya nyie wanafunzi wa vyuo .nguzo pekee na msaada wenu nii serkali zenu za wanafunzi ,sasa mnakuja kupigiwa kampeni na KIONGOZI wa CCM na usomi wenu mnakubari kumchagua mtu kwa sababu KIONGOZI frani kampgia kampeni..
Ni aibu,wanafunzi wa vyuo ni wasomi hawapaswi kulalamika .

Sasa nchi Kila mtu ana lalamika
Heeee.
Mwanasheria analalamika
Mkulima analalamika
Dereva analalamika
Mwanasheria analalamika
Duuuuu
 
Nimevisoma humu humu JF πŸ˜€

Sasa hivi kina Mtatiro hawawezi kutokea tena kutokana na watu tunaodeal nao

Ila tunapoelekea maji yakizidi Unga hatuna budi kufanya kama madereva juzi hapo
Watu wametoka mbali πŸ˜…

Hili suala lenu, ingekuwa enzi za akina Mtatiro, Kunji ingehusika
 
Miaka inabadilika na gharama za maisha zinapanda, hakuna namna lipeni tu.
Hilo la gharama kupanda linafahamika Mkuu tatizo linakuja hiyo direct cost imekuwa kubwa/imeongezeka sio kwa sababu ya gharama kupanda ila kuna baadhi ya categories zimeongezeka ambazo kimsingi hazikuwepo mwanzoni na wala hazina ulazima huo ziwepo kwa sasa

Kwani uwepo wake umefanya Gap liwe kubwa sana mfano hiyo ada ya Sports,ICT services,Graduation na makorokoro mengine....
 
Halafu sisi wakubwa zenu enzi zetu tulikutana pale Nkrumah Hall au Revolution Square na kukubaliana kufanya kunji (mgomo) ili kushinikiza kufanyika kwa jambo fulani. Sasa wewe na wenzako eti mnaandamana mitandaoni!

Kwa nini vijana wa siku hizi ni waoga kiasi hiki?
 
Kumbe UDSM mlikuwa mnakula bata sana. Mimi kwenye chuo cha kata nilikuwa nalipa 169k miaka mingi tu huko nyuma hali kuna wana mlikuwa mnalipa 97k
Hatuna tatizo na hiko kiasi ada tunalipa mara 6 zaidi ya hiyo DC

Tatizo linakuja upandishaji wake ni wa ghafla sana aisee at least wangesema haya mabadiliko yataanza kuwa applied mwakani wala kusingekuwa na maneno na pia hayo makorokoro waliyoyaongeza ni ya wizi wizi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…