KERO Kuongezeka kwa gharama za maisha chuo cha UDSM (Direct cost)

KERO Kuongezeka kwa gharama za maisha chuo cha UDSM (Direct cost)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Kwani imeongezeka kutoka tsh ngapi? Weka basi na direct cost ya ay za nyuma.
 
Kwani imeongezeka kutoka tsh ngapi? Weka basi na direct cost ya ay za nyuma.

Ilikuwa 97400 jumlaa
1380005.jpg
 
Rais wa Daruso wa sasa ni fisiemu
Kuanzia miaka ya 2010's uongozi wa chuo unafanya juu chini kuhakikisha viongozi wa DARUSO ni wa CCM ili kuzuia maandamano

Janja anafikiria jinsi budget ya boom itaishia kulipia hizo direct cost

Ni mwendo wa kula RB na kupiga shuttle pori Mabibo hostel hadi main campus

All in all gharama za maisha zimepanda kilichoongezwa ni gharama za kawaida sana
 
Hali ni mbaya nyie hamjui tu. Imagine kabla ya ongezeko la bei, kuna wanafunzi walikua wanapata ID siku ya mtihani asubuhi, hapo ni baada ya kuchangiwa na wenzao, leo inapanda kwa kiasi hiki...unahisi maisha yatakuwaje?
Kwanini mkubaliane na hayo manyanyaso, siku nyingine onesheni hasira zenu

Uongozi utabadirika tu
 
Ni kweli Mkuu hili jambo limeathiri watu wengi sana na nitafurahi kama likichukuliwa hatua mapema zaidi

Maxence Melo JamiiCheck JamiiForums hebu mtusaidie katika hili mtupazie sauti katika social media akaunti zenu

Hawa watu hawajui hata kula na kipofu aisee yaani mwezi mmoja kabla ya vyuo kufunguliwa unatangaza kupanda kwa direct cost kutoka 97400 mpaka 255400 na mnapandisha mpaka gharama za malazi

Kwenye Direct Cost kuna huduma hapo zimeongezwa kiwiziwizi tu na nashangaa huko kote zimepitishwaje aisee
Wewe bado ni mwanafunzi?
 
Halafu sisi wakubwa zenu enzi zetu tulikutana pale Nkrumah Hall au Revolution Square na kukubaliana kufanya kunji (mgomo) ili kushinikiza kufanyika kwa jambo fulani. Sasa wewe na wenzako eti mnaandamana mitandaoni!

Kwa nini vijana wa siku hizi ni waoga kiasi hiki?
Mbona hata nyie wazee waoga, yanayo endelea hapa nchini, mbona hamu kunji,
Uongo tu 😂😂😂
 
Back
Top Bottom