KERO Kuongezeka kwa gharama za maisha chuo cha UDSM (Direct cost)

KERO Kuongezeka kwa gharama za maisha chuo cha UDSM (Direct cost)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hilo la gharama kupanda linafahamika Mkuu tatizo linakuja hiyo direct cost imekuwa kubwa/imeongezeka sio kwa sababu ya gharama kupanda ila kuna baadhi ya categories zimeongezeka ambazo kimsingi hazikuwepo mwanzoni na wala hazina ulazima huo ziwepo kwa sasa

Kwani uwepo wake umefanya Gap liwe kubwa sana mfano hiyo ada ya Sports,ICT services,Graduation na makorokoro mengine....
Nakuelewa mkuu, taasisi nyingi wanashindwa kutimiza mipango ya mwaka kutokana na mapato kutokutosheleza.
 
Dah. Hii sio powa.
Nawasihi UD, wariview pricing strategy yao. Wa base kwenye direct costs. Hizi indirect costs wawape wanafunzi waiver hadi Boom litakapo panda.
 
Kwa ubora gani wa Kitambulisho cha 15 k Ili kupunguza gharama ..hivi kweli pale UDSM ukitangaza tenda hamna vijana wanaweza kutengeneza ID za bei nafuu. Nini kimependisha gharama za ID ni mafuta au material zake zimepanda?
b3149ff8-b404-4295-a91a-0fbc4819ae74-1_all_21490.jpg
 
Kuna kijana anasoma kwa kutegemea boom tu, hana sapoti ya familia.
BOOM NI LAKI 6.
DIRECT COST 255 K
HOSTEL 150
Bado hajala uyu mtu , hajapata bando, hajapata nauli, hajavaa, hana ela ya field anatunzaga boom kidogo kidogo. WAKUFUNZI WAKIANZA KUPIGWAA ROBA📌
 

Attachments

Ni muhimu kuelewa kwamba kusema ukweli siyo chuki, bali ni sehemu ya kuwasaidia wanafunzi kupata taarifa sahihi kwa wakati. Wakati mwingine ukweli unaweza usipendeze, lakini taarifa inapowasilishwa mapema huwapa wanafunzi nafasi ya planning, kufanya maandalizi na kuwashirikisha wazazi au walezi wao pale inapohitajika.

Kwa sasa, tumewafikishia wanafunzi taarifa kuhusu kuongezeka kwa baadhi ya Direct Costs. Tunatambua kuwa taarifa hii inaweza kuleta hisia tofauti, na baadhi ya wanafunzi wanaweza kuona kwamba viongozi wa DARUSO ndio chanzo cha changamoto hiyo. Hata hivyo, tunasisitiza kuwa DARUSO haijaweka wala kuamua Direct Costs hizo.

Aidha, ni muhimu kufahamu kwamba suala hili lilipitia mchakato wa kitaasisi na lilipitishwa na Senate mwezi Mei. Wakati uamuzi huo unafanyika, sisi tuliopo katika uongozi wa sasa wa DARUSO tulikuwa bado hatujawa viongozi. Hivyo, ni muhimu kutofautisha kati ya decision-making authority na jukumu la viongozi wa wanafunzi la communication and representation.

Wanafunzi wanapaswa kuelewa kwamba sisi pia ni wanafunzi kama wao. Tunatumia huduma za chuo, tunalipa gharama mbalimbali na tunakutana na changamoto zinazofanana na wanazokutana nazo wao.

Hatuna mamlaka ya kubadilisha unilateral decisions zinazofanywa na mamlaka husika za chuo. Jukumu letu kubwa ni kuwa bridge between students, instructors and university management; yaani kuhakikisha taarifa zinafika kwa wanafunzi kwa wakati, changamoto zao zinafikishwa kwenye mamlaka husika, na mawasiliano kati ya pande zote yanaimarishwa.

Kwa hiyo, pale tunapowasilisha taarifa ambayo siyo nzuri kwa wanafunzi, tafadhali tusichukulie kwamba viongozi ndio chanzo cha tatizo. Messenger should not be blamed for the message. Wajibu wetu ni kuhakikisha mwanafunzi anapata taarifa sahihi na kwa wakati, hata kama taarifa hiyo siyo ile ambayo angependa kuisikia.

Tunaamini kuwa transparency, accountability and timely communication ni msingi muhimu katika kujenga DARUSO yenye nguvu na yenye kuaminika.
 
TAARIFA YA KUHAIRISHWA

Mkutano na waandishi wa habari wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi DARUSO uliyopangwa kufanyika tarehe 04/10/2026 siku ya jumapili umeahirishwa hadi taarifa nyingine itakapotolewa.

Tafadhali endelea kufuatilia kurasa rasmi za DARUSO kwa taarifa zaidi.

Asante.
1382197.jpg
 
Back
Top Bottom