nadhani hukuchukua muda kuisoma kwa utulivu hoja yangu. mimi sikulenga kwenye matajiri wakubwa kama kina Anthony Diallo, Shirima, n.k, bali nimelenga kwa wananchi wa kawaida wa maeneo mbalimbali hapa nchini. na katika hoja yangu nimesema eneo ambalo halina zao la biashara lenye bei nzuri mara nyingi huwa halifaidiki kutokana na uwekezaji wa serikali ktk eneo hilo.
somo la hali ya kiuchumi ya maeneo mbalimbali hapa Tanzania nililipata wakati nasoma shule. nimebahatika kusoma ktk shule kongwe za serikali na nilikutana na wanafunzi toka maeneo mbalimbali. katika shule kongwe kulikuwa na utaratibu wa kuchukua wanafunzi toka mkoa mmoja kwa wingi kila mwaka. kulikuwa kuna mwaka wanakuja wanafunzi wengi toka mkoa kama Singida, mwaka mwingine watatoka Kilimanjaro, unaofuata Kigoma, n.k n.k.
sasa katika observation yangu niliweza kujua mkoa gani una changamoto za kiuchumi na umasikini kuliko mkoa mwingine kwa kuangalia hali za kiuchumi na mahitaji za wanafunzi waliokuwa wanaletwa kila mwaka shuleni kwetu. nakuhakikishia ukichukua random sample ya mtoto wa Kyela, Tandahimba, Manyoni, Maswa, Vunjo, n.k utaweza kujua eneo gani lina changamoto ya kiuchumi kuliko lingine. Na ukichunguza zaidi utajua kwamba changamoto hizo za kiuchumi zinatokana na uwepo au kutokuwepo kwa ZAO LA BIASHARA lenye bei nzuri, linalolipa, ktk eneo husika.
cc
MzalendoHalisi,
luambo makiadi