Kuongezwa muda wa Urais: Askofu Emmaus Bandekile awaonya Rais Magufuli na Spika Ndugai

Moja ya bandiko bora sana kuwekwa hapa, hasa kipindi hiki, heko na hongera Baba Askofu kwa hekima na ujasiri wako, umeutendea haki wadhifa wako, Mungu akubariki sana
 
Yeye anaongea kama yeye! Kama hutaki awafunge watu midomooo, Kwanini Wewe unajaribu kumfunga yeye mdomo?! Kwa taarifa yako, ni jukumu la viongozi wa dini (hasa Kibiblia) kuonya, kukemea, kutia moyo na hata kufundisha viongozi wa kisiasa!
Aonye mambo ya dini sio siasa, Kama anataka aache dini aingie ktk siasa
 
lakini lengo kuu lililojificha likiwa ni kulinda matakwa yao binafsi kwa njia ya kuwazuia au kuwanyamazisha watu wengine wanaoonekana kuwa ni tishio kwa nafasi zao na matakwa yao! Ahsante hapo
 
Yaani kwa hoja kama hizi za kuchezea katiba,napata wakati mgumu sana wa kuishi humu nchini in heri Mungu aje atoe hukumu
 
Ndani ya ccm na hata nje ya CCM kwa kizazi hiki sioni wa kumfikia magufuli hata robo utendaji wake.
Kwa haraka haraka toka baba wa Taifa nyerere aondoke madarakani 1984 nchi yetu haikuwahi kupata mzalendo kama magufuli wengi walijali maslahi yao ila Magufuli kajilipua kuvaa viatu vya nyerere

Tukimpoteza magufuli itatuchikua miaka 30 tena kumpata magufuli mpya

Ndio maana tunakuomba Magufuli ukae madarakani mpaka 2034 Ili uinyoshe nchi

Nchi ilishaoza hii ilishakua shamba la bibi

Magufuli tunakuomba kaa madarakani walau hata 2034 utupeleke tuwe kama Thailand

Hizi kelele za wachache mtandaoni ni za vijana wanaotumiwa na mafisadi kukuchafua zikuumize kichwa mzee wetu

Mungu akupe nguvu katika uongozi wako
 

Kama unampenda sana kamfanye awe rais wa ukoo wako.

Yeye atawale muda wake ukiisha aondoke.

Miaka minne aliyokaa madarakani, amekuza deni la Taifa kuliko Miaka yote 10 aliyotawala Kikwete, Je akikaa miaka 20 si ataweka bondi nchi nzima ili aendelee kukopa na kujenga miwhite elephant projects yake?

Muda wake ukifika atoke tu, asipotoka tutamsaidia kutoka kwa njia tunazozijua
 
Unalevel ipi ya Elimu?

Umeandika ujinga mtupu,kiufupi Wewe ni Malaya wa kisiasa
 
Askofu anamuonya Rais? Kwani lini Rais alisema anataka kuongeza muda wa kutawala? Ni vyema angewaonya wananchi. Sasa kila mtu siku hizi anaonya na sisi wananchi tukionya kuwa tunamtaka JPM aendelee vipi hapo.
 
Natamani sana kuona vichwa kama Kafulila, David Silinde kwenye serikali ijayo ya JPM hakika itakuwa ni mchaka mchaka naiona Tanzania yenye mafanikio makubwa siku za usoni.
 
Nasubiri nasaha nyingine toka kwa Askofu Niwemuganyizi" Wawili hawa hunipa faraja na kuona bado kuna jasiri wa kuita kijiko kwa jina lake! Mungu awabariki na wote wapenda haki,ukweli.
 
Uliwahik kugongewa mlango wako ukaombwa deni la Taifa?
 
Wenye busara humwomba Mungu na si binadamu.
 
Wajinga wa mihimili hii miwili wataiingiza nchi katika matatizo. Elites person najua watakataa huu upuuzi wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…