Kuongezwa muda wa Urais: Askofu Emmaus Bandekile awaonya Rais Magufuli na Spika Ndugai

Kuongezwa muda wa Urais: Askofu Emmaus Bandekile awaonya Rais Magufuli na Spika Ndugai

Nimemsikia Mbunge mmoja akiongea Bungeni akitaka Bunge libadilishe Katiba ya Nchi ili kumfanya Rais Magufuli aendelee kutawala hata baada ya kumaliza kipindi chake cha kikatiba cha miaka 10. Kama hilo halitoshi, Spika Ndugai amesikika akimhakikishia Mbunge husika kuwa kazi hiyo ya kubadilisha kipengere cha Katiba kinachoweka ukomo wa Rais kuwa miaka 10 itafanywa na wao wote [Wabunge] katika Bunge lijalo. [Spika anaonekana kuwa na uhakika kuwa Rais Magufuli na wao wenyewe watachaguliwa tena katika Uchaguzi wa Mwaka huu].

Ninapenda niwalejeze Spika Ndugai, Wabunge, na Watanzania wote kwa ujumla kuhusu habari ya Mfalme Darius na Bunge lake katika Dola ya Uajemi (Persia) na Umedi (Mede) yapata miaka 2500 iliyopita.

Mfalme Darius aliunda Baraza (Bunge) lake lenye Wajumbe 120 aliowateua yeye wenyewe. Katika hali ya kutaka kumkomoa Danieli ambaye alionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kiuongozi kuwazidi wao, Wabunge wenye nia ovu walianzisha mikakati ya siri ya kutaka kumnyamazisha Danieli.

Mikakati yote iliposhindwa, waliamua kutunga sheria ambayo walijua kuwa itamfurahisha Mfalme Darius lakini huku ikiwa na lengo lililojificha la kumnyamazisha kabisa Danieli kwani walijua kuwa hatima ya sheria ile ilikuwa ni kifo cha Danieli. Walitunga sheria ya kutukuza mawazo ya Mfalme kwa kusifu na kuabudu mradi au sanamu aliyoitengeneza Mfalme.

Walimshawishi Mfalme aitie muhuri au aisaini sheria ile. Wakapitisha Azimio la Ki-Bunge la kuzuia mtu ye yote au mamlaka ye yote kutangua sheria ile. Hata hivyo, Mungu hakuruhusu uovu ule na akaingilia kati. Wabunge wote waliopitisha Azimio lile waliuawa pamoja na wake zao na watoto wao lakini Danieli alipona na aliendelea kustawi zaidi. Kwa uelewa zaidi kuhusu habari hii someni Biblia Takatifu katika Kitabu cha Danieli 6:1-28.

Tunapenda kuwaonya na kuwatahadharisha Wabunge na watu wote wanaofanya mikakati ya kutaka kutunga Sheria mbalimbali zenye hila mtambuka ikiwemo kutaka kumfurahisha Rais aliyeko madarakani lakini lengo kuu lililojificha likiwa ni kulinda matakwa yao binafsi kwa njia ya kuwazuia au kuwanyamazisha watu wengine wanaoonekana kuwa ni tishio kwa nafasi zao na matakwa yao! Mungu anatoa onyo kali kwa watu na viongozi wa namna hiyo (Isaya 10:1-4).

Ushauri wangu kwa Rais Magufuli ni kuwa awe makini sana na watu ambao kila kukicha wanapenda kumsifia tu pasipo hata kumtahadharisha. Akiwafuata watu wa namna hiyo, basi ajue kuwa anaikaribisha hasira ya Mungu kwake mwenyewe na kizazi chake!

Ninamshukuru Mungu mwenye rehema nyingi kwa kunipa ujasiri wa kuyaandika haya (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
FB_IMG_1591817601385.jpg
 
Mwalimu Nyerere alipoweka Ukomo wa Uongozi aliona mbali sana tena ameweka akiwa bado Ikulu anakula keki ya Taifa letu la Tanzania, tusibeze Vitu tusivyo vifahamu na akaenda mbali na kusema " Mtu akikaa sana Madarakani mwishoe hulewa madaraka "
 
Rais Magufuli anafanya kazi kubwa wazo la kumuongezea muda ni wazo zuri sana
Kuwabambikia kesi kuwanunua wapinzani kujenga chato Airport kienyeji pasipo idhini ya bunge ni kazi nzuri?
 
Magufuli aliposema omba kwa ajili ya janga la corona ulimkejeli.
Sasa hivi unajifanya kumjua sana Mungu na kunukuu maandio!

Mpka oktoba lazima nguo za ndani mvae kichwani.
Corona bado ipo na maambukizi yapo watu wanaugulia majumbani wanafia majumbani
 
Kwani chadema Ina watu million ngapi na mbona mmeshindwa kumpata mtu Kama Mbowe
Ilianza kama story ila sasa tunapoelekea naona hili swala lishapita na lazima litokee hivi mimi naomba nikuulize ndugai na CCM yako hivi mmefikiria umbali kiasi gani? au nyie mnawaza maisha yenu tu ya watoto wenu na wajukuu wenu hamuyawazii?

Haiingii akilini kabisa mtu anaongea kwamba hatuwezi pata mtu kama JPM tena! hivi mko serious kweli nyie? kweli hii nchi yenye watu milioni 60+ asipatikane mtu kama kama yeye?

Kama mnaajenda zenu binafsi mseme lakini hoja hizo hazina mashiko, hivi mkiweka ukomo wa Rais maybe ikawa ni mihula minne hivi mnajua huko mbeleni mtakuja kuongozwa na Rais gani? mfano Rais aongoze kwa mihula minne hivi ikitokea akaja akapatikana Rais mbovu hii nchi itawekwa kwenye hali gani?

mimi ninaamini hata JPM mwenyewe hawezi kukubali lazima ataiheshimu katiba!

Hii nchi imeongozwa hata kabla yake na itaendelea hata baada yake, sisi wananchi hatukuwatuma hivyo, hayo ni maoni yenu binafsi sio ya wananchi mnaowawakilisha!

Hivi Spika Ndugai wanakongwa ndio wamekutuma hivyo? mpo bungeni kuwakilisha mawazo ya wananchi wenu waliyowaagiza sio kuwakilisha mawazo yenu msijisahau


Kweli JPM anafanya kazi nzuri sana lakini kwa swala la kuongezewa muda hapana kwakweli
 
Hiyo kazi kubwa mnayoimba kila siku humu ni kazi gani amefanya? Mbona sisi wananchi wakaida hatuoni maendeleo yoyote,Acheni ujinga hakuna kitu cha ajabu Magufuli amewafanyia watanzania zaidi kuongeza chuki.
Kuteka
Kutesa
Kuua
Kukandamiza
Kufunga watu midomo
Kunyima
 
Io haki mbona mmewanyima Wana chadema
kaakaa mkubwa ujue kila mtu ana haki ya kutafuta madaraka ujue uyo inafaaa ang'olewe aingie mwingine wenda anae ingia atafanya mazur zaid....so ukisema aongezeee unawanyima chance wengine !
 
ILA chadema hamna vijana wenye uwezo wa kuongoza chama
Wapo wa Tz wengine wengi ndani na nje ya CCM, wenye uwezo zaidi ya Magu, wanaweza kuongoza na kufanywa makubwa zaidi yake tena bila kuteka, kuuwa, wala kuleta farka kwenye jamii.
 
Vip Alie badili katiba ya chadema
Awamu ya I iliona mbali chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere. Hadi sasa Nyerere ndiye ana rekodi ya kuhudumu nafasi ya urais kwa muda mrefu.
Katika mazingira ya changamoto za wakati ule binafsi naona alitumikia taifa kwa nia njema kwa kipindi hicho. Mazingira duniani kote yamebadilika.

Leo tuna CCM-MASLAHI. Kikundi kidogo cha wasomi wachache cha CCM-MASLAHI kimeteka kwa maslahi. Dhambi kubwa inayokwenda kutendeka ni kubadili katiba nzuei aliyoiacha Nyerere kww manufaa ya taifa hili.
 
kila mtu ana utashi wake katika kuongoza, Inawezekana JPM amekuwa kiongozi bora wa awamu yake lakini nani ajuaye kuwa ataendelea kua kiongozi bora katika wakati ujao.
 
Back
Top Bottom