Kuota mambo ya shule ni nini tafsiri yake?

Huwa naota hii ndoto na haijapita hata wiki na cha ajabu niliota nipo advance na ndoto ilikuwa na uhalisia hadi nikaamka bado nina wenge la kujiuliza kama nishapita chuo kweli au nisubiri kujaza application forms 😁😁


Shukrani kwa ufafanuzi

Nitakucheki pia unipe tafsiri zaidi 🙏🙏
 
Ukiota unafanya mtihani manake kuna jambo gumu linataka kuja kwako either kwenye finance zako,mahusiano or elsewhere!
Unatakiwa umuombe Mungu akuepushe au kama linapaswa kuja basi muombe Mungu akusaidie kuvuka!
 
Kawaida tu ni sehemu ambayo umespend muda mwingi "ukiwa active" kuliko hata nyumbani, memories nyingi ni za huko hivyo si ajabu ubongo kukupa flashbacks 👏
 
Mie pia nimeota ndoto hiyo asubuhi ya leo na huwa naota mara kwa mara...... ila nilisikia kuwa ndoto za hivo zina maana ya kuwa kuna vita kubwa sana ili kusonga mbele kimaisha, yaani unarudishwa nyuma.
 
Kama uko level ya juu alafu unaota uko primary au high school,spiritualy ina maanisha umedumaa kimaendeleo,yani hapo ulipo uko level ya chini ambayo ndo hiyo primary ila wewe unajiona umemaliza bachelor au masters kumbe pengine ulipaswa uwe na phd au kama ni biashara unafanya ulipaswa kuwa mbali zaidi ya hapo ulipo!
Unapaswa ukomae na maombi ili uwe level ile unayopaswa kuwa!
 
Kweli kabisa mkuu huwa inatokea Sana, sema Nini hii ni hali ya kisaklojia tu Kwa sababu Shule ni moment ambayo ni ngumu na inachukua process kubwa ya maisha ya binadamu. Ndio maana hii hali hutokea Sana Kwa watu wengi
 
Uko sahihi kabisa...
 
Mkuu pole kwanza..pili tafuta mahubiri ya mwakasege kuhusu ndoto youtube..sijui wewe ni dini gani lakini ushauri wangu ni huo.kila la ķheri mkuu.
 

Hili naona kama linanihusu pia brother, juzi kati kuna mipango niliiseti fresh ila mambo yalipotokea sijui, yaani nimepoteana kabsaaa

Na ni kama vitu vitatu so sielewi 🤦🏽‍♂️🤦🏽‍♂️
 
Ndoto za shule binafsi huwa naziota sana, lakini kila ndoto nikiota huwa nipo kwenye chumba cha mtihani najiandaa kufanya mtihani.
Katika mitihani yote ya ndotoni sijawahi kufanya nikamaliza hata mmoja. Sababu ni maswali kunishinda yote yaani nakuwa sijui hata moja, nikiamka kwenye akili ya kawaida maswali nayajua kabisa na majibu yake.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Yaani zinakuwaga za kiwaki
 
Njoo pm nikweleshe vizuri ila faida ya wote hiyo ni roho ya kuludi nyuma kwenye maisha yako iyo ishara mbaya sana nenda kwenye madhabu zivunje kwa maombi ndoo maana unaota ya kale
 
Nimekusoma mkuu❤️
 
mkuu mi mara ingne naota,,, mtihan u.ekaribia kabisa kuufanya ila nakuwa sijasoma hata kidogo na sijuw ntajibu nn kwene mtihani huo!!, hii imekaaje?..
 
ukiota unataka kufanya mtihan lakin hujasoma unashangaa tu papér limekaribia inakuwaje!!jr tuokoe hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…