ROBERT HERIEL hicho kicheko maana ake nini??? Au ni ndoto za watu tulioshiba wali maharage???
Huyo kanifurahisha mno.
Ndoto mara nyingi Inategemea na mambo haya;
1. Mazingira ya uliyokuwa ndotoni,
Je ni nyumbani, njiani, mjini au shambani, porini au baharini n.k
2. Muda
Je ukiwa ndotoni ilikuwa mchana au usiku, au asubuh au jioni.
Au kulikuwa na mbalamwezi alafu chini mawingu yanapita.
3. Wahusika.
Je unawajua wahusika wa ndotoni?
Vipi mahusiano yako na wao, je mara ya mwisho kuonana nao ilikuwa lini?
Mlikuwa mnafanyaje?
Je walikuwa wanakupinga au walikuwa wapo pamoja na wewe?
Au je Baadhi ya wahusika wa ndotoni hujawahi kuwaona?
Je walikuwa wanakuambia au kufanya nini?
4. Hali yako.
Je ulikuwa katika Hali gani wakati ndoto inaendelea, je ulikuwa nafuraha, au je ulikuwa na huzuni, au je ulikuwa katika bumbuazi ukishangaa, au je ulikuwa unaogopa?
Mara nyingi maana ya ndoto kuwa nzuri au mbaya hata kabla hujajua maana ya ndoto hiyo IPO hapa.
5. Tukio lililokuwa kinaendelea(main Action)
Je tukio gani la msingi lililobeba ndoto hiyo.
Je ulikuwa unakimbizwa, na kina Nani? Kwa sababu ipi? Je ulipokuwa unapakimbillia unapajua.
Je ulivuka barabara(yalami au yavumbi) au ulivuka MTO(MTO ulikuwa na maji au umekauka)
Kama uliokota pesa, ilikuwa ni wapi? Je mazingira hayo yanaruhusu kuokota kiasi hicho cha pesa ulichookota, uliwaza kuzifanyia nini? Vipi aliyezidondosha je ukiweza kumfikirià
6. Kukatika Kwa ndoto.
Mara nyingi hapa ndipo Code ya Msingi ya ndoto ilipo. Nini kilikufanya ushtuke usingizini wakati unaota?
Je ni hofu iliyopitiliza, je ni furaha iliyopitiliza, je ni aibu iliyokuwa imekupata, au je ulikuwa unakaribia kukamatwa? Au je ulikuwa umeshinda.
Hayo ni Kwa uchache