Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Nimeweka mawazo mbadala kwa mujibu wa maoni yangu, yakifuata falsafa ya kushika hamsini zangu, watu maarufu sijipi umuhimu katika maisha yao, kwanza siwajui kihivyo. Mimi nina familia yangu ambayo inahitaji muongozo wangu na sifikiri kujikita kwenye maisha ya watu ambao hawanijui, siwajui, hawajaniomba ushauri, sielewi maisha yao yana utata gani, sifikiri kujikita kwenye maisha yao ni kitu muhimu na chenye tija.Ukishakuwa maarufu kuna gharama zake za kulipa mojawapo ndo hiki unachopinga. Hata wewe Kiranga ukiwa maarufu tutakujadili tu maana hakuna namna. Kuna watu wengi wana matatizo kama ya Lemutuz ila hatujadili kwasababu hatuwajui.
Nafikiri kufuatia sana maisha ya celebrities ni emptiness fulani katika maisha ya mtu.
Ila, kila mtu ana uhuru wa kujiamulia mwenyewe, ndiyo maana watu wengine wanapenda kuwaangalia kina Kardashians, na mimi sijawahi kuangalia hata episode moja.