Kilichofelisha maandamano ya D9
1.kufungiwa account za viongozi wa kuhamasisha maandamano tena dk za mwishoooni(ktk sehemu ambayo dola ilicheza ni hapa) morali ilishuka sanaaa!!!
2. Kukosekana backup ya jioni jioni ya mtu mwenye ushawishi( kumbuka maandamano ya Oct29 yalikuwa na backup ya Tesha na Gwajiboy akapigilia msumali wa mwisho- Ngoma ikalipuka. ( Dola ilicheza sana kufungulia makanisa yake fasta baada ya Ile 0ct29 wangefanya mchezo D9 ingekuwa mbaya sana kama Gwajiboy angeludi tena.
3. Wabongo wengi ni waoga kuwa chambo lkn vulugu wanaziweza sana tu, amini nakwambia kama D9 wangepatikana chambo basi Ngoma inge-bast.(Dola inawatu wenye akili sana sema ukiona wanazingua basi jua wanajizimaga Data tu. Walijua kbs gwajima anao chambo ambao wapo tayari kwa lolote ili mradi wasikue baba yao kasema nendeni-(kumbukeni chimbuko la maandamano ya Oct29)
4.jeshi kuingia mitaani kufanya Doria-Oct29 Wananchi waliamini jeshi liko upande wao lkn kuelekea D9 Hali ikawa tofauti na jeshi likaonekana liko upande wa watawala, hii pia iliwavunja moyo sana, kile ki- moral Cha kusema tunaenda kuandamana tukiwa na ulinzi nyuma yetu kikayeyuka. Watanzania bado wanaliheshimu sana jeshi lao la wananchi kitendo Cha JW kuingia mitaani waliona kama jeshi limetoa katazo la maandamano hivyo kwenda road ni kama kupingana na jeshi lao. (Alieishauri serikali itumie jeshi kuzuia maandamano mpeni ka cheo huko aliko kwa kuwasaidia kubaki madarakani tofauti na hapo sijui tungekuwa tunazubngumza Nini sasa hivi.
5 kukosekana watu wenye mikakati na wabunifu upande wa wanamaandamano(mtaani tunaita udambwi udambwi ulikosekana) D9 wakaludia mbinu zile zile za Oct29 sasa serikali sio wajinga kiasi hicho wazee.
Nilichokuja kugundua ukimtoa Mange wanaharakati wengi ni weupe kichwani, hawako smart kbs, full mihemuko, mikulupuko, kurukia rukia vitu bila kuvipima na kupata uhakika wavyo,( wakashau kwamba kipindi kama hicho jamii Iko ktk Hali ya kuwapima Imani, kwa hiyo ilibidi Kila taarifa wanayoitoa kwa uma iwe ya uhakika na sio kurukaruka na vijitaarifa vya kuokoteza. Sasa madhara yake raia wakawaona kama wazushi tu.
Mwenzao mange haokotezi taarifa, akipiga anapiga kweli, ban ya mange ikawa imeyumisha movement yotee( maana ndio mwenye taarifa za kuaminika/ mbeba maono
6. Lockdown- hii siisemei sana nadhani Kila mtu anajua Lockdown ilivyogeuka nyota wa mchezo kwa serikali😅
Waandaa maandamano ilibidi wawe mbele ya muda kwa kuisoma akili ya serikali ilivyopeperusha sherehe ya uhuru na kujua kingefuata Nini baada ya serikali kuvunja sherehe hizo. Kiufupi viashiria vilikuwa vingi mapema sana ambavyo vilionesha siku ya D9 watu tungefungiwa ndani lkn watu hao hawakuwa na mbinu mbadala.(Tatizo walilonalo mpaka Leo)
7. Ukimya wa Chadema kwenye kusaport maandamano direct, hilo lilinishangaza na ninaendela kushangaa😅 lkn viongozi wa Chadema nao ni watu kama sisi, wanatamani kulala sehemu nzuri na wapate usingizi nzuri na wake zao! Mbeeh! Kila siku kulala kwenye sakafu iliyomwagiwa maji sio mchezo wazee😅 ( hapa maji yaliwamwagika tumboni.)
8. Ukimya wa serikali- hapa pia walicheza walidhibiti Ile payuka payupa ya watu wao hiyo adui hakujua serikali ilikuwa ikipanga Nini kiundani.
9. Serikali kuwaibua wale jamaa wa jihad- hii iliwasaidia sana lkn mbinu hii ingeweza kuleta madhara makubwa sana kama na wale wa upande wa pili wasingekubali kujishusha kidogo, watu wale wangesema sasa hawa twende nao bampa to bampa hakika ingekuwa mbaya sana. Sasa kitendo Cha watu wale kufikiria kujishusha na kutumia busara iliwapa serikali kupumua kidogo( lkn siku nyingine wasiludie mbinu hii)
Anyway Leo ngoja niishie hapo maana nimejitahidi kuandika sana, Mimi sio mpenzi wa kuandika so kama kutakuwa tipping error mnisamehe.
Pia maoni yangu kuhusu maandamano yajayo ya D25 ukweli mchungu ni kwa mpaka sasa serikali ime leval uwanja 2-2
Wanaharakati wasipokuwa makini wanaendwa kupigwa comeback mbaya ya 2-3 ama 2-5. Waache kukurupuka hakuna kipindi ambacho dola ipo makini kwenye upande huo kama sasa.
Lkn watu wa maandamano wakiongeza akili na mikakati mujarabu sio ajabu watu wakapigwa ka kuwanyong'onyeza kabisaaaa ( japo mmmmhhh sioni)
—Hii ni bila mihemuko ndo utaielewa.
Mods nawaomba sana hii comment muipandishe iwe Uzi kamili kama mtaweza Kuna chakujifunza hapa kwa Kila upande.🙏🙏