Kupangiwa muda wa kula ni utumwa

Kupangiwa muda wa kula ni utumwa

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Utumwa ni hali ya kutumikishwa na kunyang'anywa hiari yako.

Utumwa mbaya ni ule wa kifikra, ambapo mtu mmoja au kundi la watu linawaburuza kiasi watacho.

Kupangiwa muda wa kula iwe kazini kwako au popote pale huo ni utumwa.

Jikwamue na utafute uhuru wako wa mwili na fikra.
 
Utumwa ni hali ya kutumikishwa na kunyang'anywa hiari yako.
Wazo lako lina mashiko isipokua ungelijengea hoja zinazo eleweka kuhusu hususan unapo sema/taka neno  utumwa
Utumwa mbaya ni ule wa kifikra, ambapo mtu mmoja au kundi la watu linawaburuza kiasi watacho.
Kwa namna binadamu walivyo umbika, sio kila mmoja anaweza kufikiri kwa mfanano na mwingine. Na hii imepelekea binadam kugawanyika katika makundi tofauti ili kuweza kupata uwiano na mgawanyo mzuri katika namna ya kuishi ama kujioatia kipato.
Hapa namaanisha sio kila mtu anaweza akawa mfanya biashara ama akajiajiri.
Najaribu kumaanisha kwamba kila mtu akiwa mkulima nani atanunua chakula cha mwingine?
Ama kila mtu akiwa anajitegemea je nani atamtegemea mwingine??
Kupangiwa muda wa kula iwe kazini kwako au popote pale huo ni utumwa.
Mkuu, ustaarabu ni jambo la kawaida katika maisha ya binadam, hivyo basi hata unapo kuta wengine wameweka muda wa kula ama nyumbani kwako ukipanga muda wa kula ni jambo la kistaarabu ama utaratibu wa kawaida katika maisha tunayo ishi pamoja na jamii ama maeneo tofauti tofauti
Jikwamue na utafute uhuru wako wa mwili na fikra.
Hapa mwisho nakushauri tu upunguze kuweka umuhimu kwenye maisha ya watu wengine.
 
Utumwa ni hali ya kutumikishwa na kunyang'anywa hiari yako.

Utumwa mbaya ni ule wa kifikra, ambapo mtu mmoja au kundi la watu linawaburuza kiasi watacho.

Kupangiwa muda wa kula iwe kazini kwako au popote pale huo ni utumwa.

Jikwamue na utafute uhuru wako wa mwili na fikra.
Tajiri unapangiwa Muda wa Kula? Au Hili jina ni la urithi wewe ni Apeche Alolo?
 
Back
Top Bottom