Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.

Hivi vitu lazima uviondowe mwenyewe, serikali haihusiani kabisa!
Hivi unajua Mafia wanapelekewa meli, wanaiaribu ili wabaki na ngalawa zao?
Hivi kumbe Kisiwa cha Mafia wamelekewa Meli wakaiaribu ....? ......Huo ndio ujinga....adui namba moja......
Meli kama ile Mv Kigamboni?
 
Wewe ni kilaza wa kufa mtu mkuu,mimi nimesoma bandiko lako nikitegemea kuona kama kuna sehemu utaandika sababu za CCM kutawala milele ni zipi ila wala sijaona!!
 
Inaonekana ww na mtoto wako mnakaa mnadiskasi kidemokrasia akikosea au akikukosea,
Watoto wangu sijawahi kuwaadhibu hata siku moja,Nimewapa uhuru wa kajadiliana na mimi kila kitu,kama mzee,...,Watoto wangu wamefankiwa sana kimaisha

Mtoto kama mtoto ana safari refu ya kusoma taangu anazaliwa mpaka anakuwa mkubwa wa kutengeneza familia yake mwenye sasa kama una tabia ya kumpiga na kuanza kumuadhibu mtoto atasoma nini kutoka kwako kama mzee...

Mkuu,haya ninayo kufahamisha ni tabu sana kwa wewe kufahamu,lakini kama hii habari ataisoma Muhindi,Mwarabu,Mzungu watafahamu nini ninachoongea
 
Ccm wanajua wa tz ni wapole ndio maana wanawachezea watakavyo waliosema amani haiji ila kwa ncha ya upanga hawakukosea tungechapana hata kwa wiki moja tungeheshimiana sana wanachofanya ccm ni sawa na kumtia mwanaume mwenzako kidole halafu badala ya kuchukia anachekacheka ulaya waliheshimiana baada ya vita so was Kenyans cc bado tuko usingizi wa pono ccm wasiombee wa tz waamke watatafuta mlango wa kutokea hawatauona
 
KUSEMA CCM ITAKAA MILELE NI KAMA KUMTUKANA MUNGU, kwa sababu Mungu peke yake NDIYE aliyekuwepo tangia kitambo na atakuwepo milele.
 

Miaka 50 kwa NCHI ni midogo sana. Hata kizazi kimoja hakijapita tangu Uhuru!! Angalia China na India ndo utajua uwiano wa miaka kwa maendeleo ya NCHI.
 
Miaka 50 kwa NCHI ni midogo sana. Hata kizazi kimoja hakijapita tangu Uhuru!! Angalia China na India ndo utajua uwiano wa miaka kwa maendeleo ya NCHI.
Mkuu angalia Korea ya kusini na Africa zilikuwa wapi 50 yrs ago na sasa tuko wapi. Miaka 50 ni mingi kama unabaki pale pale na wengine wanachapa mwendo.
 
Swala la CCM kutawala milele sikubaliani nalo. Ila ni kweli itaendelea kutawala kwa kipindi kirefu kijacho na hasa ukizingatia mikakati inayojengwa ikihinikizwa na China, kuhakikisha vyama vyote vilivyoshiriki kupigania ukombozi Afrika havipotei. Ni ukweli kuwa China ilihamanika sana kupotea kwa UNIP ya Zambia na KANU ya Kenya ikiamini ni mkakati wa nchi za magharibi kuviondoa madarakani vyama vilivyopigania uhuru barani Afrika. Ndio maana imekuja na mkakati huu wa kuvinusuru kwa kuvijengea uwezo wa kimkakati kuhakikisha havipotei. China imeamua kutumia resorcess zake kuvinusuru vyama hivi na inaelekea kufanikiwa kama si hivyo mapinduzi ya Mugabe na Zuma, ZANU PF na ANC vilikuwa inaelekea kupotea.
 
"CCM ita tawala milele, endapo hakuna kitakacho badirika, hii ni kutokana na uendeshaji wa siasa za sasa, Tuukubari kweli, magufuli kasema ukweli"

Mwaka 2015 CCM walipata kura milioni 5.5 upinzami walipata kura mikioni 4.2,
Wananchi milioni 4.2 ni wapinzani wa serikali ya CCM, hao akina mbowe, zito, Lisu, Mdee na wengineo wengi hao ni wawakilishi tu, unapozungumzia upinzani zungumzia hilo kundi hapo juu.

Haya mambo hayajaanza awamu hii, yalikuwepo tokea zamani, Ajenda ya ufisadi iliwapa nguvu wapinzani,

Ilizimika mwaka 2015 baada ya ujio wa JPM,

Ajenda inayofuata ndiyo itakayo ondoa ukweli huo ulio ueleza, hii huenda ikawa ni ajenda hatari kuliko ile ya ufisadi.

Hivyo basi, CCM haitatawala milele.
 
La CCM kutawala milele ni la kweli kwani ni agizo la rais na polisi na jeshi wanatakiwa walisimamie kama ilivyo kwa maagizo mengine.
 
La CCM kutawala milele ni la kweli kwani ni agizo la rais na polisi na jeshi wanatakiwa walisimamie kama ilivyo kwa maagizo mengine.

mbeleko za mazuzu ya CCM hizi hapa zikipokea maagizo
 

Attachments

  • CCM.jpeg
    54 KB · Views: 29
Mkuu angalia Korea ya kusini na Africa zilikuwa wapi 50 yrs ago na sasa tuko wapi. Miaka 50 ni mingi kama unabaki pale pale na wengine wanachapa mwendo.

Mataifa hayo ni ya asili. Siyo kama yetu ya kutengeneza. Wenyewe 1950s walikuwa tayari ni mataifa yenye miaka lukuki.
 
Paschal Mayala,naona unatafuta nafasi ya kuteuliwa...utaipata muda siyo mrefu hakuna kilichowahi kudumu milele chini ya jua
Wengi mnashindwa kumsoma Mwanafalsafa Mayala. Ukisoma katikati ya mistari uandishi haubabaishi. Yapo mazingira ya CCM kuendelea kutawala milele, lakini hakuna mazingira ya CCM kutawala milele. Kuna kani kinzani zitakapotokea basi zinauwezo wa kubadilisha kwendo wa chombo kinachosafiri njia nyoofu, kikasimama au kubadili mwelekeo. La pili, Kama ni umilele umehesabiwa sehemu moja tu! yaani Mungu! Kwa maana hiyo, milele ya CCM inaweza kuwa kitambo kidogo tu! Kumbuka miaka 1000 mbele za Mungu ni sawa na usiku wa jana Ukishakupita!
 
mkuu naona uminyooka unafuata mstali uleeee
 
kwa leo acha nikuite mpuuzi! milele ukiwa na maana hadi masihi anarudi au? huo ukweli wa huyu mtu ni upi? ukweli wa kuwa Saddam Husein ni wa Kuwait au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…