Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Asalam Ailekum wandugu,
Nahitaji mtaalam wa kunifanyia makadirio ya ujenzi wa nyumba hususan kupaua kwa kutumia bati. Nyumba ipo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Natanguliza Asante.

waelykum salaam warahamattullah wabarakattu,mkuu utakapohitaji fundi wa umeme usisite kunijulisha,Email yangu ni jumaramadhani8O3@yahoo.com AU 0718302132
 
Nilitafuta fundi kwa kuezeka akanipa makadirio ya around 8.1 million tukakubaliana akaanza kazi na gharama zilikuja hivi
Mbao treated za kupaua 2.8 M
Mabati ya maxcover 3.5 M
Kofia 360000
Misumari 140000
Ufundi 800000

Mbao zilibaki nyingi sana kiasi cha kutosha kupiga draft ndani vyumba vyote vitatu kwa hiyo kazi ya draft imebaki si kubwa .
Pamoja na gharama zote nilizotumia balance ilikuwa laki 4

Mkuu aspen habari yako,utakapohitaji fundi wa umeme usisite kunijulisha.Namba yangu ni 0718302132
 
Matunyengule. kwa vipimo vyako vya 7.2mt kwa 11mt. mbao ni 2kwa4=56, 2kwa36 na 1kwa8=15. bati za migogo mipana = 96, mabati ya kawaida =72. mabati yaliyo kama vigae =42

Mkuu tunashukuru kwa ufafanuzi, unaweza kunisaidia kunichekia na mimi kwa nyumba ya 9.5 m kwa 17 m hivi? nafikilia kutumia bati pana za ALAF nadhani gauge 28 zitatosha na idadi ya mbao
 
Matunyengule. kwa vipimo vyako vya 7.2mt kwa 11mt. mbao ni 2kwa4=56, 2kwa36 na 1kwa8=15. bati za migogo mipana = 96, mabati ya kawaida =72. mabati yaliyo kama vigae =42

Asante sana mkuu mavuno nyamanoro kweli upo sahihi mana haitofauti sana na makadirio ya fundi wangu hata hivyo Kwa kuwa upo Mwanza kama tutaafikiana unaweza kuchukua hii kazi. tuma picha kwenye matunyengule@gmail.com . Kwa sasa nipo Arusha Ila Bwana mdogo ndiye amesimamia kazi zote. hapo kwenye 2x3 ni mbao ngapi? Vile vile sahihisha namba yako ya cm, amepokea mtu mwingine ambaye hausiki kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Nyumba ya sqm120 si banda hilo? At least sqm 250!! Watu wanatishana sana bei za kuezeka!!
 
Hamna gharama za namna hiyo za upauz kwa nyumba zetu za kawaida huyu fundi aache tamaa za kijinga
 
Mafundi tuko mikoani nabeizetu ni nafuu sana. mi ni mtaaramu wa mambo hayo hii fani iko kwenye damu. sikama najifagiri. niko mwanza kwasasa namalizia kupaua hapa morogoro nitumie ramani kwa email nikupe makadirio. (kombaemmamuel42@gmail.com)
Nitakucheki. niko moro
 
Mi nimemaliza juzi juzi kupaua. Mabati 3.2m, mbao 2m na,Fundi ni kama 1.4m, vyumba vitatu vikubwa sana! Viwili ni master,sebule,jiko na stoo na ni Nyumba yenye coridor ndefu. Fundi na wasaidizi wake walimaliza kazi nda ni ya siku tano na nilisimamia mwenyewe.
Nashangaa watu wanaleta mabei makuubwaaa hapa ya kifisadi,acheni kutisha watu.

bati gani mkuu na alaf au kiboko, mbao ni treated au za kawaida
 
bati gani mkuu na alaf au kiboko, mbao ni treated au za kawaida

Kuna fundi mmoja hapa anaitwa mavuno nyamanoro ni mwaminifu na makadirio yake ni mazuri sana. Aliifanya kazi yangu vizuri kwa gharama ya laki 4 tu. Angalia picha hizi.
 

Attachments

  • Photo0958.jpg
    Photo0958.jpg
    46.6 KB · Views: 1,831
  • IMG-20140204-WA0007.jpg
    IMG-20140204-WA0007.jpg
    51.1 KB · Views: 1,959
  • IMG-20140205-WA0006.jpg
    IMG-20140205-WA0006.jpg
    47 KB · Views: 1,921
Last edited by a moderator:
Kuna fundi mmoja hapa anaitwa mavuno nyamanoro ni mwaminifu na makadirio yake ni mazuri sana. Aliifanya kazi yangu vizuri kwa gharama ya laki 4 tu. Angalia picha hizi.

Mkuu makadirio ya garama zote kuanzia msingi had hapo ilipofika ni kama shilingi ngap maana na mim nataka nianze ujenzi soon
 
Last edited by a moderator:
Jamani kupaua ni gharama kuna rafiki yangu alitajiwa jumla ya 17M (ufundi, mbao, bati-ALAF, ukubwa around 15x20). Hapahapa DSM, Akaomba apunguziwe walau 14, ikashindikana. Akaahirisha. Kama huyo rafiki yangu akiiona hii post, atampigia huyu jamaa mara moja.

Hahahaa, alienda kampuni ee? safi sana. maisha magumu inabidi wewe mwenyewe ufanye kazi siyo umpe mtu kazi halafu wewe mikono mfukoni. Toa pesa kidogo upate makadirio ya idadi ya bati/ vigae, na mbao treated, tafuta pa kuzinunua kwa bei rahisi nunua weka ndani, anza kufanya research ya fundi wa kupauwa-unaweza kumpata kirahisi kwenye site za watu wanakofanya kazi tena unaona na viwango vya kazi, mnanegotiate mnakubaliana. Sasa weweunatafuta fundi kwenye ofisi za watu waliofunga tai?!!!..ukimlipa si yeye anayepanda juu ya bati, kwa hiyo ujue anamlipa fundi na yeye anabaki na pesa mfukoni for nothing, mjini hapa!
 
Nyumba yangu ya vyumba 4 jiko sebule na dining, nilitumia sio chini ya 6M so ukiweka 6.5-7M itatosha kbs!
 
Mkuu makadirio ya garama zote kuanzia msingi had hapo ilipofika ni kama shilingi ngap maana na mim nataka nianze ujenzi soon

Kama una kiwanja anza msingi kwanza kwani msingi hauna gharama maalum kwa kuwa inategemea eneo ulipo na aina ya vifaa vya kutumia kama aidha msingi wa mawe au matofali. ila kwa Mwanza upatikanaji wa mawe ni mkubwa. Hata hivyo gharama za boma hadi kupaua hazitofautian sana. Kwa kifupi angalia gharama nilizotumia kuanzia msingi, boma, lenter, kupaua na magrill.
 

Attachments

Kama una kiwanja anza msingi kwanza kwani msingi hauna gharama maalum kwa kuwa inategemea eneo ulipo na aina ya vifaa vya kutumia kama aidha msingi wa mawe au matofali. ila kwa Mwanza upatikanaji wa mawe ni mkubwa. Hata hivyo gharama za boma hadi kupaua hazitofautian sana. Kwa kifupi angalia gharama nilizotumia kuanzia msingi, boma, lenter, kupaua na magrill.

Hujazungumzia tofali brother.
 
mkuu hata mm mwenyewe nimeshutuka kabisa nikasema hiyo bei nitawezaje na mm ingawaje ndo kwanza niko katika msingi wa nyumba kwa hali ya mtanzania wa wakawaida inakuwa ngumu best hiyo bei aliyoitaja huyo mkuu
Usiogope maana hata majibu yenyewe hayaja dadavua vizuri, mfano hizo bati za kisasa lazima ujue vipimo halisi na aina la paa sasa hapo sijui ametumia vipimo gani, pia ikijulikana aina ya paa itasadia kujua mbao kiasi gani na za size gani
 
Back
Top Bottom