usihofu mama, iko namna hii,
Nyumba ina sehemu kuu 3
sehemu ya kwanza ni msingi
sehemu ya pili ni boma na
sehemu ya tatu ni paa
kati ya hizo sehemu kuu 3 sehemu ya msingi na sehemu ya paa ni part 2 zinazohitaji umakini sana na zinakuwa na gharama kubwa kidogo,
sehemu ya paa ni part inayotumia skilled labour na ni sehemu yenye risk,
mbali ya swala la kiufundi, paa kwenye nyumba ndo linaweza kubadilisha nyumba iwe nzuri au iwe mbaya,
sasa natoa mfano tu wa nyumba ndogo ya vymba 3 vya kulala, sitting room, dining, kitchen na store jumlisha veranda zote za mbele na nyumba, chukulia mfano hiyo nyumba ina jumla ya ukubwa wa 140sqm,
kutegemea na aina (design) ya hiyo ramani na paa lake labda paa lina ukubwa wa 270sqm
mahitaji ya kupaua mfano wa hiyo nyumba yapo kama ifuatavyo.
1), mbao za dawa, hasa mbao nzuri ni za SAO HILL, kama bati litatumika la Industrial Trough (I.T) (hilo ni bati la migongo mipana, manake mbao za papi hazitakuwa nyingi kama mbao za makenchi, hapo kwa SAO HILL ukubwa wa nyumba kama hiyo (tunayo'assume) jaribu kutenga pesa isiyopungua 3m za mbao tu
2), Bati kama nilivyoainisha hapo juu ni I.T mfano na running meter ni 270 , kwa mabati ya ALAF ya IT gauge 28 wanauza kwa meter moja 13500/= kupitia agent, bila agent ni 13800/= manake ni kwamba bati tu hapo litagharimu karibia 4m
3), kofia na valley labda zipo jumla 40, kofia moja wanauza 21,000/= (hizo ni kofia zenye urefu wa 3m,
manake kofia na valley zinaweza kugharimu karibia milioni moja
4), mengineyo kama misumari ya kupigia makenchi, misumari ya bati, usafiri vyote kwa pamoja weka milioni 1
5), ufundi (tafuta local fundi) labda akakufanyia kwa bei ya 2m,
ila ukumbuke local fundi akija anaagalia nyumba imejengwaje na anabuni tu namna paa litakavyokuwa na si kwa kuffuata ramani inaonyeshaje, tarajia makosa mbali mbali hapo, ila pia na ushauri atakaokuwa anakupa local fundi ujue unaweza kukugharimu wewe baadae nakubaki kulalamika kuwa nilishauriwa hivi na fundi,
kwa maelezo zaidi ni'PM email yako ntakutumia sample za ramani na budget zake na ukipenda unaweza kuzitembelea kama upo hapa dar, au mwanza, arusha na moshi,