mkuu wewe ulijenga kwa gharama kiasi gani? itakuwa poa kama utaweka na picha ya hiyo nyumba,
labda tu niwatoe wasi wasi wanaotaka kujenga kwamba, kama una kiwanja na nikikubwa kiasi, na unaishi nyumba ya kupanga vyumba viwili, bora jenga hivyo vyumba viwili na upaue kwa bati la kawaida ili uhamie kwako, wakati upo kwako tafuta sasa hela ya kujenga nyumba unayoota kichwani.
shida moja ya client wengi wanapenda vitu vizuri lakini hawaafikiani na bei,
kwa mfano tu anayeishi kwenye nyumba yake masaki hana tofauti na anaishi kwenye kibanda chake cha vyumba viwili mpiji magohe,
mfano mwingine taa (bulb) kazi yake kutoa mwanga lakini kuna bulb ya jero na taa mpaka za laki 7, tofauti ya jero na laki 7 kwa kazi moja ya kutoa mwanga sijui unanipata?