Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

kati ya Ando na Alaf yupo ni mzuri zaidi? au unanishauri yup>
 
Ahsanteni kwa elimu. Kuna vitu nimechota naenda kuvifanyia kazi
 
Wakuu

Naomba ushauri wa level ya kuezeka paa. Fundi mwashi anasema zinatakiwa kozi mbili baada ya lintel, na muezekaji anasema zinatakiwa kozi tatu? Nani ni mkweli?

Fundi paa anadai kozi mbili zitafanya madirisha yasipendeze kwamba paa litaonekana liko chini. Fundi mwashi alojenga anasema nyumba iko juu tayari hivyo kozi tatu zitafanya nyumba isipendeze.

Kozi mbili baada ya linta ni sawa. Ya tatu itakuwa matungizi. Je ulieka kozi ngapi baada ya msingi?
 
Kuna fundi alinipigia hesabu ya bati 250 za futi kumi, nilinunua nusu nikamwambia aje tuanze ila ni lazima niwepo, akagoma. Nikamtafuta fundi mwingine kuja kufanya kazi, akazipiga zikapungua bati 11 tu. So nilipiga kwa bati 140 tu. Tofauti ilkuwa bati 110. Tumia strategy zangu, nunua robo tatu ya alizokwambia na simamia kazi kwa 100%. Utafanikiwa kuokoa gharama. Vinginevyo mafundi ni wezi sana.
 
nilifikiri nimestuka peke yangu
inategemea japo 3mil ni nyingi sana. Maximum ni kama 1.5mil hivi. 3mil kakupiga sana. Cheki na fundi mtaalamu wa bei poa, namba zake ni 0755297312. Msafirishe toka kahama. Ila ni mzuri na bei zake ni powa na yuko fasta sana
 
Wakuu Mimi Ni Fundi Wa Kupaua Nymba Za Aina Zote Na Bei Zetu Ni Nafuu Sana Naona zinazotajwa Hapa Ukilinganisha Na Zakwetu Ni Nusu Yake Kwa Kweli, Ningekua Na Uwezo Wa Kupost Picha Nilizopaua Ningeziweka Hapa, Napatika Morogoro Hapa Kila La Heri
 
inategemea japo 3mil ni nyingi sana. Maximum ni kama 1.5mil hivi. 3mil kakupiga sana. Cheki na fundi mtaalamu wa bei poa, namba zake ni 0755297312. Msafirishe toka kahama. Ila ni mzuri na bei zake ni powa na yuko fasta sana

safi sana
 
Chiwaso umenipa mwanga ni kubanana ila kama waishi mkoa huo huo kimbembe km kiwanja unacho mkoa mwingine utawadhibiti vipi?,ila nisaidieni ivi mafundi wa kichina wanaweza kutumika kujenga?
 
Last edited by a moderator:
Ukimuhitaji aliyenifanyia kazi hii kwa bei poa. Kupaua then nicheki.
 

Attachments

  • 1448021569519.jpg
    1448021569519.jpg
    72.1 KB · Views: 869
Huyo aliyekuambia kozi tatu yuko sahihi hasa kama nyumba ni kubwa maana ukishapiga fisherboard zinakua ziko karibu sana na madirisha (kama ni kozi mbili) na hivyo kutokuvutia sana.

Bt kama nyumba ndogo na paa haliendi sana juu basi kozi mbili ziko poa.
 
Mpe kazi bei zake ni smart
Kiongozi kama ni fundi ambae unamuamini na ungependa aendelee kupata kazi kutokana na ufanisi na uaminifu wake unaonaje ukiweka namba zake hapa jukwaani ili kila muhitaji kwa muda wake atawasiliana nae au wewe ni dalali wake hivyo unahitaji kila ambae anawasiliana nae lazima taarifa zianzie kwako ili upate 10% ?...Mimi nahitaji huduma za huyu fundi kutokana na recommendation zako hivyo tafadhali dondosha mawasiliano yake hapa ili niwasiliane nae kama hakuna shida katika hilo.
 
kupaua si gharama kiasi hicho kaka acha tamaa na kutisha watu labda gharama hizo ni kwa site za masaki na maeneo kama hayo au huko ni kutafuta faida za juu kabisa....hizo kazi tunafanya kila siku na bei ni za kawaida kabisa mf.. Nyumba ya vyumba 3 au 4 yenye vipimo standard itachukua mbao treated za hadi sh 1.5m, bati kama ni south around 3.5m na ufundi ni around 1-1.2m na tunafanya daily

Pm me your number Mkuu
 
16m x 12 zinaenda bati ngapi?

Kati ya Alaf na Nabaki zipi imara?

Approximately kama bati 215 pia mimi sijawai kufanya biashara na Araf ila najua Nabaki ni brand kubwa na wana garantii nzuri na vitu vyao vina ubora isipokuwa ni bei sana
 
Cjawahi kufanya kazi ya udalali na unfortunatel kazi ninayoifanya hainipi nafasi ya kujaribu kazi za udalali. Najua alinifanyia kazi nzuri na kwa bei ambayo sikuitegemea so shukrani yangu kwake ni kumtangaza yy na kazi zake.
0762017013
0754543341
 
wakuu kwa aliye na anuani za ando ( mahali ilipo ofisi na namba ya simu ) atusaidie.
 
Back
Top Bottom