Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Zumbemkuu na wadau wengine wa ujenzi:

Hii mada ya gharama za ujenzi imekuwa inakuja mara kwa mara kwenye ukumbi huu. Nami nimekuwa naifuatilia kwani ni shughuli ninayoipenda na ninajishughulisha nayo kwa muda mrefu.

Mimi ni mhandisi lakini siyo wa ujenzi, japo uchoraji na upigaji wa hesabu ndiyo shughuli yangu ya kila mara. Kwa kipindi kirefu nimekuwa natumia MS Excel kurahisisha makisio ya gharama za ujenzi. Na kwa kweli nimekuwa sichezi mbali sana na gharama halisi kwa kujenga mdogomdogo (yaani kwa kusimamia mwenyewe na mafundi wa mitaani maeneo ya Mwanza na Dar es Salaam.).

Muhimu ninajitahidi kupata ramani kamili ya nyumba ili kupata:

  1. Urefu wa kuta zote utakaosaidia kupata idadi kamili ya matofali
  2. Eneo la nyumba-sakafu (ground floor area) ili kupata gharama za sakafu, vigae, ceiling/gypsum board, idadi ya mabati nk.
  3. Eneo la kuta zote (wall area) ambalo linategemea unanyanyua kozi ngapi za matofali ili kupata idadi ya matofali, gharama za lipu, rangi nk.

Jedwali linasaidia kukokotoa idadi ya vifaa hivyo kirahisi baada ya kuweka vipimo hivyo vichache.

Kwa kutokana sasa na takwimu hizo kwa kutumia formular mbalimbali za civil engineering na uzoefu wa ujenzi, jedwali litakusaidia kupata makisio pia ya gharama kwa "automatic", yaani papo kwa papo. Fine tuning unaweza kuifanya, lakini tayari unakuwa na takwimu za kutosha hata ukimwita fundi muanze kujadiliana idadi ya vifaa vya ujenzi (matofali, ndoo za rangi, maboksi ya vigae, idadi ya mabati, gypsum board, nk) pia gharama za vifaa na gharama za ufundi kwa vile unakuwa una tatwimu zote muhimu na siyo kubishana tu na fundi.

Hili najua ni tatizo kubwa kwa watu wengi hasa wale wanaotaka kujenga nyumba kwa mara ya kwanza. Matokeo yake ni kutishika na kuacha kujenga au kupata mjanja akakuzidi akili na kuishia kununua vifaa vingi usivyohitaji na kama haupo site anaviuza! Aidha matokeo ya mkokotoo wa gharama hizi unaweza kukusaidia kupanga vizuri awamu za ujenzi kwa kulingana na uwezo wako ili ujenge nyumba yako bila taabu.

Nashukuru programu ya BURE ya Sweethome huwa hainiangushi, kwa muda wa nusu saa tu naweza kuchora ramani ya nyumba kubwa inayojitosheleza. Lakini hii ni kwa vile nimefundisha technical drawing na nimejifunza na kuitumia AutoCAD miaka ya nyuma. Hata hivyo ni programu rahisi kwa mtu yeyote kujifunza mwenyewe kama ana uelewa wa ufundi kidogo. Upungufu wake ni kutoweka paa kirahisi. Hivyo huwa nakomea kwenye kuta tu na kukweka furniture halisi kirahisi kabisa nipendavyo ili kupata feeling ya nyumba itakavyokuwa. Sweet Home 3D - Draw floor plans and arrange furniture freely

Kama una mchoro wa nyumba yako tayari, ingiza urefu wa kuta zote (ndani na nje) kwa utaratibu mzuri bila kukosea. Ni kujumlisha na kutoa tu. Kwa kurahisisha unaweza kujikumbusha hesabu za mzingo pia. Kisha kokotoa eneo la sakafu. Halafu mambo mengine ya kufanya ni kuingiza bei za ufundi/vifaa mbalimbali kulingana na eneo lako kama unaona zangu si sahihi. Jaribu kubadili takwimu kwenye maeneo MEUPE tu. Ama sivyo kama hujui kutumia Excel utaivuruga!

Nakiri kwamba haya makisio bado si kamili, kwa mfano sijaweka zege la msingi na makisio mengine yanaweza kuendelea kuboreshwa. Lakini kwa sasa nimeona nitoe mchango huu bure kwa jamii - eeh jamiiforums.

Upande wa msingi bado haujakaa vizuri na kwa kweli unategemea sura ya eneo na tabia ya ardhi unapotaka kujenga nyumba yako. Kazi hii hakikisha inafanywa kitaalamu. Kwa hiyo kwa upande wa msingi unaweza kuweka kozi 0 za msingi na hivyo kuondoa kabisa makisio ya msingi. Lakini kama unajenga msingi wa tofali tu, makisio ya matofali yanayohitajika utayapata.

Hapa nimeambatanisha:

  1. Ramani ya nyumba ikiwa na vipimo (ramani ambayo ilitolewa hapa na Zumbemkuu. Nimetumia ramani hii kugandamizia ili kuchora ramani hii(programu ya Sweet Home 3D inaruhusu jambo hili).
  2. Jedwali la MS Excel. NB: Jedwali la MS Excel ninalotoa hapa lina formular nyingi na nyingine nitazidi kuziongeza jinsi muda wangu unavyoruhusu, kwa hiyo pitia hapa kupata jedwali jipya au lililoboreshwa baada ya muda fulani.

****Nimeboresha tena awamu ya nne (Version 4)****:
- Ramani: Test house plan Vers3 - 12-2014-combined.pdf
- Jedwali_la_kukadiria_gharama_za_ujenzi_Test-House-Vers4.xlsx


mkuu cliff huu mchango wako nimeuleta na kwenye uzi huu,
itapendeza kama mods akina Invisible watapendezwa kuupandisha ujumbe huu kwenye ukurasa wa kwanza
 
Last edited by a moderator:
Asalam Ailekum wandugu,

Nahitaji mtaalam wa kunifanyia makadirio ya ujenzi wa nyumba hususan kupaua kwa kutumia bati. Nyumba ipo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Natanguliza Asante.


--------------------
Naongeza,gharama za kujenga paa zinategemea vitu vifuatavyo
1.aina ya paa -kama ni ya mgongo ama flat
2.roof complexity-kama uwepo wa kona nnyingi ,box zinatofautiana
3.angle ya mwinamo-
4.material tumika -mfano bati,udongo,zege,bati aina gani,vigae,biomass,nyasi....
5.gharama ya mtaalam-msanifu na fundi
6.eneo ilipo nyumba yako toka upatikanaji wa vifaa-
7.upatikanaji wa malighafi
Hivyo unapotaka kujua gharama ni lazima vitu hivi uvitafiti.Nawasilisha
 
kazi za watu hizo wamesomea chuo kikuu miaka minne....watu hao wanaitwa wakadiriaji ujenzi...kikristo wanaitwa quantity surveyors (QS)...NIKUPE NAMBA YAKE UMTAFUTE UONGEZE AJIRA KUTOKA ZILE MILIONI MOJA ZIFIKIE HATA MILIONI MOJA NA MOJA?
 
Mi ya kwangu ina vyumba 3, sitting room, dining, kitchen na vyoo viwil vya ndani. Nataka niweke bati ya m-south. Jumla ya garama itakuwa 2,540,000 tu.hizo garama ni kuanzia bati, mbao na ufundi.
Au kwa vile iko vikindu? Achwni kutisha watu ujenzi inawezekana.
 
Mi ya kwangu ina vyumba 3, sitting room, dining, kitchen na vyoo viwil vya ndani. Nataka niweke bati ya m-south. Jumla ya garama itakuwa 2,540,000 tu.hizo garama ni kuanzia bati, mbao na ufundi.
Au kwa vile iko vikindu? Achwni kutisha watu ujenzi inawezekana.

Mkuu naomba kujua wapi unanua hizo bati za msouth? na mimi nataka kuezeka mkuu
 
Mbagala lang3 opposite na NMB ATM kuna hardware pale utapata kwa bei poa
 
njoo ofisini kwangu nitakupa ushauri mim nauza bati za rangi na treated timber ni buguruni chama, call 0713283670
 
mkuu wewe ulijenga kwa gharama kiasi gani? itakuwa poa kama utaweka na picha ya hiyo nyumba,

labda tu niwatoe wasi wasi wanaotaka kujenga kwamba, kama una kiwanja na nikikubwa kiasi, na unaishi nyumba ya kupanga vyumba viwili, bora jenga hivyo vyumba viwili na upaue kwa bati la kawaida ili uhamie kwako, wakati upo kwako tafuta sasa hela ya kujenga nyumba unayoota kichwani.

shida moja ya client wengi wanapenda vitu vizuri lakini hawaafikiani na bei,

kwa mfano tu anayeishi kwenye nyumba yake masaki hana tofauti na anaishi kwenye kibanda chake cha vyumba viwili mpiji magohe,

mfano mwingine taa (bulb) kazi yake kutoa mwanga lakini kuna bulb ya jero na taa mpaka za laki 7, tofauti ya jero na laki 7 kwa kazi moja ya kutoa mwanga sijui unanipata?

Mkuu Zumbe, kuna ramani nimeipenda lakini ina Sq M 384, naomba nipe makadirio ya paa kwa mabati ya migongo mipana (I.T)
 
Mkuu Zumbe, kuna ramani nimeipenda lakini ina Sq M 384, naomba nipe makadirio ya paa kwa mabati ya migongo mipana (I.T)

Duu, mkuu hiyo nyumba ni kubwa si mchezo, loh, sijajua paa limekaa style gani ila hapo hazipungui running meter zaid ya 400, running meter moja ALAF ni Tshs. 13,500/=
 
Wakuu

Naomba ushauri wa level ya kuezeka paa. Fundi mwashi anasema zinatakiwa kozi mbili baada ya lintel, na muezekaji anasema zinatakiwa kozi tatu? Nani ni mkweli?

Fundi paa anadai kozi mbili zitafanya madirisha yasipendeze kwamba paa litaonekana liko chini. Fundi mwashi alojenga anasema nyumba iko juu tayari hivyo kozi tatu zitafanya nyumba isipendeze.
 
Wataalam wa hili jukwaa, kwa kuwa garama zimepanda za ujenzi, naaka kupaua nyumba yangu yenye ukubwa wa 16mx27m, nataka kutumia zile bati za kigae....hapo nahitaji mbao ngapi treated za 4x2, na 2x2? na pc ngapi za bati? fundi ninaye ila kwa wastani fundi anaweza kula ngapi kwa nyumba kama hio?
 
Bro, nimepaua recently nyumba ya 16.2 x 14.9 hapa DSM, SAOHILL treated timber ni gharama but ndipo nilipokwenda just for assurance, 4 x 2 nilichukua 180, 2 x 2 nilikosa but fundi alitaka 90 so nikaongeza 4x 2 mbao 50. Bati niiweka msouth IT 4 na niichukua 135 pcs but nadhani fundi alitaka kuniibia coz nilimbana site na siku ya mwisho zilibaki bati 28. fundi amekula 2 mil but ni msumbufu. So gharama ya mbao ilikuwa around 4.7mil, bati ni 7.2 mil,fundi 2 mil, mengineyo kama 0.5 mil. Wish u all da best
 
Jamani kupaua ni gharama kuna rafiki yangu alitajiwa jumla ya 17M (ufundi, mbao, bati-ALAF, ukubwa around 15x20). Hapahapa DSM, Akaomba apunguziwe walau 14, ikashindikana. Akaahirisha. Kama huyo rafiki yangu akiiona hii post, atampigia huyu jamaa mara moja.
jamani mim nauza mbao pia ni agent wa mabati kutoka kampuni tatu Alafu, Dragon na Afrina. bati la Alaf migongo mipana gauge28 mita ni 15340,na vigae kuna aina aina tatu 28gauge ya kwanza bei ni 15812 kwa mita moja,pili ni 16166 na tatu ni 17240.Dragoni 28 gauge migongo mipana ni 12000 kwa meter na vigae 13500 kwa mita na mbao ninazo.njooni tujenge pamoja msiogope
 
Kwenye MABATI NA KOFIA mafundi huwa wanaagiza nyingi kuliko mahitaji alafu wanakula timing ukizubaa wanakwiba bati ukikaba sana wanazipiga mbili mbili :frown:
 
Back
Top Bottom