Kwa hiyo fundi anapojenga msingi ni muhimu ajue uzito wa paa?
Mafundi tuko mikoani nabeizetu ni nafuu sana. mi ni mtaaramu wa mambo hayo hii fani iko kwenye damu. sikama najifagiri. niko mwanza kwasasa namalizia kupaua hapa morogoro nitumie ramani kwa email nikupe makadirio. (kombaemmamuel42@gmail.com)
Wadau nasikitika kuwataarifu kuwa huyu member mavuno nyamanoro alifariki dunia kwa ajali ya gari huko Biharamulo tarehe 15 January 2015.
May his soul R.I.P
Dah!! Nimestuka na kusikitika sana.Wadau nasikitika kuwataarifu kuwa huyu member mavuno nyamanoro alifariki dunia kwa ajali ya gari huko Biharamulo tarehe 15 January 2015.
May his soul R.I.P
Usiogope maana hata majibu yenyewe hayaja dadavua vizuri, mfano hizo bati za kisasa lazima ujue vipimo halisi na aina la paa sasa hapo sijui ametumia vipimo gani, pia ikijulikana aina ya paa itasadia kujua mbao kiasi gani na za size gani
Niko njiani kuanza dream house yangu. Architect anamalizia mchoro. By the time nafika kwenye paa najua gharama haitakuwa chini ya million 30 kupaua peke yake. Nyumba ninayoish ambayo nilipaua kwa vigae na mbao za dawa miaka 15 hivi iliyopita iligharimu karibu million 15. Ina vyumba vinne vya kulala, sebule 2, dining room, jiko, store na patios 2.
Ujenzi sio lelemama.
Kila mtu anajipimma kwa uwezo wake, wengine 7 tu zimetutosha kwa bati hizi za mnaziita za msouth!
mkuu wewe ulijenga kwa gharama kiasi gani? itakuwa poa kama utaweka na picha ya hiyo nyumba,
labda tu niwatoe wasi wasi wanaotaka kujenga kwamba, kama una kiwanja na nikikubwa kiasi, na unaishi nyumba ya kupanga vyumba viwili, bora jenga hivyo vyumba viwili na upaue kwa bati la kawaida ili uhamie kwako, wakati upo kwako tafuta sasa hela ya kujenga nyumba unayoota kichwani.
shida moja ya client wengi wanapenda vitu vizuri lakini hawaafikiani na bei,
kwa mfano tu anayeishi kwenye nyumba yake masaki hana tofauti na anaishi kwenye kibanda chake cha vyumba viwili mpiji magohe,
mfano mwingine taa (bulb) kazi yake kutoa mwanga lakini kuna bulb ya jero na taa mpaka za laki 7, tofauti ya jero na laki 7 kwa kazi moja ya kutoa mwanga sijui unanipata?
Ukipakuwa hilo faili lina kila kitu mkuu
Hahahahahaaaaa nimeishia kucheka tu, hawakujui ndio maana
Oya humu ndani! Mbona tunatishana sasa? Au humu wamejaa wenye nyumba hawataki watu wajenge zao?
"Nasikiaga tu baba mwenye nyumba sijawahi kusikia baba mwenye gari"
Wewe una nyumba?
Sina nyumba. MI NI BABA MWENYE GARI! Ila mwenye nyuma wangu hawezi kupanda nyumba aendapo kazini so huwa Nampa lift