Jasmoni Tegga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2020
- 12,624
- 24,751
Roho ya ^kwa nini^ siyo mbaya ikiwa positive. Kosa ni kijicho na wivu. Halafu kumwonea wivu mtu mwingine eti kwa the so-called mafanikio yake, ni kujishushia heshima na kujidhalilisha mchana kweupe, kwa sababu there is so much, even infinite possibilities, that every person can accomplish.Mwanzo wa kushindwa kwako huanzia kwenye roho ya kwanini na kijicho kwa waliofanikiwa
Acha kututukania nchi wewe!!! Wivu hauna chama, sawa!??? Kila mtu, regardless of jiografiko pozisheni yake, wivu, kijicho na chuki vinamkaa, endapo asipokuwa na roho ile nyingine ya utu na ubinadamu.Bongo(Tanzania) hii mtu akifanikiwa anachukiwa na chuki huletwa na wivu, watu wanapenda kuona fulani ameshindwa kufanya jambo kwa kukosa pesa au amefilisika basi hapo watatoa pole kinafiki huku moyoni wanafurahia Sasa itokee umefanikiwa jambo lolote utapigwa majungu, chuki na kuzushiwa kila jambo baya ili tu uonekane hauna maana kwenye jamii na sehemu za kazi
Kwa sehemu nimemsamehe Mond.. Kumbuka alikotokea na pengine mbele ya kayafa hakuwa na jinsi
Habari zenu,
Kwakweli kama wote mnavyojua kijana Diamond Platnumz ni moja ya vijana wapambanaji sana katika nchi hii,ni wale vijana waliotoka from the bottom huko chini kabisa na wakafanikiwa kupata mafanikio makubwa kutokana na juhudi binafsi.
Kinachonishangaza sasa ni trend kubwa ya Watanzania hasa vijana kumchukia huyu ndugu yetu hata bila sababu za maana kabisa badala ya kujifunza kutoka kwake.
Mbaya zaidi Watanzania tumejikita kumfanya ashuke pale alipo au aonekane hana chochote wala lolote, ukipita mitandaoni huko huoni hata wanaompongeza kwa mafanikio yake, wengi utaona wanapambana kumshusha inasikitisha sana, nakumbuka hata mimi mwenyewe kuna kipindi mkumbo huo ulinipitia kutokana na habari za mitandaoni, lakini nikagundua ni majungu tu.
Vijana wa Kitanzania tuache Majungu na fitina tuchape kazi, umbea hauna posho, hatuwezi kufanikiwa kwa kipiga majungu bila kupambana.
Asanteni.
Punguza mihemuko, hakuna sehemu nimeandika kuhusu chamaAcha kututukania nchi wewe!!! Wivu hauna chama, sawa!??? Kila mtu, regardless of jiografiko pozisheni yake, wivu, kijicho na chuki vinamkaa, endapo asipokuwa na roho ile nyingine ya utu na ubinadamu.
mkuu wewe sababu zinazokufanya umchukie daimondi ni zipi?Waswahili walishasema mkuki kwa nguruwe.
Asilimia kubwa ya hii mijitu ni minafiki.
Yaani unakuta jitu lenyewe linamchukia mtu fulani ila likiona kuna watu wengine na wao wanachukia mungu mtu wao yanaanza kubonga.
Unafiki na tabia yake ya kulazimisha ku-monopolise soko la muziki.mkuu wewe sababu zinazokufanya umchukie daimondi ni zipi?
Vijana wapambanaji wapo wengi.....Habari zenu,
Kwakweli kama wote mnavyojua kijana Diamond Platnumz ni moja ya vijana wapambanaji sana katika nchi hii,ni wale vijana waliotoka from the bottom huko chini kabisa na wakafanikiwa kupata mafanikio makubwa kutokana na juhudi binafsi.
Kinachonishangaza sasa ni trend kubwa ya Watanzania hasa vijana kumchukia huyu ndugu yetu hata bila sababu za maana kabisa badala ya kujifunza kutoka kwake.
Mbaya zaidi Watanzania tumejikita kumfanya ashuke pale alipo au aonekane hana chochote wala lolote, ukipita mitandaoni huko huoni hata wanaompongeza kwa mafanikio yake, wengi utaona wanapambana kumshusha inasikitisha sana, nakumbuka hata mimi mwenyewe kuna kipindi mkumbo huo ulinipitia kutokana na habari za mitandaoni, lakini nikagundua ni majungu tu.
Vijana wa Kitanzania tuache Majungu na fitina tuchape kazi, umbea hauna posho, hatuwezi kufanikiwa kwa kipiga majungu bila kupambana.
Asanteni.
maoni yako yahishimiweUnafiki na tabia yake ya kulazimisha ku-monopolise soko la muziki.
Yaani inshort anapambana kujifanya Ruge part 2.
How,kibiashara huwezi kulazimisha monopolization unless serikali iingilie kati ili uwe msambazaji pekee kama TANESCO au usambaze kilicho bora na kuua soko kwa wengine.Nachokiona kwako ni kutafuta justification ya chuki zako kama wengine sababu diamond anamiliki media moja Tz na sio media zote.hata kama ataamua kuwabania wasanii wengine kupitia media yake still kuna media nyingi wanazoweza kutokea bila kusahau social media ni accessible kwa kila mtu.Labda hamjajua moja ya indicator ya uvivu,umaskini wa mali na fikra ni kuchukia wenye mafanikio.Unafiki na tabia yake ya kulazimisha ku-monopolise soko la muziki.
Yaani inshort anapambana kujifanya Ruge part 2.
Uko sahihi kabisa,chuki husababishwa na wivu na kutojitambuaBongo(Tanzania) hii mtu akifanikiwa anachukiwa na chuki huletwa na wivu, watu wanapenda kuona fulani ameshindwa kufanya jambo kwa kukosa pesa au amefilisika basi hapo watatoa pole kinafiki huku moyoni wanafurahia Sasa itokee umefanikiwa jambo lolote utapigwa majungu, chuki na kuzushiwa kila jambo baya ili tu uonekane hauna maana kwenye jamii na sehemu za kazi
Wabongo roho mbaya sanaKaka yani watu hawapendi kuona mtu anaendelea kanunua gari 0 kilometres, ooo gari ya bei rahisi mtu hata baiskeli hana
Amemonopolise wapi?Unafiki na tabia yake ya kulazimisha ku-monopolise soko la muziki.
Yaani inshort anapambana kujifanya Ruge part 2.
Youngblood naomba niseme haya machache
Mti wenye matunda ndio hupopolewa mawe. Kuchukiwa ni ada ya mwanadamu. Hapa duniani kila kitu kina uwili! Kukiwa na wanaokupenda basi wanaokuchukia hawakosekani, kukiwa na wanaokusifia basi wanaokukosoa hawakosekani pia.
Watu duniani kote hufurahia mabaya ya mtu kuliko mafanikio yake na ndio maana habari mbaya za watu huvuma kwa kishindo kuliko habari zake nzuri.
Diamond kijana asiye na elimu lakini mwenye mafanikio makubwa naye ana mapungufu yake..hakuna mkamilifu la hata mmoja chini ya jua.
Chuki kubwa kwa Diamond ukiachana na ile ya wivu wa wasanii wenzake na vijana washindwa wengine. Imekolezwa na yeye kuambatana na KAYAFA. Mtu aliyetajwa kwa ukatili upendeleo na roho mbaya! Kumbuka ukiwa karibu na waridi nawe utanukia lakini pia ukiwa karibu na harufu mbaya nawe utanuka!
Uzuri wa Diamond anajitambua nakuitambua nafasi yake katika jamii hivyo hazipi nafasi chuki zinazomuandama kwa namna zote.. Ukimya ni silaha maridadi sana kwa haters. Kamwe usijaribu kujibishana na hater kwakuwa hiyo ndio nafasi pekee anayoitafuta kukuumiza na kupunguza machungu yake, mnyamazie azidi kuumia.
DIAMONDS ARE FOREVER!