Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Yeah. Hapo uliposema "weledi wa uokozi" ndiyo jambo la msingi sana.
Mtu hajakatazwa au kuzuiliwa kusaidia kutoa msaada wa kuokoa. Lakini huyo mtu anayetoa msaada wa uokozi kwamba yeye kwanza kama Mwokozi atakuwa Salama na yule Anayeokolewa pia atakuwa salama. Lengo litafanikiwa. Isiwe tu ni kazi ya kupangua matofali na kukata nondo kumbe kwa kufanya hivyo unasababisha mzigo mkubwa ushuke juu ya waathirika na kuwaponda, unaziba matundu yanayopitisha hewa kwa waathirika ndani ya kifusi au unagusa vitu vinavyoweza kusababisha moto kutokea n.k.
Nilitegemea kauli ya kwanza kwa Chalamila na Mliro ni kufunga ule mtaa immediately then rescue team iingie kazini.
 
Nani anayezuia matumizi ya majengo chakavu? Kulikuwa na stop oder yoyote kuhusu matumizi?
Kwa sasa sio wakati wa kumtafuta "mchawi" eti ni kosa la nani. Kwa sasa tungejikita ni kwa nini wahusika zima moto, Polisi, Jw na hata raia wenye uwezo na kazi ya uokozi hawajaonesha hawajitokezi juhudi zao??
 
Ndio akili za wafia dini wa jf. Halafu unampa jengo mtu kama huyu asimamie akiona fundi mtaalam kavaa kibaraghashia anamfukuza anaweka mvaa + , halafu jengo linajengwa kiwango cha chini
Kila sehemu unajitahidi kuchomeka itikadi zako mbovu za kidini zisizokuwa na kichwa wala miguu,ukiambiwa mmiliki wa jengo ni mwarabu utakuja hapa umeinamisha kichwa kwa aibu.

Na najua hadi sasa hapo ulipo unafanya juhudi za kumjua mmiliki kama ni muislam au mkristo ili uanze kuandika mada za mashambulizi.
 
Kihistoria (Uislamu)

1. Mimar Sinan (1490–1588)

Mhandisi na msanifu maarufu wa Dola ya Ottoman.

Alijenga majengo makubwa, kama Msikiti wa Suleymaniye na Msikiti wa Selimiye nchini Uturuki.



2. Ahmad Lahori

Msanifu mkuu wa Taj Mahal, India.

Alifanya kazi chini ya mfalme Shah Jahan wa Dola ya Mughal.



3. Zaha Hadid (1950–2016)

Msanifu wa Kiislamu wa Iraq na Uingereza maarufu kwa majengo ya kisasa.

Mifano: Guangzhou Opera House (China), Sheikh Zayed Bridge (Abu Dhabi).





---

Wa Kati ya Kisasa na Sasa

1. Adrian Smith

Msanifu mkuu wa Burj Khalifa, Dubai (jengo refu zaidi duniani).

Pia alihusika na ujenzi wa Jeddah Tower (Saudi Arabia, jengo linalotarajiwa kuwa refu zaidi duniani).



2. Fazlur Rahman Khan (1929–1982)

Mhandisi wa Kiislamu mwenye asili ya Bangladesh.

Aliunda teknolojia ya muundo wa "tube" iliyotumika kwenye Willis Tower na John Hancock Center (Marekani).



3. Norman Foster

Msanifu mkuu wa The Gherkin (London) na Apple Park (California).



4. Santiago Calatrava

Anajulikana kwa majengo makubwa yenye miundo ya ubunifu, kama The Oculus (New York).





---
Hii list yako mbona wengine umewatambulisha kwa dini yao na wengine umeandik tu majina yao.

Wewe ni mzima kichwani?
 
Hili ghorofa ni la zamani,halikujengwa miaka ya karibuni.Pia ni kosa kwa mwenye ghorofa na walioweka store kwenye juu ya hili ghorofa,kila kitu kinatengenezwa kwa uwezo wa kuhimili mzigo,kama gari la tani 2,ubebe mzigo wa tani 10,litauvunjika.Hata barabara zinajengwa kwa uwezo wa kupitisha gari zenye mzigo wa uwezo wa barabara.Tumia akili,kosa ni hao wanaoweka store kwenye nyumba za ghorofa juu,badala ya kukaa watu.
Kosa ni CCM kutokusimamia kanuni na taratibu za ujenzi wa majengo.Tumia akili chawa wa mama wenu.
 
JW ndio wanaingia sasa,baada ya masaa 5 tangu tukio litokee
kitaalamu hii ni sahihi kabisa katika response ya Majanga...huwezi kimbiza rasilimali zote at per kwenye eneo active la ajali ...unajuaje ajali nyingine inaweza kuendelea??Umejiridhisha vipi kama sio tukio "chambo" ili muingie kichwa kichwa ??
Tupunguze lawama pasipohitaji lawama.
Unaikumbuka Septemba 11 ??Jengo la kwanza limepigwa wote wakakimbilia pale halafu likapigwa na jengo la pili ...sasa baada ya hapo wahanga na waokoaji wote wakawa wahanga.
 
Hao watu kama wapo uko chini si wanaiva jamani wawapitishie ata maji na chakula
Umewaza mbali lakini shida yako au matamanio yako yanaweza kuwa ndo mauti kwao. Unawapaje maji na chakula i.e. unapita/unapitisha wapi? Halafu FAHAMU kwamba binadamu anauwezo wa kuishi bila chakula siku 5-7 halafu bila maji ni siku 3 (tatu). Sasa hapo hata saa 24 (siku moja) haijapita. Ila Asante kwa Huruma yako inaonesha UNAJALI.
 
kitaalamu hii ni sahihi kabisa katika response ya Majanga...huwezi kimbiza rasilimali zote at per kwenye eneo active la ajali ...unajuaje ajali nyingine inaweza kuendelea??Umejiridhisha vipi kama sio tukio "chambo" ili muingie kichwa kichwa ??
Tupunguze lawama pasipohitaji lawama
Kongole mkuu. Umetoa jawabu la Kitaalam sana :HYPERCLAPHD:. Wachache watakuelewa inaweza kuwa ni tukio "Chambo"
 
Back
Top Bottom