Kupunguza tatizo la ajira serikali iruhusu huduma ya kupokea pesa kupitia PayPal

Kupunguza tatizo la ajira serikali iruhusu huduma ya kupokea pesa kupitia PayPal

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani

Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.

Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.

Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.

Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.

Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.

Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake i tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.

Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga.
 
Umeongea point ya msingi sana na ukizingatia sasa hivi ni asubuhi.
Huwa naona wenzetu wanauza sana bidhaa zao online na sisi ndio wanunuaji pia, lakini sisi hatuuzi kwa sababu ya payment method tu. Kwa uhalisia kumbe hata mtu wa mwenge angeweza kuuza kinyago chake nje ya nchi kwa sababu ya urahisi tu wa njia za malipo.
 
Kwa uhalisia kumbe hata mtu wa mwenge angeweza kuuza kinyago chake nje ya nchi kwa sababu ya urahisi tu wa njia za malipo.
Ni kweli hata wenye maduka Mfano wanaouza bidhaa za ,batiki,viatu vya kimasai ,nk wangeweza uza online bila shida issue ni kuwepo urahisi wa kupokea malipo.Kwenye hili la kupokea malipo Tanzania tuko nyuma mno hatuwazi kuwa Kama kulivyo na machinga mitaani ,online pia mtu aweza fanya umachinga na akapata pesa na si lazima awe mfanyabiashara mkubwa kanaweza kuwa hata katoto ka darasa la tatu kakatengeneza game kakauza online kakajipatia pesa ya kununua askirimu
Wako wanunuzi Hadi wa mawazo ya biashara.
 
Usisingizie wazee mkuu.Vijana wengi sana serikalini na kiasi fulani bungeni.

Nikihesabu vijana walio na nafasi ya kutoa maoni yao yakasikilizwa ni wengi.Au una maana gani kusema wazee?
Tatizo walioko kwenye hizo nafasi ni wazee tu hawana wajualo wanaishi miaka ya 1980.
Yani kila nikipokea ela kuitoa napoteza zaidi ya 30% ya hiyo pesa hadi roho inaniumaga sana
 
Mtoa mada hebu eleza kwanini benki ya tanzania haijaruhusu mfumo wa kupokea pesa kwa njia ya PayPal ... ili hoja yako isiwe ya upande mmoja[emoji102]
 
Mtoa mada hebu eleza kwanini benki ya tanzania haijaruhusu mfumo wa kupokea pesa kwa njia ya PayPal ... ili hoja yako isiwe ya upande mmoja[emoji102]
Mimi Sijui Kenya hapo inaruhusiwa hayo majibu wanayo wenyewe.Kama yupo anayejua kwa Nini Tanzania hawaruhusu kupokea pesa kwa PayPal atuwekee sababu humu.Mimi.nimeeleza upande wangu ninaoujua
 
YEHODAYA, Jiulize hao kina Millard ayo wanalipwa kwa njia gani huko youtube, na uliza jamiiforums wanalipwa kwa njia gani kupitia adsense, usiache kutumia fursa ulizonazo kwa kusubiria majibu ya jumla ya serikali wakati wenzio wapo hapa na wanapata malipo unayozani hayawezekani.
 
Jiulize hao kina Millard ayo wanalipwa kwa njia gani huko youtube, na uliza jamiiforums wanalipwa kwa njia gani kupitia adsense, usiache kutumia fursa ulizonazo kwa kusubiria majibu ya jumla ya serikali wakati wenzio wapo hapa na wanapata malipo unayozani hayawezekani.
Hizo Ni kampuni zinatumia njia za kawaida za kupokea malipo.

PayPal inashuka kwenye individual level.Na kumpa malipo direct kwenye Simu yake ya mkononi au account instantly.Mfano dakika hii mtu aweza Mfano aweza jirekodi aka save kawimbo kake kwa mfumo wa Mp3 akauuza online na ndani ya sekunde Kama Ana PayPal akaanza kupata pesa immedeately mtu aki click kununua.
 
Back
Top Bottom