Kupunguza tatizo la ajira serikali iruhusu huduma ya kupokea pesa kupitia PayPal

Kupunguza tatizo la ajira serikali iruhusu huduma ya kupokea pesa kupitia PayPal

Itabidi serikali iangalie namna ya kwenda na wakati huu tuliopo vinginevyo tutaendelea kuwa vilaza wa ukanda huu tutakuja kustuka hata mrundi katupiku
 
Itabidi serikali iangalie namna ya kwenda na wakati huu tuliopo vinginevyo tutaendelea kuwa vilaza wa ukanda huu tutakuja kustuka hata mrundi katupiku
Kweli kabisa maana naona Rwanda kuna program walifanya wakipewa support na Ujerumani na DHL kwahiyo tukilala tunaweza kuwa nyuma ya wakati kwa ukanda huu wa Mashariki.
 
Itabidi serikali iangalie namna ya kwenda na wakati huu tuliopo vinginevyo tutaendelea kuwa vilaza wa ukanda huu tutakuja kustuka hata mrundi katupiku
Serikali.kupanua Soko la ajiri Ni pamoja na kuangalia Sera zake .Sera zingine zinafinya ajira badala ya kuipanua Kama hii ya kuzuia PayPal kupokea pesa inaminya ajira
 
Itabidi watu wahamie kwenye money gram na western union sasa
Ha ha ha unamuuzia kitu mtu online halafu umtake aende Ofisi ya money gram au Western Union akutumie pesa na neno la Siri!!!!!! Hupati mtu Kitu chenyewe ulichouza Mfano Cha dola tano!!! Nani akubali usumbufu huo wa kijinga .

Hanunui bidhaa yako na ukimpigia Simu hapokei
 
Mtoa mada hebu eleza kwanini benki ya tanzania haijaruhusu mfumo wa kupokea pesa kwa njia ya PayPal ... ili hoja yako isiwe ya upande mmoja[emoji102]
Serikali ndio ije ijitetee kwanini hawajaruhusu, hii si kazi ya raia mtaka huduma.
 
Hivi ni kweli njia za online transactions za mabank zimepigwa ban kama huu uzi unavyodai?
 
Serikali.kupanua Soko la ajiri Ni pamoja na kuangalia Sera zake .Sera zingine zinafinya ajira badala ya kuipanua Kama hii ya kuzuia PayPal kupokea pesa inaminya ajira
Kuna sera na taratibu nyingine zinatuchelewesha sana.
Mfano kupata passport uende na barua ya mwaliko. Sasa hivi kwa changamoto ya ajira unawekaje masharti magumu ya watu kwenda nje kutafuta?

Hili la PayPal sijui hata kama viongozi wetu wanaelewa kinachoendelea duniani. Kila mtu yupo busy na Stigler, Reli.
 
Tuko busy na Chadema,...
Habari ya uchumi siyo kipaumbele chetu

we kama unataka turuhusu paypal... Sema hivi SERIKALI ITUMIE PAYPAL KAMA NJIA MBADALA YA KUIDHIBITI CHADEMA....

Kesho asubuh BOT wanaruhusu mchakato
 
Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani

Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.

Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.

Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.

Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.

Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.

Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafs na ubunifu wake i tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.

Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga.
Ili chadema ipokee hela za mabeberu????? Sisiem oyeeeh
 
Ha ha ha unamuuzia kitu mtu online halafu umtake aende Ofisi ya money gram au Western Union akutumie pesa na neno la Siri!!!!!! Hupati mtu Kitu chenyewe ulichouza Mfano Cha dola tano!!! Nani akubali usumbufu huo wa kijinga .

Hanunui bidhaa yako na ukimpigia Simu hapokei
Hapo ndo shida inapoanzia ila nimeona eBay wanatumia Western union nikashangaa sana
 
Mimi nadhan serikali kupitia wizara ya fedha wangelisemea hili.
Mm nadhan wao wanawaza TRA mapato yatapungua.
 
Nilipenda kujua sababu ya msingi ya serikali yetu kuzuia hili....
 
Nilipenda kujua sababu ya msingi ya serikali yetu kuzuia hili....
[emoji1][emoji1]ufipa hawatasema hilo kamwe .. jua kuna mambo ya utakatishaji fedha ndiyo maana kupokea pesa kutoka nje sio rahisi hivyo kama tunavyojipangia sisi
 
Hapo ndo shida inapoanzia ila nimeona eBay wanatumia Western union nikashangaa sana
Aisee labda umuuzie mbongo mwezetu aliyeko nje .Uuzie wamarekani au wazungu wa ulaya kitu Chako online halafu umwambie akutumie pesa ya alichonunua kupitia Western Union it is a joke of a century
 
Nilipenda kujua sababu ya msingi ya serikali yetu kuzuia hili....
Nafikiri labda Serikali inapenda Sana raia wake Wawe watumia pesa za kigeni sio wapokea pesa za kigeni
 
Mimi nadhan serikali kupitia wizara ya fedha wangelisemea hili.
Mm nadhan wao wanawaza TRA mapato yatapungua.
Mapato yanapungua kivipi Mfano Mimi nimeuza pesa zimeletwa kwenye Akaunti au Airtel ,Tigo,TTCL ,Vodacom au ,halotel pesa kwa miamala yote nakatwa service charge ambayo Kodi ya TRA imo na kwenye miamala yote ya benki ninayofanya na pia faida zao wapatazo kwa biashara wanakatwa kodi.Na mimi.pesa ikiingia nanunua bidhaa na huduma mbalimbali zenye Kodi ndani naongeza mzunguko wa pesa na ongezeko la kodi
 
Back
Top Bottom