Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
serikali 1.zanzibar iwe mkoa tu au wilaya.nchi gani ina idadi ya wakazi sawa na jimbo la ubungo?

Wazenji wapo 1.5 million tu ! Lakini ni wajanja zaidi wamewekeza kwenye Ubunge Uwaziri na vyeo vingi tu wao ni wachache lakini Viongozi ni wengi sana ambapo wanalipwa na pesa ya Jasho la Tanganyika kisha wakishiba wanaanza kulalamikia lalamika ili kuwapumbaza watanganyika wasijitfmbue Kuwa Wanachunwa Kama buzi
 
Serikali tatu ili nasi tanganyika tipate pa kisemea mambo yetu watanganyika.
 
Laiti Pesa iliyotumika kuubembeleza Muungano ingetumika kujenga Hosptal Leo hii Nchi nzima tungekuwa na Hospt za Rufaa kila Mkoa Tunahitaji
Serikari moja tu wala si zaidi
 
Tamaa za madaraka na ubaguzi ni dhambi mbaya sana!tunahitaji serikali moja ya jamhuri ya muungano wa tanzania na mikoa yake miwili ya pemba na unguja kutoka zanzibar ikiungana na ile ya tanganyika!
 
Mkuu inawezekana watoto kwenye familia kuitisha kura ya maoni ili kuamua kuwa wanamtaka baba yao aendelee kuwa baba au la?
Mkuu vipimo vya DNA vimeshathibitisha kuwa yule aliyedhanwa kuwa wa watoto wawili si baba wa tatoto wawili bali ni baba wa mtoto mmoja......
 
Serikali 3 is the best option kwa upande wangu.

Serikali mbili ni kuendeleza kero za muungano na pia katiba ya Zanzibar ya sasa ni tatizo kwa muundo uliopo.

Serikali moja itakuwa vigumu ku-manage kuiendesha.

Serikali moja ndiyo kisasa! Dunia nzima watu wanahangaika kuungana nyie mnarudi-"reverse" ajabu!!
 
Serikali tatu au Muungano ufe basi. Zanzibar iwe na dola yake kama nchi huru. Muungano hauna faida yoyote zaidi ya u.pu.mb.avu tu wa kuwanyonya na kuwakamua wazanzibar. Wazanzibar msipokuwa huru mwaka huu hamtakuwa huru tena mpaka mwisho wa dunia. Komaeni mpaka kieleweke coz mnaweza tangaza uhuru wa zanzibar mwaka huu kama mko serious.
 
Muungano na wadanganyika mie basi,niachiwe nipumue,zanzibar kwanza.
 
Serikali tatu au Muungano ufe basi. Zanzibar iwe na dola yake kama nchi huru. Muungano hauna faida yoyote zaidi ya u.pu.mb.avu tu wa kuwanyonya na kuwakamua wazanzibar. Wazanzibar msipokuwa huru mwaka huu hamtakuwa huru tena mpaka mwisho wa dunia. Komaeni mpaka kieleweke coz mnaweza tangaza uhuru wa zanzibar mwaka huu kama mko serious.

huo ni mtazamo hasi wazanzibar wananyonywa nini? toa tu maoni yako,jwani walio wengi wamechoshwa na huu unaoitwa Muungano ambao kiuhalisia haupo.
 
Serikali 1 moja tu..ikishindikana hio basi kila nchi iende kivyake na muungano ufe tu..wapemba waanze kulipia ukaazi na kodi za ugeni kwenye nchi ya watu.
 
MAONI YANGU KWAMBA;Kiuhalisia 'HAKUNA MUUNGANO' ambacho kilifanyika mwanzo ilikuwa kwamba ni makubaliano kwamba TAIFA moja kuwa KARIBU na jingine kwa sababu za kiusalama;kwa kuwa sasa kila nchi inaweza kujitosheleza kiusalama,kiuchumi,kijamii nk basi kila nchi ijitegemee na MAANDALIZI yake ni kuwa na SERIKALI TATU
 
Serikali mbili ndiyo zimeonyesha kushindwa kabisa na kupelekea kufanya reform ya constitution ya Tanzania.Nawashangaa CCM wanaoendelea kung'ang'ania serikali mbili kama ni hivyo kwanini sasa kunafanya constitutional reform?

Bora kuingia gharama kuliko kuendeleza malumbano na manung'uniko kutoka kwa wenzetu wa visiwani. Solution ya kudumu ni serikali 3 au 1 ingawa moja haiwezekani sababu wazanzibari walishatia msumari kuwa no matter what serikali ya mapinduzi ya Zanzibar lazima iendelee kuwepo. Hivyo serikali 3 ndiyo mpango mzima.
 
napendekeza serikali tatu sb ni kama za jaji nyalali,jaji kisanga na jaji warioba lakini sb nyingine nikuwa wazanzibar wamegeuza tanganyika shamba la bibi kwa kutoa uraia wa tanzania ovyo kwa waarabu then wanakuja bara na kupata haki za kiraia kwenye kupata mali ya asili kama ardhi na huduma nyinginezo....yaani ndio deal kubwa inayofanyika zenj sasa hivi
 
Hivi CCM wanafuatilia matokeo haya? Ina maana kuwa Ccm nchi hii wamebaki asilimia 2 au kuna wanaccm wako kwa serikali 1 au 3? Unajua ukiwa na viongozi aina ya Nape na Mwigulu wanaoamini Ccm itatawala milele wanadhani wanaweza kuwaalazimisha watazanzania aina ya muungano wanaoutaka. Ni serikali 3 au patachimbika!
 
Hivi CCM wanafuatilia matokeo haya? Ina maana kuwa Ccm nchi hii wamebaki asilimia 2 au kuna wanaccm wako kwa serikali 1 au 3? Unajua ukiwa na viongozi aina ya Nape na Mwigulu wanaoamini Ccm itatawala milele wanadhani wanaweza kuwaalazimisha watazanzania aina ya muungano wanaoutaka. Ni serikali 3 au patachimbika!

Ni mamlaka kamili ya zanzibar au patachimbika.
 
Back
Top Bottom