Kurejea kwa Vitendo vya Uhalifu. Rais wangu Samia acha polisi wafanye kazi

Kuna wahalifu wengi sana wako mtaani saivi kutokana na maelekezo ya upelelezi kukamilika ndo mtu kushikiliwa au kupelekwa mahakamani. Tunaishi mtaani tunawaona
Unadhani polisi wakipewa rushwa na watuhumiwa kuna mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kweli?
 
Samia ndio chanzo cha tatizo, Yeye alifikiri Magufuli alikuwa njinga aliwachia vijana wafanye shughuri zao bila bughuza ili mradi hajipatie kipato na kujikimu, Samia alibomoa na kuwafukuza hao vijana kwenye maeneo walipokuwa ndiye alifanya makosa makubwa,hapo hakuna cha panya lord,ni vijana waliokosa chakula wananjaa kali,tunakoelekea hali itazidi kuwa mbaya zaidi hata wamwage askali 1000,Samia hahachie wamachinga wafanye biashara kama enzi za Magufuli ili tatizo litaisha lenyewe, lasivyo tunaenda kutengeneza vikundi vya kujilipua kama Somalia, Maana mwenye njaa ana cha kupoteza hata ukimpa elfu 10000 tu kwamba jilipue tu anaweza.
 
Rais anatenda kazi kama waziri wa mambo ya nje ambaye anatakiwa kupeti peti huko wakati uharifu ukishika kasi. Panya road wametoa roho uhai ya mwanafunzi wa chuo huko Kawe na waharifu waliojifanya wafuasi wa Mwamposa wakitokea kanisani lakini ghafla wanabadilika kuwa kama simba kurarua binadamu.......hii sio sawa....mharifu habembelezwi la sivyo kuna siku wataingia kwenye jumba la vitasa hapo watajua hawajui...panya road sio binadamu wa kawaida, wanavuta na kujidunga madawa kabla ya utekelezaji wa tukio na sio rahisi kuwatambua mpaka apatikane kijana ajiunge humo ili wapate taarifa sahihi.

Wakipanga kufanya tukio wanachagua maeneo angalau matatu moja wapo lazima watafanukisha ila wanaambatana na boda boda ambao huwezi kuwatilia shaka
 
Nitake radhi. Mie nakaa Songea. Dar nina ndugu na marafiki
CDF mstaafu Mabeyo, IGP mstaafu Sirro ndio walikuwa kiboko cha panya road na waliandika kitabu kwenye mapango ya Amboni, mapango Mwanza, Ruembe Kilosa, Dar es Salaam, MKIRU na Mnazi bay Mtwara
 
Kwa msingi wa andiko lako ulitaka wahalifu kama Hawa mapanya yaachiliwe. Hawa ni watoto wa wenye nafasi na wanafanyia hayo Kwa ulimbukeni wa wanaowalea !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…