UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,753
- 12,932
Nisikuchoshe na Usinchoshe, tusichoshane!
Maisha haya ya kitanzania yaliyojaa dhiki, umasikini, roho mbaya, husda, vijicho, masengenyo na masimango ingekuwa ngumu sana kutoboa kimaisha kama wengi wetu tusingepita kwa kina karumanzira ili kuwekwa sawa.
Kila mtu anafahamu kilichompeleka kwa mganga lakini ukweli ni kwamba watu ndiyo sababu ya watu kwenda kwa waganga!.
Mara nyingi watu wanaofanya twende kwa waganga kwa ajili ya tiba ya kuweka miili sawa ni MASHANGAZI & WAJOMBA (USHANGAZINI na UJOMBANI).
Hadi leo sijafahamu ni kwanini kwenye jamii hii ya watanzania kina-Shangazi na Wajomba mara nyingi kama si zote wamekuwa na husda sana kwa watoto wa ndugu zao,yaani wapo radhi wakaroge huku na huko ili kuona mtoto wa ndugu yao hafanikiwi,na mara zote hizo wanapokuwa wakihangaika na watoto wa ndugu zao huwa wamewasahau watoto wao kwamba wanaendelea kukua na umri kuzidi kusonga, mwisho wa siku wanakuja kushituka watoto wa ndugu waliokuwa wakiwapiga vita wamefanikiwa huku mitoto yao akiendelea kugombania ugali wa mazabe hapo makwao.
Tusingechukua hatua mapema za kwenda kwa Sangoma kuwekwa mili sawa bila shaka mashangazi na wajomba wangekuwa wametumaliza zamani sana.
Kuanzia kizazi cha miaka ya 1970 hadi 1990 ukikuta mtu hana Chale kwenye mwili wake basi yawezekana hakuwa akiishi Tanzania na kama aliishi Tanzania uenda hakuwa na Mashangazi au Wajomba.
Asilimia 90% ya kizazi cha Miaka 1970 hadi 1990 wamepigwa Chale na Chale nyingi zilizopigwa kwa watu hao ni kuwekwa sawa ili mambo yanyooke baada ya kuharibiwa na Ndugu zao hasa Mashangazi na wajomba.