Kusavaivu hadi leo hii wengi wetu bila kupigwa chale tusingetoboa



  • Sijawahi pigwa chale.
  • Sijawahi pelekwa kwa Mganga.
  • sijui mganga.

Nimezaliwa 1971
 
Miaka ya 80 nikiwa Old Moshi secondary, wakati wa kuoga tulikuwa tunachekana na wingi wa chale kwenye mwili. Sio mchezo, usipochanjwa hutoboi. Mtu anakuambia hajui kwa mganga ni Mungu tu Ila mwilini chale zimejaa, Ni uuuuungwana!!
 
Ungegegeda tuu, wala hakuna ambacho kingekuathiri baadae. Hizo ni imani za kinjinga zinazowasumbua wajinga, hazina matokeo yeyote ya maana kwao zaidi ya kuharibu miili yao, kujipotezea baadhi ya fursa nk.
 
Uchawi unaoongelewa kwenye biblia sio huu wa kiafrica na kitanzania mnaofundishana hapa
 
Unadanganya, Sidanganyiki, Usidanganye.

Hakuna kitu kama hicho Tanzania.

Chale haina uhusiano wowote ule wa moja kwa moja na yale uliyoyainisha kwenye muktadha wako..

Wacha upotoshaji.
 
...Sasa sisi Tunakuchoshaje ? [emoji57][emoji57]
 
Iyo ni Imani yako tu ya chale ss kwetu hatufanyi ayo mambo na tunasavaivu vzr kabisaa tena ni jamii kubwa tu ambayo haifanyi izo mila
 
Kwa upande wa, kutokuugua maladhi kama malaria nk, nakumbuka kwa Bibi yangu chai asubuhi ilikuwa ni dawa, hakuna chai kama chai, ni majani ya mitishamba, yanachemshwa, mnatia sukari mnapiga kama vile tanga wizi!
Leo hii nikisikia mtu anasema anaumwa malaria huwa nashangaa, Mimi naweza kukaa hata miaka 7 bila kuugua malaria
 
Mimi nakumbuka nilipelekwa kwa mganga nikiwa na miaka sita iv ila ilipfka zoezi la kupigwa chale nilikemea kwa kumtaja Yesu
Mzazi alisitisha kila kitu tukaanza safari ya kurudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…