Kuna watu wataleta nyuzi za kishamba sana eti haoni mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya miaka 5 au 10 ya Dr Magufuli. Sisemei Dr Magufuli hajafanya kazi , la hasha, Kajitahidi na kachapa kazi ila Tanzania ina watu mil 58 , naamini kuna watu Zaidi ya mil 1 wanaoweza kufanya vizuri kwenye kiti cha Urais Zaidi ya Dr Magufuli.
Wengi wanaomzunguzia Dr Magufuli kama mungu ni washamba Fulani ambao hawana exposure ya kutosha na elimu yao ni ya chini sana. Lakini tatizo lao kubwa ni IQ yao kuwa chini sana below the bottom line .
Tanzania kukosa viongozi wazuri ni matokeo ya Katiba mbovu na matumizi mabaya ya vyombo vya dola ambavyo vinatumika kuua Demokrasia ambayo ndio njia sahihi ya kuwaona viongozi wazuri. Wengi wanahofu hata wamekata tamaa ya siasa kwa sababu ya vitisho vya wenye mamlaka wasio jali haki za binadamu hata ndani ya chama cha CCM.
Hata Nyerere aliimbiwa nyimbo kama hizi na maadhi ya wapumbavu na wasio na akili lakini mwishoni mwenyewe Nyerere akaona hatoshi. Laiti angekubali vichwa kama kina Kambona leo Tanzania ingekua moja ya nchi zenye uchumi bora na Imara Africa Zaidi ya Nigeria na South Africa.
Ethiopia imetawaliwa na Mawaziri wakuu wawili wakatili wasio jail haki za binadamu ,wao waliamini katika maendeleo ya mkono wa chuma nao si wengine ni Hailemariam Desalegn na Meles Zenawi.
Katika vipindi vyao haki za buinadamu zilizorota sana, waandishi wa Habari wengi walifungwa na kuteswa , wananchi wengi walikimbia nchi yao , wapinzania wangi wakaishia gerezani . Pamoja na maendeleo waliyo yaleta kama barabara, Ethiopia airlines, etc mwisho chama chao kikakiri hawahitaji viongozi wakatili wanao angalia maenmdeleo bila haki za binadamu , wanahitaji demokrasia, uhuru wa kuchagua, uhuru wa kuongea na kusikilizwa etc.
Hawa wote waliimbiwa manyimbo ya kipumbavu kama wanayo imba kima kessy, msukuma, lijuakali,Sanga na wapumbavu wengine bungeni wasio jitambua kutokana na IQ zao kuwa chini sana.
Baada yah hapo chama kikamleta kijana msomi na mwelevu Abiy Ahmed ambaye ameleta neema kwa watu wa Ethiopia, maendeleo anasimamia, uchumi unaenda kwa kasi, hata kisasi na mtu, vyama vya siasa vinafanya siasa, wandishi wanaandika mambo yao kwa uhuru, walio kimbia nchi yao wamerudi,mahakama zinafanya kazi zao kwa uhuru, vyombo vya dola vinasimamia haki sawasawa bila kumwonea mtu etc.
Ni lazima watanzania tuendelee kuzipuuza sauti za hawa wachumia tumbo, wasio na akili. Tanzania inauwezo wa kutoa viongozi ambao wanaweza kubadilisha nchi hii ndani ya miaka michache, ikawa nchi nzuri, yenye uhuru, yenye uchumi imara, yenye kujali haki za binadamu, yenye demokrasia etc.
Kumbuka: Wale waliokua nondo Olevel wakiamini wao ndio wenye akili Tanzania, Siku wameenda shule kama Ilboru , Mzumbe Kibaha, wakashangaa wanashika mkia.
Pongezi sana kwa Dr Magufuli na Marais wote waliopita,
Dr Magufuli fanya kazi yako ,sepaaaaa.
Wapo wengi wenye maono na Taifa hili.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania wote Mil 58.
Mzuvendi Tabutupu salaam
Wanasaikolojia wanasema "mtu anayeongea kwa sauti ya juu katika mazungumzo, au mtu anayetumia lugha kali katika mijadala analazimisha watu waamini kua hakuna mbadala wa anachokiongea na pili amepungukiwa mapenzi na anao ongea nao ( Mfano mzuri ni pale unapokua na penzi changa uongeaji wake huwa tofauti na unapokua umemchoka uliyekua unampenda)
NAOMBA NIKUPE ELIMU HII ADHIMU UKITAKA ICHUKUE UKIGOMA HEWALA UKIAMUA KUNITUSI INSHALLAH...
MOSI
Makhalifa/Viongozi/Watawala ni uzao na si mafunzo. watu hawa ni uzao wanmwishoni mwa mwaka yaani Oktoba hadi Desemba pale, hawa haswa huletwa katika dunia hii kwa ajili ya kuongoza.
PILI
Makhalifa/Viongozi/Watawala ubora wao sasa huchagizwa na makuzi ambayo hujumuisha elimu, mazingira na hata maumbile (urefu, ufupi, unene au wembamba).
Nitafafanua kidogo mjeledi huu
ELIMU
Hapa Makhalifa/Viongozi/Watawala hupewa Muongozo wa kiuzoefu dhidi ya kazi yao Mfano wake ni sawa na kumchukia mtoto mwenye kipaji cha kuchora kisha ukamuingiza darasani kumnoa zaidi.
MAKUZI
Wanasaikolojia wanasema mtoto aliyelelewa katika mazingira ya ukatili katika kipindi cha mwaka mmoja hadi sita hawezi kuwa na upendo, wala huruma akikua.
MAZINGIRA
Wanasayansi ya jamii wanasema "asili ya mwanadamu haina uhalisia wake yenyewe, bali ni zao la mazingira yanayomzunguka" mazingira humfinyanga mtu kulingana na yenyewe na si kinyume chake.
MAUMBILE
Urefu; tabia za maumbile zinawahukumu watu wa aina hii kuwa watulivu katika MAAMUZI na wenye kujiamini, kitu ambacho kinawatengenezea marafiki wengi kuliko maadui.
Ufupi; tabia ya maumbile huhukumu kwamba watu wa kaliba hii hujihisi kudharauliwa na kutopewa kipaumbele katika maamuzi, hujikuta wakiwa na maadui wengi hasa wale wasiokua na busara katika ung'amuzi wa Mambo
Aidha hupenda kuchomoza katika kundi kubwa la watu ili kuonyesha uwepo wao, hivyo hujikuta wakilazimika kutumia nguvu nyingi kuthibitisha nia yao.
Unene + Urefu; tabia za maumbile huwahukumu watu hawa kama watu wavivu na wakatili sana, hupenda kutumia maumbo yao makubwa kupata vitu visivyo halali yao
Pia hujiamini kupindukia na kuingia kwenye kundi la watu wenye dharau na hii huwa nzuri au mbaya bi maana anakuachia kwa kukuhurumia au kwa kujua muda wowote akihitaji jambo Hilo atalipata
Wembamba + Urefu; vipenzi vya wanawake, wazinifu wapenda sifa, wasiojali hisia za mtu, hujihusisha pia na ukatili japo ukatili wao ni wa kihisia zaidi kuliko kimaungo.
Watulivu sana, wasio na papara katika Mambo, hujiamini sana, kitendo cha kupelekea kuwa na dharau, ni rahisi kutengemeza maadui wa siri kuliko wa dhahiri
Hivyo uzao ule wa Mwisho wa Mwisho Makhalifa/Viongozi/Watawala akikumbwa na tabia hizo za kimaumbile unapata matokeo sawia.
KWANINI HOFU KUWA DR. MAGUFULI HAKUNA KAMA YEYE?
Dr. JPM amefanikiwa kuwa wa pekee kutokana na yeye kuwa na combination nyingi sana ambazo zinaleta matokeo chanya na hasi yenye muelekeo chanya.
Nitahitimisha kwa combination hiyo;
Ni uzao wa mwisho wa mwaka, amekuzwa katika kutumia jasho katika kupata mkate, amelelewa kijasiri na katika kuamini katika yeye, amekuzwa katika mazingira ya dini, amefunzwa upendo wenye kuzingatia haki na utu, amepata elimu katika kiwango cha juu sana Dr. Of Philosophy PhD.
Kutokana na kimo chake rejea sifa tajwa hapo juu. Hivyo utaona ni namna gani inavyokua ngumu kukumbana na sifa zote hizi katika sehemu moja.
JE HAKUNA KAMA YEYE?
La hasha, wapo wanaoweza kuwa kama yeye au hata zaidi ya yeye bali lipo jambo moja lililothibitika kijamii kwamba "Ndege mmoja aliyepo mkononi ni bora kuliko wawili walio porini"
NINI KIFANYIKE SASA?
Hypothetically
Dr. JPM anatakiwa kabla ya kuchoka/kuchokwa na kuondoka atupe zawadi ya mfumo wa upatikanaji Viongozi
Mfanowe;
Liwepo Baraza la Usalama wa Taifa lenye wajumbe ambao hupatikana kwa kupandishwa vyeo kutokana na weledi na sifa zao tukuka kazini.
Mfano; amewahi fanya Jambo la kizalendo lenye tija kwa nchi hivyo kupata wadhifa fulani, Baraza hili litakua ni siri na automatic yaani wajumbe wake kutumikia kwa kiapo ambacho watakua chini ya watchdogs na adhabu yake atakapo kengeuka ni kuwa wiped out yeye na kizazi chake.
Baraza hilo litakua na wajibu wa kupitisha viongozi wa kada mbali mbali kwa njia ya Kura za Siri.
Usiku mwema.