Kusema hakuna mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya Dkt. Magufuli ni kukosa akili

Kusema hakuna mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya Dkt. Magufuli ni kukosa akili

Kapumbavu sana haka kazee, njaa zake eti kanataka katiba ibadilishwe.. utarudi kwenu sijui wapi unajua mwemyewe.
20200611_181914.jpeg
 
Kuna watu wataleta nyuzi za kishamba sana eti haoni mtu wa kuvaa viatu vya Urais baada ya miaka 5 au 10 ya Dr Magufuli. Sisemei Dr Magufuli hajafanya kazi , la hasha, Kajitahidi na kachapa kazi ila Tanzania ina watu mil 58 , naamini kuna watu Zaidi ya mil 1 wanaoweza kufanya vizuri kwenye kiti cha Urais Zaidi ya Dr Magufuli.

Wengi wanaomzunguzia Dr Magufuli kama mungu ni washamba Fulani ambao hawana exposure ya kutosha na elimu yao ni ya chini sana. Lakini tatizo lao kubwa ni IQ yao kuwa chini sana below the bottom line .

Tanzania kukosa viongozi wazuri ni matokeo ya Katiba mbovu na matumizi mabaya ya vyombo vya dola ambavyo vinatumika kuua Demokrasia ambayo ndio njia sahihi ya kuwaona viongozi wazuri. Wengi wanahofu hata wamekata tamaa ya siasa kwa sababu ya vitisho vya wenye mamlaka wasio jali haki za binadamu hata ndani ya chama cha CCM.

Hata Nyerere aliimbiwa nyimbo kama hizi na maadhi ya wapumbavu na wasio na akili lakini mwishoni mwenyewe Nyerere akaona hatoshi. Laiti angekubali vichwa kama kina Kambona leo Tanzania ingekua moja ya nchi zenye uchumi bora na Imara Africa Zaidi ya Nigeria na South Africa.

Ethiopia imetawaliwa na Mawaziri wakuu wawili wakatili wasio jail haki za binadamu ,wao waliamini katika maendeleo ya mkono wa chuma nao si wengine ni Hailemariam Desalegn na Meles Zenawi.

Katika vipindi vyao haki za buinadamu zilizorota sana, waandishi wa Habari wengi walifungwa na kuteswa , wananchi wengi walikimbia nchi yao , wapinzania wangi wakaishia gerezani . Pamoja na maendeleo waliyo yaleta kama barabara, Ethiopia airlines, etc mwisho chama chao kikakiri hawahitaji viongozi wakatili wanao angalia maenmdeleo bila haki za binadamu , wanahitaji demokrasia, uhuru wa kuchagua, uhuru wa kuongea na kusikilizwa etc.

Hawa wote waliimbiwa manyimbo ya kipumbavu kama wanayo imba kima kessy, msukuma, lijuakali,Sanga na wapumbavu wengine bungeni wasio jitambua kutokana na IQ zao kuwa chini sana.

Baada yah hapo chama kikamleta kijana msomi na mwelevu Abiy Ahmed ambaye ameleta neema kwa watu wa Ethiopia, maendeleo anasimamia, uchumi unaenda kwa kasi, hata kisasi na mtu, vyama vya siasa vinafanya siasa, wandishi wanaandika mambo yao kwa uhuru, walio kimbia nchi yao wamerudi,mahakama zinafanya kazi zao kwa uhuru, vyombo vya dola vinasimamia haki sawasawa bila kumwonea mtu etc.

Ni lazima watanzania tuendelee kuzipuuza sauti za hawa wachumia tumbo, wasio na akili. Tanzania inauwezo wa kutoa viongozi ambao wanaweza kubadilisha nchi hii ndani ya miaka michache, ikawa nchi nzuri, yenye uhuru, yenye uchumi imara, yenye kujali haki za binadamu, yenye demokrasia etc.

Kumbuka: Wale waliokua nondo Olevel wakiamini wao ndio wenye akili Tanzania, Siku wameenda shule kama Ilboru , Mzumbe Kibaha, wakashangaa wanashika mkia.

Pongezi sana kwa Dr Magufuli na Marais wote waliopita,
Dr Magufuli fanya kazi yako ,sepaaaaa.
Wapo wengi wenye maono na Taifa hili.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki watanzania wote Mil 58.
Kabla ya magufuli wengine nao walikuwa wanasema ccm haina rais anaweza kuongoza vile vile lakini magu katokea kwa hiyo hilo hata lisikupe tabu
 
Jana nimetizama Series moja hivi inaitwa Tom Clancy Jack Ryan season 2 inaelezea kisa kama hiki hiki cha utawala huu wa magufuli utadhani walikuja kutengenezea idea yao huku kwetu.

Yani mule mule spinnings, mauaji kufunga wakosoaji jela dah. Unajua hata udikteta una test tofauti tofauti kati ya taifa na taifa. Lakini udikteta ule wa kwenye ile filamu ni typical magufuli type.
 
Huu mkakati unalenga kuendeleza utulivu na utii kwa serikali kwa awamu ya pili ya JPM, ikumbukwe viongozi wengi hupoteza nguvu wanapoelekea kuhitimisha awamu zao.
Itakuwa faida pia kwa JPM kumteua mrithi anayemtaka kwa surprise, huku wapinzani wake wakiwa njia panda ya yeye kuendelea au kung'atuka
 
Rais anaye ondoka madarakani huwaga hana nguvu ya kumteua mridhi wake
Huu mkakati unalenga kuendeleza utulivu na utii kwa serikali kwa awamu ya pili ya JPM, ikumbukwe viongozi wengi hupoteza nguvu wanapoelekea kuhitimisha awamu zao.
Itakuwa faida pia kwa JPM kumteua mrithi anayemtaka kwa surprise, huku wapinzani wake wakiwa njia panda ya yeye kuendelea au kung'atuka
 
Mosi kabisa niwaambie ukweli kwamba mimi sio CCM na sitokua CCM maana watu wanaweza sema nampromote mkuu labda mimi ni ccm La hasha!

Mimi siipendi ccm ila namkubali jpm
Jpm ni kiongozi mzalendo kama alivyokua baba wa taifa, na ameweza kutekeleza mengi sana na kwa muda mfupi sana

Africa changamoto kubwa iliyonayo ni kukosa viongozi wazalendo na wanaopenda nchi zao ili ya kweli lakini Jpm ni mzalendo na anaweza kusimamia misingi ya utaifa na kulinda rasilimali zetu kwa nguvu zote

Nakumbuka awamu iliyopita jinsi madini na mikataba ilivyokua inasainiwa hovyo hovyo na kukawa na skendo hadi za kuuza twiga nje,mikataba mibovu ya madini ya asilimia 99 mwekezaji daah
Sidhani kama Tanzania itakaa ipate viongozi wazalendo kama Nyerere na Jpm ni wazalendo pure


Ameweza kutenda mengi sana miradi mikubwa na kila siku nawaambia watu kwamba nchi yoyote ile ili ifikie mafanikio na wakati wa kutekeleza maamuzi magumu lazima muumie kidogo ni ile mpitie kwenye kipindi cha mpito Transitional stage hata walter Rostow mwanauchumi na theory yake hii yenye kipengele hicho imeweza kuokoa na nchi nyingi zimeiga na wako mbali

Kwa karne hii utapata wapi kiongozi anayeweza kusimama na kulinda rasilimali za nchi kizalendo hivi?Haya magumu ya sasa ni ya muda tu pindi hii miradi ikiisha na hichi kipindi cha mpito kikipita hapo ndo mtaanza kuona matunda ya hii miradi ukweli nawaambia

Hiki ni kipindi cha mpito tu mateso ya muda baada ya miaka kadhaa hii miradi ikianza kuleta faida na tija mtashuhudia nchi itakavyosonga mbele kwa kasi ya 5g

Viongozi aina ya magufuli ni wachache sana na wanapatkana kwa nadra sana tujivunie huyu mtu

Lakini pia nashauri awaache wapinzani tu wafanye yao,wanasema kelele za chura hazimnyimi tembo kunywa maji,ruhusu ukosolewe ruhusu wafanye mikutano,waruhusu na waachwe na wale wasiumizwe waachwe tu maana ni haki yao kikatiba kukosolewa sio dhambi kukosolewa hakuuwi wala hakujeruhuwi wala hapachomi mwili bali hujenga na kuimarisha maana huwa naumia sana nikiona wanayofanyiwa wapinzani najisikia hasira na uchungu mwingi sana inakua kama vile wanatritiwa kama vile wao sio binadam hii sio fair hii area irekebishwe haki huinua taifa

Kwa kumalizia tu kwa kweli nchi ili iweze kufika mbali inahitaji kama mmepata
Kiongozi mzalendo na mleta maendeleo akae angalau miaka 20 asimamie na kukijenga hicho anachokifanya maana mfano jpm akiondoka 2025 atakuja mwingine na yake haya 2030 atakuja mwingine na yake yaani jenga bomoa jenga bomoa na ndo maana Africa haisongi mbele mauchaguzi kila siku na kila mtu anakuja na ajenda yake anaharibu ya yule aliyetangulia haiendelezwi

Sasa kwangu mimi nashauri katiba ingebadilishwa tu jpm atawale hata miaka 30 au hata 20 halat wabunge tuendelee kuchagua kama kawaida jpm ni mtu wa kipekee sana ukimuwaza hata katika ulimwengu wa roho na maombi ni mtu muhimu sana ni mtu ambaye hawezi akadanganyika katu alisaliti taifa lake ni mzalendo wa kweli anastahili atawale miaka hata 30 au hata milele
 
Back
Top Bottom