Kusema Majaji ni maCCM ndiyo kauli mbaya kuliko zote kwenye kesi ya Mh. Lissu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Mashahidi wa Mh. Lissu wanakiri kuwa Lissu amewaita majaji maCCM. Kauli hii ni mbaya sana kwa utawala wa sheria kwakuwa inahimiza watu wake na watu wengine wasioipenda CCM wasiende mahakamani kudai haki zao maana hawazipata kama wao sio wanaCCM; wajichukulie sheria mikononi mwao.

Kama hali itakuwa hivyo basi nchi haitatawalika na watu watahukumiana kwa hisia na dhana.

Kauli hii inalenga kuwatweza majaji na kuulemaza mhimili wote wa mahakama usifanye kazi yake kwa wafuasi wa chadema na wa vyama vingine ispokuwa CCM.

Kama Lissu, mwenyekiti wa chadema kweli kasema hivyo na kama chadema ndiyo imeasisi kauli ya No reforms no election kama wanavyosema mashahidi; basi Chadema inaweza kuadhibiwa kama chama kwa kupewa onyo au kufutwa kwenye daftari kwa kosa la kuhamasisha uvunjaji wa sheria.

Ni manoni yangu tu, msiyapige rungu.
 
Lissu ameongea ukweli halisi based on obvious trends and visible patterns, yuko sahihi kwa asilimia mia moja.
 
1. Uongo upo wapi?
2. Mbona mchakato wa kuwapata majaji ni uthibitisho tosha?
3. Kwamba hujui ujaji ni kama tuzo kwa mahakimu wanaofuata maelekezo dhidi ya wapinzani?
4. Kwamba hujui majaji wanajiingiza kwenye siasa muda mfupi baada ya kustaafu?
5. Mbona dunia yote inaujua huo ukweli?
6. Mbona kwa muda mrefu sasa wengi hawaendi mahakamani kwa sababu mifumo ya haki imeingiliwa na serikali ya ccm?
7. Semeni na simamieni ukweli kuliponya Taifa!
 
Majaji wa Tanzania huteuliwa na rais na rais hawezi kukuteua kutoka chama cha upinzani, hilo ni tatizo. Mara nyingi tumepinga mfumo wa majaji kuteuliwa na kula kiapo cha utii kwa rais na ndicho kumefanya kesi ya Lissu itumie mwaka mzima bila sababu za msingi zaidi ya kuyumbishwa na CCM.
 
Kwamba kusema majaji ni maccm ndio uhaini, machoko kweli pigwen miti hadi akili ziwarudi
 
Hujamsikia kwenye ushahidi wake akielezea kiundani kwanini majaji wanasemekana kuegemea upande wa CCM?

Alizungumzia kuanzia namna uteuzi wao ulivyo, namna kesi za upande wa upinzani zinavyoendeshwa kimihemko na mengine mengi.
 
J.inga kabisa
 
Mihimili ipo mitatu
1.Serikali,huchaguliwa na Wananchi(kuna pahala wanajichangua wenyewe kwa mabavu)

2.Bunge,huchaguliwa na wananchi(Kuna pahala wanaibiwa kura na Serikali na kupangwa na serikali)

3.Mahakama,hawa wanachaguliwa na Serikali na kufuata maamuzi ya serikali si tena chombo huru kwa 100%.Hata wao wanaililia Serikali..utwajua ni wazuri uwe na jambo lako na huna pesa za kutosha.
 
Mkuu mbona unapaka mafuta kwa jambo ambalo liko wazi?
Ukiwa na kesi ya kisiasa usitegemee kupata haki katika mazingira ya sasa.
 
Ebu niambie sababu ipi mahakama wakamkuta Tundu Lissu ana kesi ya kujibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…