Kusema Majaji ni maCCM ndiyo kauli mbaya kuliko zote kwenye kesi ya Mh. Lissu

Kusema Majaji ni maCCM ndiyo kauli mbaya kuliko zote kwenye kesi ya Mh. Lissu

kavulata hunaga akili kila siku nakwambia unamkumbuka Jaji Augustino ramadhani? Aligombea Urais kupitia chama gani? Pumbavu hunaga akili kila siku nakwambia wewe ni takataka
 
Kama Mahakama sio huru, ebu nijibu yafuatayo;
a) Kwanini Lissu aliendelea kuwa Afisa wa Mahakama Kuu akijiua si huru na Majaji wake ni Ma CCM?
b) Kwanini Lissu anakubali kujitetea kwenye Mahakama yenye Majaji Ma CCM na mashahidi wake akina Mnyika, Golugwa, Brenda Rupia na Heche wanakubali kutoa ushahidi kwenye Mahakama yenye Majaji Ma CCM?

Yeye anatimiza uwajibu wake huna akili
 
Alivunja Katiba? shida yenu nyinyi hamsomi katiba mnaropoka tu mnavyojisikia kuropoka bila kuzingatia sheria mama na sheria nyingine. Utawala wa sheria unakutaka kama unaona jambo sio sawa kwa mujibu wa katiba na sheria uende mahakamani ukalilalamikie jambo hilo. Kama majaji ni maCCM jambo hilo lililamikiwa wapi? na je, ni kosa jaji kuwa mwanachama wa CCM, chadema au ACT kwa mujibu wa sheria zetu?

Katiba gani hiki kijitabu takataka unafikiri kwanini wenye akili timamu wanataka katiba mpya
 
Mashahidi wa Mh. Lissu wanakiri kuwa Lissu amewaita majaji maCCM. Kauli hii ni mbaya sana kwa utawala wa sheria kwakuwa inahimiza watu wake na watu wengine wasioipenda CCM wasiende mahakamani kudai haki zao maana hawazipata kama wao sio wanaCCM; wajichukulie sheria mikononi mwao.

Kama hali itakuwa hivyo basi nchi haitatawalika na watu watahukumiana kwa hisia na dhana.

Kauli hii inalenga kuwatweza majaji na kuulemaza mhimili wote wa mahakama usifanye kazi yake kwa wafuasi wa chadema na wa vyama vingine ispokuwa CCM.

Kama Lissu, mwenyekiti wa chadema kweli kasema hivyo na kama chadema ndiyo imeasisi kauli ya No reforms no election kama wanavyosema mashahidi; basi Chadema inaweza kuadhibiwa kama chama kwa kupewa onyo au kufutwa kwenye daftari kwa kosa la kuhamasisha uvunjaji wa sheria.

Ni manoni yangu tu, msiyapige rungu.
Ni ukweli mtupu waipokee waitafakari na hawana chakufanya maana mamlaka yao ya uteuzi na budget zao za kuendesha shughuli zao lakini na Ulinzi wa majaji, vyote hivi vinatoka serikali kuu na hapa ndio uhuru wa mahakama ulipofia. Hawana Authority, Uhuru wa kibajeti, na ulinzi ili waweze kusimama katika yaliyo ya haki.
 
Lissu anakunyima usingizi
Haninyimi usingizi hata kidogo, kinachoninyima usingizi ni uharibifu wa huduma ambazo kodi yangu imehusika pia kuzijenga kwa manufaa ya wananchi wa kawaida kabisa wasiojua hili wala lile. Watu ambao lazima waamke na afya kisha watoke wakatafute ndio wapate chakula cha leo tu basi, kile cha kesho watakitafuta kesho.

Lissu au mtu mwingine haninyimi usingizi kwasababu sisi wote tunapita tu hapa lakini barabara tunazozijenga leo zitabaki na watakaobaki.

Hakuna haja ya kuleta mabadiliko kwa kutumia nguvu nyingi kwakuwa muda wa mabadiliko ukifika hata kama wewe huyataki yatakuja tu, hayazuiliki. Mahitaji ya watu yanazidi kubadilika hakuna mtu atazuia yasibadilike.

Kwanini ufe kabla ya muda wako ili ulete mabadiliko? Kufa kwa hivyo ni kufa kizembe, kwasababu hata bila wewe kuwepo mabadiliko yatakuja tu. Hata upigane na kuipata tz yote ikawa mali yako binafsi ni bure, maana siku za mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke sio nyingi; utaiacha tu.

Tupendane ili tusaidiane wakati tunayasubiri mabadiliko ya kweli, sio haya ya kutiana ngeo na kufungiana vyumbani kwa makosa ya kulazimisha mabadiliko.
 
Ni ukweli mtupu waipokee waitafakari na hawana chakufanya maana mamlaka yao ya uteuzi na budget zao za kuendesha shughuli zao lakini na Ulinzi wa majaji, vyote hivi vinatoka serikali kuu na hapa ndio uhuru wa mahakama ulipofia. Hawana Authority, Uhuru wa kibajeti, na ulinzi ili waweze kusimama katika yaliyo ya haki.
Duniani kote hakuna mhimili wa dola unaoweza kusimama peke yake ukiwa huru kabisa bila kuiegemea serikali iliyoundwa na chama fulani cha siasa. Serikali inaweza kufuta mahakama zooote na bunge na mambo yake yakaenda lakini sio kinyume chake. Kazi ya majaji haizalishi bidhaa yoyote ya kuuza wapate fedha walipane mishahara, ulinzi, matibabu, shule nk. Serikali lazima iwajengee majengo.

Anaekwambia kuna mahakama ambayo haina uhusiano na serikali tawala anafanya hivyo makusudi. Hata Lissu kama angekuwa Rais majaji wake angewatoa wapi, Ubelgiji, wanaCCM au wanaChadema wenzake?
 
Najua na ndio maana Check and balances ni muhimu, leo hii ni jaji gani anadhubutu kutengua maamuzi ya Raisi ? Kenya wametengua, Marekani ni ubabe wa Trump tumeona oda zikitengeliwa. Tunachozungumza zaidi ni kwamba je Jaji wa Tanzania anauwezo wa kutengua maamuzi ya Raisi, na je akitengua usalama wake ukoje ? Hii ni muhimu kwasababu amri jeshi wa nchi anajulikana ni nani na ndio mwenye kutoa go ahead za Kill orders ! Mlitaka Lissu asiseme ukweli tuzidi kusema katiba yetu ni nzuri ndio maana Nchimbi ameondoka madarakani kwa amani huku Nchimbi Mwenyewe akiwa haonekani wala kusikika wala kukabidhi ofisi ?
 
Back
Top Bottom