Kusema mtoto kulelewa na Bibi na Babu ataharibika ni Uongo kwa sababu tupo wengi ambao hatujaharibika

Kusema mtoto kulelewa na Bibi na Babu ataharibika, ni ukweli, kwa sababu wapo wengi ambao wameharibika

Mimi nawajua wengi ambao wamelelewa na Mama na baba na wameharibika.

Na wapo waliolelewa na bibi na babu wameharibika.

Hivyo kama utakuja kwenye suala la ukweli unaona kabisa ni kasumba
 
sio kila bibi analemaza mtoto ila asilimia kubwa hulea mtoto kimayai mtoto anakua wa hovyohovyo muhimu mzaz kama uko hai lea mtoto wako mwenyewe

Chunguza wabibi wanaolea watoto wao hovyo ndio walewale waliolea watoto wao hovyo.

Mama wa sasa ndio bibi wa kesho.
Baba wa sasa ndio Babu wa kesho.
 
Maneno Yako ni matamu masikioni na ushuhuda mzuri kwa wenye ufahamu!Hakika Babu na bibi ni walezi wa uhakika kama wakiwa na maadili Safi.Nimelelewa nao ,Babu na bibi kwa miaka mingi upande wote kwa mama na kwa baba .Niliposoma posti hii machozi yamenitoka nikumkubuka hasa bibi yangu mzaa mama alivyonilea kwa matumaini na faraja kubwa.Hakusoma Wala kujua kiswahili,ilikuwa na kubogoma kinyaki mwanzo mwisho!Nikipata tabu mwanzoni kuelewana nae,maana aliongea kinyaki Mimi kiswahili.Cha maana alichonifundisha ni kumtegemea Mungu wa kweli2Kuheshimu watu wote,3Kuwa mnyenyekevu4Kuondokana na majigambo na sifa za kijingajinga5Kufanya kazi kwa moyo wote Hapa nilipo Nina miaka53,Nipo fiti kwa kazi kama roboti.Njaa nasikia kwa majirani tuu Ahsante Mungu kwa kunipeleka huko!
 

Ukisema Watu wote unamaanisha jambo gani?

Kwa uelewa wako, Mama yako kama alishindwa kukulea wewe kwenye maadili ataweza kumlea mtoto wako(mjukuu wako)?

Wewe kama huwezi kulea watoto wako unategemea ukiwa bibi utaweza kulea wajukuu?

Ninawajua Watu wengi waliolelewa na Baba na mama ambao ni Wamebarikiwa.

Hata jamii unayoiona leo wengi wamelelewa na Baba na mama, haya tuambie kwa nini kuna mmomonyoko wa maadili?
 
Uandishi wako wa kitu kizima/ guadiani wakati wewe bado hujafika hata miaka 50, ni ishara kwamba alilelewa na bibi na babu huishi kuendena na umri wako, huo pia ni kuharibika. Kisaikolojia au kitaalamu huo ugonjwa tunauita........ mental fixation
Hoja Yako ni dhaifu sana.
 

Kuishi na Babu na bibi ukiwa Majanja unakuwa na maarifa ambayo kwa zama hizi ni nadra kuwa nayo.
 
Kusema mtoto kulelewa na Bibi na Babu ataharibika, ni ukweli, kwa sababu wapo wengi ambao wameharibika
Hakuna kitu hicho!Babu na bibi ni wazazi wa wazazi hivyo uzoefu wa kulea unawabeba!
 
Wewe Robert Heriel Mtibeli umeharibika.
Kuna tusi ulinitukana tulipopishana msimamo siwezi kusahau. Ni MTU asiye kua na malezi mema tu ndio angeweza kuandika lile tusi.

Hivi mimi nikitofautiana na wewe mtizamo lakini nikatumia lugha ya kukukejeli na dharau alafu wewe ukanitukana utakuwa na kosa?

Mimi namjibu mtu vile anavyokuja. Usitegemee uniletee mambo ya ajabu kwa kisingizio cha kupishana mtazamo alafu mimi nisikupe majibu ya ajabajabu. Sipo hivyo.
Nakupa kile unachonionyesha

Tusi kwa tusi
Hekima kwa hekima
Upumbavu kwa Upumbavu
 
Kasoro zipo tangu Adam hadi Manabii,ajenge hoja sio kuchambua Moja ya kumuudhi yeye tuu!
 
๐Š๐ข๐ฅ๐š ๐ฆ๐ญ๐ฎ ๐š๐ง๐š ๐ฆ๐ข๐ญ๐š๐ณ๐š๐ฆ๐จ ๐ฒ๐š๐ค๐ž ๐ค๐š๐ญ๐ข๐ค๐š ๐ฆ๐š๐ข๐ฌ๐ก๐š
 

Ni kweli
 
Kwa hiyo hapo ulipo unajiona hujaharibika.asee kweli kuishi kwingi kuona mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ