Kusema ukweli, wakoloni Tanzania yetu hawakuiibia kitu!

Kusema ukweli, wakoloni Tanzania yetu hawakuiibia kitu!

Kessy west,
Hayo Masalia waliyatoa wapi? Waliyakuta tumeyahifadhi kwenye Makumbusho tuliojenga huko Mtwara? Na tumeanza kusikia au kujua kuhusu hayo masalia lini? Na nani aliyefanya archeoligical survey na kuyachimba, kuunganisha vipande vipande na kuyatunza? Ni sisi?
 
Mwanzi1,
Fedha zote Wajerumani walitoa, na wao walipewa kama mkopo huko kwao na hawakuweza kurudisha shauri Vira Kuu ya Dunia ilianza, kumbuka Ujerumani wakikaa hapa chini ya miaka 30, sass hiyo ni michache sana kuweza kurudisha fedha wakiowekeza kwenye miradi yote waliojenga.
 
Hayo Masalia waliyatoa wapi? Waliyakuta tumeyahifadhi kwenye Makumbusho tuliojenga huko Mtwara? Na tumeanza kusikia au kujua kuhusu hayo masalia lini? Na nani aliyefanya archeoligical survey na kuyachimba, kiinganisha vipande vipande na kuyatunza? Ni sisi?
Unafahamu nyerere alikuwa na maana gani kuzuia shughuli za uchimbaji wa madini Tanganyika Na Akasema tutakuja kuchimba wenyewe Siku tukiwa tumeendelea??????
 
Barbarosa, Duh aisee badilika kidogo hao wakoloni bado wanatuibia tu. Angalia sehemu zote walizozichagua kukaa ni zenye mali sana wamechota toka enzi hizo na mpaka leo wanachota. Jifunue hilo blangeti na ubadili fikra[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina shaka kama unaijua vyema Historia ya Nchi hii,
 
CC mohamedi said na wenzake kina Bashiru na siasa za majitaka ya Leo

State agent
waasisi wa tanu na ccm ni watu wa mwambao ambao wengi walipokea dini ya mwarabu hawa ndiyo waliochangia kujaza propaganda kuwa wazungu wa ile dini ya magharibi kuwa ni wabaya sana. watu hawa wa mwambao wameshiriki sana katika kuandika vitabu vya kufundishia shule zetu, vitabu vyenye kujaa historia ya upotoshaji.

jiulize jambo moja: ni wapi waarabu walijenga japo mita moja ya reli? ukinitajia nidai buku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hujui ubaya wa wakoloni mpaka umri huo basi bora unyamaze
Jama huyo lazima ajitambue. Hajui kwamba Babu zetu na Bibi zetu walipelekwa utumwani kituo cha kuondokea kikiwa hapa Tz bandari ya Bagamoyo wakateseka sana na wengine wakafia njiani wakipelekwa ulaya na America kwenda kufanya kazi ngumu na ndo sababu wenzetu walitajirika sisi bado tupo na uchumi duni.

Actually tukiwa aggressive kama Africa nzima, twaweza kuwadai fidia watu wetu zaidi ya 70 Million walipata taabu sana. Unakuta nchi ambazo hazina Bandari kama Congo, Uganda etc watu walitembezwa kwa miguu huku wengine wakifia njiani mpaka wawafikishe Bagamoyo ili wapakiwe kwenda ulaya na kwingineko. Acha kabisa ni machungu sana.
 
Fedha zote Wajerumani walitoa, na wao walipewa kama mkopo huko kwao na hawakuweza kurudisha shauri Vira Kuu ya Dunia ilianza, kumbuka Ujerumani wakikaa hapa chini ya miaka 30, sass hiyo ni michache sana kuweza kurudisha fedha wakiowekeza kwenye miradi yote waliojenga.

Damage was done hata kama ni siku moja, huwezi kusema eti walikuwa wamekopa, hiyo haiwapi ruhusa ya kufanya msako wa nyumba hadi nyuma na kunyang'anya watu akiba ya vyakula vyao. Na hata hivyo unasema walijenga, swali ni walijenga kurahisisha maisha ya nani? Hakuna nchi yoyote duniani wakoloni walikwenda wakarahisisha maisha wa wazawa au kuwapa nafasi ya juu ya mkoloni. Kama ni kuiba walituibia sana na mpaka leo huwezi kuweka thamani walivyonufaika na Tanganyika. Kuanzia mazao yatokanao na maziwa makuu, mpaka pamba, katani, madini bila kusahau rasilimali watu.
 
Hapa kibwengu umenena waliotuibia watanzania ni miccm kuanzia awamu ya pili mpaka sasa. Ila acha roho mbaya hii miili yetu ni tutakufa wote hata umtangulize mwenzio kama ulivyokua unataka Lisu afe.
 
Kikiwo,
Ngoja nikuulize swali simpo sana, kama leo hii Meli ikipaki bandari zetu Dar, Tanga au Mtwara na kusema wanaotaka kwenda Ulaya au Uarabuni kuwa Watumwa wapande, unafikiri Meli zitaondoka tupu?
Isitoshe usisahahu utumwa una pande mbili, hata sisi tulikamata na kuuza ndugu zetu pia, hao waliuza babu zetu kwa Mkoloni utawadai fidia pia?
 
waasisi wa tanu na ccm ni watu wa mwambao ambao wengi walipokea dini ya mwarabu hawa ndiyo waliochangia kujaza propaganda kuwa wazungu wa ile dini ya magharibi kuwa ni wabaya sana. watu hawa wa mwambao wameshiriki sana katika kuandika vitabu vya kufundishia shule zetu, vitabu vyenye kujaa historia ya upotoshaji.

jiulize jambo moja: ni wapi waarabu walijenga japo mita moja ya reli? ukinitajia nidai buku.
Kitabu kipi kimeandika Mwarabu alijenga reli ?

ukikileta nachana kadi ya CHADEMA Hadharani.
 
Ngoja nikuulize swali simpo sana, kama leo hii Meli ikipaki bandari zetu Dar, Tanga au Mtwara na kusema wanaotaka kwenda Ulaya au Uarabuni kuwa Watumwa wapande, unafikiri Meli zitaondoka tupu?
Isitoshe usisahahu utumwa una pande mbili, hata sisi tulikamata na kuuza ndugu zetu pia, hao waliuza babu zetu kwa Mkoloni utawadai fidia pia?
Kwani na wewe uliuza ndugu zako?
 
Kama hujui ubaya wa wakoloni mpaka umri huo basi bora unyamaze
Ingetuonesha ubaya wao kuliko kumnyamazisha ndugu.
Leo tunahitaji uhuru wa kweli kuliko hata wakati tulipotaka waingereza waondoke.
Cha ajabu waliondoka kwa kupitia sanduku la kura ambalo mkoloni wa leo hataki hata kuliona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom