Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Kuna kikundi cha watu kinatumia nguvu Kubwa kuiaminisha jamii kuwa Mh. Mbowe alikuwa amelewa na hiyo ndo sababu ya kuvunjika mguu.

Kwanza ifahamike kwamba katika nchi yetu kulewa siyo kosa. Lakini pia kinacho shitua zaidi ni kwamba, wanao shabikia suala hili ni wale ambao siku za hivi karibuni walionyesha kukwaruzana na Mh. Mbowe.

Cha ajabu, mmojawapo anaye jaribu kuwaaminisha watu kuwa Mh. Mbowe alilewa ni spika Ndugai. Spika Ndugai akiwa kwenye kiti cha uspika kaongea kwa uhakika wote kuwa Mbowe alilewa, lakini kwa mtu anayemjua vizuri mlevi, kudondoka kwenye ngazi lazima angeumia kisogoni.

Hivi karibuni spika Ndugai aliingia kwenye majibizano na Mh. Mbowe, kwahiyo Ndugai kuongea haya anayoongea kunatia shaka Kubwa sana. Sidhani kama ana lengo zuri. Inawezekana ni kutimiza lengo lake kumchafua Mbowe ili asirudi bungeni kama alivyo Kwisha nukuliwa kuwa Mh. Mbowe hatarudi bungeni.
 
Ati yamepangwa na ikulu,aise,umeandika utumbo sana,anyway, TL ni dikteta ambaye akiishika nchi,tutaisha,na jamaa ukimwangalia,ni kama kichaa hivi.
Shilawadyu tu ikul ilijimix sembuse kub
 
Spika amesema kuwa ripoti wa madaktari wake imethibitisha Mbowe alilewa njwiiiiiii
 
Muhusika anafahamika tangu alipoanza kuongea sentensi ya kwanza.
 
Ni jambo la aibu ilihali polisi wanaendelea na kazi yao kama Moroto alivyoahidi ,Spika anatangazia umma kikao rasmi Bungeni " Nimetuma madakitari wangu kwa madaktari hospitali ... Mbowe alikuwa kalewa Chakari..." Tunaharibu umoja nabustawibwa taifa letu kwa sababu za hovyo.
 
TUSINGEMUAMINI,ILA ANGEMTAJA LISSU AU LEMA TUNGEMUAMINI.HAYA MAMBO YA KUPIGANA RISASI,KUTEKANA NA KUVUNJANA MIGUU HAYAMPENDEZI MUNGU HATA KIDOGO.
 
Shetani mara nyingi hushindana na haki kumbukeni kuwa Samson aliingia kwenye mtego kupitia kwa mkewe Delila.
 
Daktari anasema amevunjika mfupa wa "tibia" mtukuka mheshimiwa spika anasema hajavunjika tumwamini nani?. Chuki inayovuka mipaka hadi kwenye maradhi ni uzandiki. Ndugai alipokwenda kumtakia hali Mbowe ilikuwa ni kumpa pole ama kumdhihaki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika amesema kuwa ripoti wa madaktari wake imethibitisha Mbowe alilewa njwiiiiiii

Spika anatoka Chama gani na unadhani hao Madaktari nao watakuwa wanatokea Chama gani na je, ulitegemea waje na Ripoti tofauti na yao hiyo?
 

Siku zote Mwizi huwa na Kiherehere kingi tu cha Kujitetea na Unafiki uliokomaa kwa waliomshtukia au wale ambao wanataka Kumuadhibu akome.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…