Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Kushambuliwa kwa Mbowe: Polisi wasema wanaendelea na Uchunguzi, wapiga marufuku tukio hilo kufanywa la kisiasa. CHADEMA yamuhusisha Mchungaji Mashimo

Kuna kikundi cha watu kinatumia nguvu Kubwa kuiaminisha jamii kuwa Mh. Mbowe alikuwa amelewa na hiyo ndo sababu ya kuvunjika mguu.

Kwanza ifahamike kwamba katika nchi yetu kulewa siyo kosa. Lakini pia kinacho shitua zaidi ni kwamba, wanao shabikia suala hili ni wale ambao siku za hivi karibuni walionyesha kukwaruzana na Mh. Mbowe.

Cha ajabu, mmojawapo anaye jaribu kuwaaminisha watu kuwa Mh. Mbowe alilewa ni spika Ndugai. Spika Ndugai akiwa kwenye kiti cha uspika kaongea kwa uhakika wote kuwa Mbowe alilewa, lakini kwa mtu anayemjua vizuri mlevi, kudondoka kwenye ngazi lazima angeumia kisogoni.

Hivi karibuni spika Ndugai aliingia kwenye majibizano na Mh. Mbowe, kwahiyo Ndugai kuongea haya anayoongea kunatia shaka Kubwa sana. Sidhani kama ana lengo zuri. Inawezekana ni kutimiza lengo lake kumchafua Mbowe ili asirudi bungeni kama alivyo Kwisha nukuliwa kuwa Mh. Mbowe hatarudi bungeni.
 
Ati yamepangwa na ikulu,aise,umeandika utumbo sana,anyway, TL ni dikteta ambaye akiishika nchi,tutaisha,na jamaa ukimwangalia,ni kama kichaa hivi.
Shilawadyu tu ikul ilijimix sembuse kub
 
Spika amesema kuwa ripoti wa madaktari wake imethibitisha Mbowe alilewa njwiiiiiii
 
Muhusika anafahamika tangu alipoanza kuongea sentensi ya kwanza.
 
Ni jambo la aibu ilihali polisi wanaendelea na kazi yao kama Moroto alivyoahidi ,Spika anatangazia umma kikao rasmi Bungeni " Nimetuma madakitari wangu kwa madaktari hospitali ... Mbowe alikuwa kalewa Chakari..." Tunaharibu umoja nabustawibwa taifa letu kwa sababu za hovyo.
 
Ajabu sana. Sikuwepo kwenye tukio lakini naongea kama nilikuwepo. Ile amri ya kutoshuhudia uwongo sijui watu huwa tunaionaje?

Nakumbuka vibaka wengi huvamia watu waliolewa kuliko wale ambao hawajanywa kilevi! Watoto wao wanaona namna mnavyowasingizia na mnavyotukania wazazi wao.

Wananchi wanaona mnavyojipendekeza ili mpate nafasi. Mfano mdogo tu - je, Mbowe angeamua aseme kwamba mmojawapo wa aliyemvamia alikuwa Mheshimiwa Silinde - Stori yake ingekuwaje?
TUSINGEMUAMINI,ILA ANGEMTAJA LISSU AU LEMA TUNGEMUAMINI.HAYA MAMBO YA KUPIGANA RISASI,KUTEKANA NA KUVUNJANA MIGUU HAYAMPENDEZI MUNGU HATA KIDOGO.
 
Shetani mara nyingi hushindana na haki kumbukeni kuwa Samson aliingia kwenye mtego kupitia kwa mkewe Delila.
 
" Sasa jambo lenyewe (Mbowe kuvamiwa) lina hadithi nyingi ya jinsi lilivyotokea maanake inasemekana jana mpaka saa sita usiku alikuwa mahali, inaniwia ugumu kusema chochote kwa hatua hii lakini...eeh! niseme tu kwamba msichukulie kama watu wanavyoongea, watakaosema hali halisi ni vyombo vya usalama na niwaombe vyombo hivyo vitoe taarifa mapema iwezekanavyo, waeleze ilitokea nini isiwe ni kazi yangu...wanavyozidi kuchelewa hadithi zinakuwa nyingi "-Spika Job Ndugai.

Siku zote Mwizi huwa na Kiherehere kingi tu cha Kujitetea na Unafiki uliokomaa kwa waliomshtukia au wale ambao wanataka Kumuadhibu akome.
Daktari anasema amevunjika mfupa wa "tibia" mtukuka mheshimiwa spika anasema hajavunjika tumwamini nani?. Chuki inayovuka mipaka hadi kwenye maradhi ni uzandiki. Ndugai alipokwenda kumtakia hali Mbowe ilikuwa ni kumpa pole ama kumdhihaki!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika amesema kuwa ripoti wa madaktari wake imethibitisha Mbowe alilewa njwiiiiiii

Spika anatoka Chama gani na unadhani hao Madaktari nao watakuwa wanatokea Chama gani na je, ulitegemea waje na Ripoti tofauti na yao hiyo?
 
Daktari anasema amevunjika mfupa wa "tibia" mtukuka mheshimiwa spika anasema hajavunjika tumwamini nani?. Chuki inayovuka mipaka hadi kwenye maradhi ni uzandiki. Ndugai alipokwenda kumtakia hali Mbowe ilikuwa ni kumpa pole ama kumdhihaki!

Sent using Jamii Forums mobile app

Siku zote Mwizi huwa na Kiherehere kingi tu cha Kujitetea na Unafiki uliokomaa kwa waliomshtukia au wale ambao wanataka Kumuadhibu akome.
 
Back
Top Bottom