Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Yataisha tu!Kumbe Bado haya Mambo yanaendelea?
Mi nilidhani yalikemewa yakaachwa..
Kuna Kiongozi wa Kisalafi Abu Fadhil kassim Mafuta huyu jamaa Ndo Kiongozi wao na wanamuamini sana kwa miaka mingi..Mitafaruku Mingi naona kama yye ndo aanzisha..
Ila waislamu wangepunguza Vurugu za wao kwa wao..
Kwa mfano Qassim Mafuta huyu naye ni changamoto. Anawagawa sana watu. Kazi yake ni kuraddi tu watu. Juzi kati kamraddi Mufti Menk kwamba msimfuate. Sasa yeye ni nani?
Ndiyo maana aliulizwa; ukitoa kuraddi watu, kufuga kwako ndevu na kuvaa kanzu fupi una kipi cha maana ulichokiacha kwenye jamii? Hana! Yeye badala ya kufundisha elimu yeye anafundisha misimamo na kisha anawagawa watu. Qassim Mafuta ni mfitinishanaji tu! Hamna Sheikh pale.
Jamii ya Kiislamu hapa Tanzania licha ya kwamba walifahamu kuwa wana ikhtilafu baina yao ila waliheshimiana kwa tofauti zao. Ila tangu lilipozuka kundi la salafi/Answar sunna kila kitu kikawa tofauti, zile ikhtilaf wao wamezifanya aqida/itikadi na matokeo yake wanaleta vurugu kwenye jamii.
Laiti kama mimi ningelikuwa na mamlaka ningelipiga pini kundi la Salafi kama walivyofanya Misri. Misri ukiwa na usalafi kama wa Qassim Mafuta wanakukamata ndani.